Kutana na ‘Liu Zhaohua’ mgunduzi wa dawa za kulevya

Adil_101

Senior Member
Jul 26, 2022
110
339
(The Most Intelligent Criminal In History?)

UZI

Anaitwa Liu Zhaohua, mshindi wa 2 katika mashindano ya somo la chemistry akiwa shule, aliyejifunza mwenyewe kutengeza madawa ya kulevya ya methamphetamine, kwa purity ya 99%

Mpaka sasa, wauza unga kibao bado wanadadisi ni kwa vipi Liu aliweza kugundua formula ya kutengeneza methamphetamine yenye ubora wa kiwango cha 99%.

Kwake ku-crystallize tani 1 ya methamphetamine kwa siku haikuwa kesi, na alikuwa akiuza mpaka tani 5 kila siku za unga huo.

Kinachowasumbua wana-chemia wa leo ni kuwa, Liu alijifunzia wapi kutengeza mchanganyo huo!?, aliwezaje kutengeneza madawa yenye quality ya juu!? na huku mchakato wa utengenezwaji wa madawa hayo (Process yake) ilikuwa ni rafiki kwa mazingira na ‘pollution-free’ kabisa.

IMG_20230413_185846.jpg

Aliandika Forest Harris kuwa “Until today, there is not a single drug maker in the world, including some professor-level ones who can reach the overall quality (purity, crystallization, and appearance) of the meth produced by Liu Zhaohua...

…They may have no problem with the theoretical aspects, but the process technology they master cannot do it”.

Liu alizaliwa March 5 ya 1965 kule Fu'an, Fujian, China. Inasemekana kuwa, alikuwa ni mwenye akili sana tangu udogo wake.

Alilipenda somo la Chemistry tokea akiwa mdogo, muda mwingi ambao alikuwa free yeye alikuwa unaupoteza kwenye kusoma vitabu vya Chemistry vilivyokuwa vimejazana chumbani kwake.

Alikuwa ametokea kwenye familia masikini, hivyo baada ya baba yake kufariki hakuendelea na shule.

Mwaka 1983 akajiunga na jeshi, akadumu huko mpaka kwa miaka 4, kabla ya kuajiriwa kama afisa wa mahakama mwaka 1987.

Kutokana na Performance yake kazini, aliweza kukutana na vigogo wengi sana, na mmojawapo wao alikuwa ni Chen Daozhong ambaye huyu ndio alimuingiza Liu ungani.

Mwaka 1996, akafanikiwa kufungua-factory yake mwenyewe katika mji wa Fujian, ambayo ilidili na kuzalisha methamphetamine kwa kiwango kikubwa zaidi, mwanzoni alifanikisha kuzalisha mpaka kilo 20 za methamphetamine kwa siku.

Mwaka huo huo polisi wakamshtukia Liu, baada ya askari kanzu mmoja aliyejifanya kama mnunuzi, kupeleka taarifa za Liu kwa mamlaka husika.

Liu akalijua hilo, na akafunga ofisi yake hio ya Fujian, na kukimbia.

Alikimbilia na kujificha Puning, kule Guangdong, na mwaka 1999 akafanikiwa kufungua factories nyingine mbili sasa, moja hapo hapo katika mji wa Puning na nyingine ni katika mji wa Yinchuan, kule Ningxia.

Hapo ndio uzalishwaji wa Liu ulipokua zaidi.

Mwaka huo, polisi walisanukia tani zaidi ya 11 za methamphetamine ambazo zilikuwa ni za Liu, na wakajaribu kuandaa mipango ya kumkamata wakati walipopata taarifa kuwa Liu alikuwa kwenye chumba namba 818 cha hoteli moja ya kifahari ya huko Guangzhou.

Polisi walifunga mji, wakaweka vizuizi vya aina zote za kumdhibiti Liu bila mafanikio. Aliweza kuwachoropoka akiwa na baiskeli, na walipoenda kwenye chumba cha hoteli aliyokuwepo, walikuta amechonga ukutani “Liu Zhaohua, came here to visit”. Hii iliwavuruga sana polisi.

Alikuwa na wake 3 wa ndoa, na watoto 4 na mara kadhaa alikuwa akinukuliwa akisema “The first wife is my favorite, the second wife is my most loving, and the third wife is my most loving”.

Mwaka 2000 Liu alienda kuishi jimbo la Quanzhou, akibadili jina na kujiita Li Senqing.

Akiwa huko, aliishi maisha ya kawaida na wanajamii wenzake, na mmoja wao aliwahi kumpa maua yake akasema “He was kind to people, but rather petty, a rich man with the air of a small citizen”.

Biashara zake zilizidi kumlipa, na ili kuzidi kujiimarisha zaidi, alianza kugawa mali zake kwa serikali, ili kuwapunguzia makali.

Aliwahi kutoa ekari zake 24,000 za pale Phoenix Forestry kwa serikali na nyinginezo nyingi.

Nov 24 ya mwaka 2004, Wizara ya Ulinzi ya China iliweka mezani kama $24,160, kama zawadi kwa mtu yeyote atakaye fanikisha kuyafichua machimbo ya Liu na kazi zake.

Baada ya kuliona tangazo hili kwenye TV, Liu alikimbilia kurudi tena kwenye mji wa Fujian alikokulia.

March 5 ya mwaka 2005, akiwa kwenye harakati za kusheherekea birthday yake ya kutimiza miaka 40, Liu alikamatwa kwenye nyumba fulani ya kupanga ambayo alikuwa amejificha.

Tar 26 June 2006, Guangzhou Intermediate People's Court, iliamuru Liu ahukumiwe kifo kutokana na...
IMG_20230413_190441.jpg

..makosa ya kuzalisha na kuuza madawa ya kulevya aina ya methamphetamine.

Alikuwa na utajiri wa kama $5B kwa kipindi hicho. Na ilifikia wakati Liu alikuwa akizalisha madawa mengi kuliko kiwango cha madawa yanayozalishwa dunia nzima kwa ujumla.

IMG_20230413_190540.jpg
 
..makosa ya kuzalisha na kuuza madawa ya kulevya aina ya methamphetamine.

Alikuwa na utajiri wa kama $5B kwa kipindi hicho. Na ilifikia wakati Liu alikuwa akizalisha madawa mengi kuliko kiwango cha madawa yanayozalishwa dunia nzima kwa ujumla.View attachment 2586730
Liu aliikataa ile hukumu mwanzoni, ila ‘The Public Security Bureau’ kutupilia mbali kukataa kwake, na hatimaye akawa-executed Sept 15, 2009.

Kule China kuna wengine wanamini Lui was real-life version of China's "Walter White(Breaking Bad)", ila mi naamini Walter ni Walter.
IMG_20230413_190623.jpg
 
Liu aliikataa ile hukumu mwanzoni, ila ‘The Public Security Bureau’ kutupilia mbali kukataa kwake, na hatimaye akawa-executed Sept 15, 2009.

Kule China kuna wengine wanamini Lui was real-life version of China's "Walter White(Breaking Bad)", ila mi naamini Walter ni Walter. View attachment 2586731
iLike u story
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom