Mtuhumiwa na tabasam

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,848
2,669
Nimekuwa nikiona watuhumiwa wengi wakiachia mitabasam mpaka basi ilhali wengine ni wahalifu kweli. Tangu watuhumiwa wa epa, liyumba, zombe, mramba, yona, muro, n.k. Kuna kifungu kinawataka kukenyua mbele ya kamera? Kama hamna kamera huwa bado wanakenyua? Ukinuna utashindwa kesi? Hayo ni baadhi ya maswali tu
 
Hii ni tekiniki ya kumsambaratisha adui kwenye uwanja wa mapambano. Wanasaikolojia wanatuambia kwamba, kama unaweza kutabasamu wakati wa matatizo ni namna moja ya kukubaliana na hali halisi na kutafuta namna bora ya kukabiliana na tatizo lililopo.
Kutabasamu katikati ya matatizo ni hali ya kuchagua haiji moja kwa moja (automatically) kama ambavyo inamtokea mtu wakati wa furaha au jinsi jamii inaavyokutegemea kwamba kwa kuwa una matatizo ni lazima utaonyesha hali ya kuwa na mawazo mazito. Kutabasamu ni mtaji wa kisaikolojia na kuifanya akili iweze ku relax na kufikiri vizuri kushinda tatizo lililopo.
 
Nimekuwa nikiona watuhumiwa wengi wakiachia mitabasam mpaka basi ilhali wengine ni wahalifu kweli. Tangu watuhumiwa wa epa, liyumba, zombe, mramba, yona, muro, n.k. Kuna kifungu kinawataka kukenyua mbele ya kamera? Kama hamna kamera huwa bado wanakenyua? Ukinuna utashindwa kesi? Hayo ni baadhi ya maswali tu

Kimsingi hizi kesi zote ulizozitaja watuhumiwa wametabasamu kwa sababu wanajua ni kweli walifanya hayo makosa lakini hawatatiwa hatiani/hawatafungwa kwa sababu kadhaa.
 
Wana kazi kwel kwel. Mtu kama zombe alikuwa akipitiliza tabasam
 
Back
Top Bottom