Binti wa miaka 25 akamatwa na Gramu 448.12 za dawa za kulevya Tegeta kwa Ndevu

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,206
4,696
Pongezi kwa kazi nzuri iliyofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Madawa ya Kulevya nchini chini ya Kamishna Jenerali James Kaji.

Maria Edson Mtambo ni Mfanya Usafi ambaye amekamatwa na Madawa ya Kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa gramu 448.12 akiwa maeneo ya Tegeta Kwa Ndevu, Jijini Dar es Salaam.

Alizificha ndani ya kifurushi cha Vitabu viwili akijiandaa kuzisafirisha kwenda nchini India kwa Mpenziwe.

FB_IMG_16012994770588802.jpg

——————

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema kuwa katika tukio la kwanza, mnamo Septemba 17 mwaka huu Mamlaka hiyo ilimkamata Mary Edson Mtambo (25) kabila Mnyiha na mkazi wa Tegeta kwa Ndevu ambaye alikua akisafirisha vifurushi vya vitabu viwili ambavyo ndani yake kuliwekwa unga wa dawa za kulevya aina ya Heroin wenye uzito wa gramu 448.14.

Kaji amesema kuwa, binti huyo anajishughulisha na kazi za usafi huko Tegeta na aliyekuwa anamtumia Vifurushi hivyo vya dawa za kulevya ni mpenzi wake ambaye ni raia wa kigeni.



=======

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama imefanikiwa kukamata takribani kilo 343.7 za dawa za kulevya aina ya Mirungi na Dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 448.14 katika matukio mawili tofauti kwa mwezi Septemba 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema kuwa katika tukio la kwanza, mnamo Septemba 17 mwaka huu Mamlaka hiyo ilimkamata Mary Edson Mtambo (25) kabila Mnyiha na mkazi wa Tegeta kwa Ndevu ambaye alikua akisafirisha vifurushi vya vitabu viwili ambavyo ndani yake kuliwekwa unga wa dawa za kulevya aina ya Heroin wenye uzito wa gramu 448.14.

Kaji amesema kuwa, binti huyo anajishughulisha na kazi za usafi huko Tegeta na aliyekuwa anamtumia vifurushi hivyo vya dawa za kulevya ni mpenzi wake ambaye ni raia wa kigeni.

Aidha amesema kuwa katika nyakati tofauti mkoani kigoma iliwakamata watuhumiwa George Justine Mathew (21) kabila la Muha na mkazi wa Kigoma mjini akiwa na maboksi mawili yenye jumla ya kilo 16.05 za majani makavu ya dawa za kulevya aina ya Mirungi katika eneo la kutuma na kupokea vifurushi, Posta Mkoani Kigoma.Aidha walimkamata Alex Benedict Ntiruka (31) kabila la Muha wa Kasulu Kigoma akiwa na maboksi mawili yenye jumla ya vifurushi nane vya majani makavu ya dawa za kulevya aina ya Mirungi yanayokadiliwa kuwa na uzito wa kilo 16, na alikuwa akifanya maandalizi ya kuyatuma katika eneo la Posta, Kigoma.

Jenerali Kaji amesema kuwa Mamlaka hiyo na Serikali wapo makini wakati wote na yeyote anayejihusiha na biashara hiyo atakamatwa na sheria itafuata mkondo wake.

Amesema kuwa wameendelea kufanya uchunguzi na kubaini mtandao wa usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Mirungi nje ya nchi na kufanikiwa kuwakamata washiriki wa mtandao huo na watafikishwa mahakamani.

Pia amewashauri vijana kuwa makini na mahusiano na raia wa nchi za Magharibi ili waepukane na majanga hayo na amewashukuru wasafirishaji wa vifurushi wakiwemo Posta na DHL kwa ushirikiano katika vita ya dawa za kulevya.
 
Back
Top Bottom