Mtuhumiwa wa Dawa za Kulevya anaswa akiwa amejibadilisha muonekano na kuwa kama mzee

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
IMG_20160821_174027.jpg

Polisi nchini Marekani wamemkamata mtoro mmoja baada ya kugundua kuwa alikuwa akidanganya kuwa yeye ni mtu mzee.

Polisi walizingira nyumba moja huko Massachusetts na kumuamrisha Shaun "Shizz" Miller atoke nje.

Kisha akatoka nje akiwa amejibadilisha na kuwa kama mtu mzee, lakini wakati polisi waligundua kuwa alikuwa ni yule walikuwa wakimtafuta mwenye umri wa miaka 31 walimkamata.

Amekuwa mafichoni tangu ashtakiwe kwa kuhusika kwenye ulanguzi wa madawa ya kulevya mwezi Aprili.

Wakati polisi walisaka nyumba hiyo walipata bunduki mbili na karibu dola 30,000 pesa taslim

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom