Mtu ni nini hasa??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtu ni nini hasa???

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Chambo81, Jul 19, 2012.

 1. Chambo81

  Chambo81 JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi hua nasikia MTU akisema huu ni mwili wangu, sikio langu, pumzi yangu, moyo wangu, mawazo yangu, akili yangu, hisia zangu... Roho yangu n.k..


  Sasa maswali ninayojiuliza:-  • [*=1]mtu ni roho, mwili, hisia, au ni nini hasa?

   [*=1]sababu hata mtu akifa bado maiti itaitwa mwili wa fulani. sasa yeye "fulani" yuko wapi?

   [*=1]yeye ni kitu gani?

  Kila kitu katika mwili wa mtu kinamilikiwa na huyu mtu...ndo maana "...angu" haziishi...so kama kila kitu ni changu..."mimi" mwenyewe nipo katika nafasi gani sababu mpaka pumzi bado ni yangu...zamani nikiwa mtoto nilidhani "mtu" ni roho lakini baadae nikaona haitoshi mtu kua ni roho sababu roho ni ya "mtu" so huyu "mtu" halisi ni nini hasa?

  Naomba msaada wenu wana jf maana hii kitu inanisumbua sana kuielewa!!!
   
 2. R

  Richardbr Senior Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: May 29, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtu ni roho inayoishi ndani ya mwili wenye masikio,moyo,ubongo(hapo kuna aina mbalimbali za ubongo)
   
 3. Blessed

  Blessed JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 2,488
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  mtu ni utu!
   
 4. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ukienda kibaiolojia, seli huunda kiungo, viungo huunda mfumo, mifumo huunda mwili, mwili na uhai ndani yake ndio kiumbe hai, viumbe hai wako wa aina nyingi/falme mbalimbali, mtu yuko katika falme ya wanyama.
  Kiimani, bila roho katika mwili na uhai hamna. Endelea kutafakari.
   
 5. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nimeipata hii pahala nimei paste labda itakusaidia

  MANENO "nafsi" na "roho" yanamaanisha nini kwako? Wengi huamini kwamba maneno hayo yanamaanisha kitu fulani kisichoonekana na kisichoweza kufa kilicho ndani yetu. Wao hufikiri kwamba mtu anapokufa kitu hicho kisichoonekana hutoka ndani ya mwili wa binadamu na kuendelea kuishi. Kwa kuwa fundisho hilo limeenea sana, watu wengi hushangaa wanapogundua kwamba si fundisho la Biblia. Basi, Neno la Mungu linasema nafsi na roho ni nini?

  FUNDISHO LA BIBLIA KUHUSU "NAFSI"

  Kwanza, tuzungumzie nafsi. Huenda unakumbuka kwamba mwanzoni Biblia iliandikwa katika Kiebrania na Kigiriki. Waandishi wa Biblia walitumia neno ne′phesh la Kiebrania au psy·khe′ la Kigiriki walipoandika kuhusu nafsi. Maneno hayo mawili yanapatikana zaidi ya mara 800 katika Maandiko, na Tafsiri ya Ulimwengu Mpya huyatafsiri yote kuwa "nafsi."

  Unapochunguza jinsi neno "nafsi" linavyotumiwa katika Biblia, utaona kwa wazi kwamba neno hilo humaanisha (1) watu, (2) wanyama, au (3) uhai wa mtu au mnyama. Na tuzungumzie baadhi ya Maandiko yanayoonyesha mambo hayo matatu.

  Watu

  "Katika siku za Noa . . . watu wachache, yaani, nafsi nane, walichukuliwa salama kupitia maji." (1 Petro 3:20) Kwa wazi neno "nafsi" katika andiko hilo linamaanisha watu, yaani, Noa, mkewe, wanawe watatu, na wake zao. Andiko la Kutoka 16:16 lina maagizo kwa Waisraeli kuhusu kuokota mana. Waliambiwa: "Okoteni kiasi chake . . . kulingana na hesabu ya nafsi ambazo kila mmoja wenu anazo katika hema lake." Kwa hiyo, kiasi cha mana kilichookotwa kilitegemea kiasi cha watu katika kila familia. Maandiko yafuatayo ya Biblia yanaonyesha matumizi ya neno "nafsi" kumaanisha watu, Mwanzo 46:18; Yoshua 11:11; Matendo 27:37; na Waroma 13:1.

  Wanyama

  Tunasoma hivi katika masimulizi ya Biblia kuhusu uumbaji: "Mungu akaendelea kusema: ‘Maji na yajawe na nafsi hai na viumbe vinavyoruka viruke juu ya dunia kwenye uso wa anga la mbingu.' Mungu akaendelea kusema: ‘Dunia na itokeze nafsi zilizo hai kulingana na aina zake, mnyama wa kufugwa na mnyama anayetambaa na mnyama-mwitu wa dunia kulingana na aina yake.' Ikawa hivyo." (Mwanzo 1:20, 24) Katika andiko hilo, samaki, wanyama wa kufugwa, na wanyama-mwitu wote wanaitwa kwa neno lilelile-"nafsi." Ndege na wanyama wengine wanaitwa nafsi kwenye Mwanzo 9:10; Mambo ya Walawi 11:46; na Hesabu 31:28.

  Uhai wa mtu

  Wakati mwingine neno "nafsi" humaanisha uhai wa mtu. Yehova alimwambia Musa: "Watu wote waliokuwa wakiiwinda nafsi yako wamekufa." (Kutoka 4:19) Adui za Musa walikuwa wakiwinda nini? Walitaka kumuua Musa. Raheli alipokuwa akimzaa mwanawe Benyamini, ‘nafsi yake ilitoka (kwa sababu alikufa).' (Mwanzo 35:16-19) Wakati huo Raheli alipoteza uhai wake. Fikiria pia maneno ya Yesu: "Mimi ndiye mchungaji mwema; mchungaji mwema huitoa nafsi yake kwa ajili ya kondoo." (Yohana 10:11) Yesu alitoa nafsi au uhai wake kwa ajili ya wanadamu. Katika maandiko hayo ya Biblia, ni wazi kwamba neno "nafsi" linamaanisha mtu. Utapata mifano mingine yenye maana hiyo ya neno "nafsi" kwenye 1 Wafalme 17:17-23; Mathayo 10:39; Yohana 15:13; na Matendo 20:10.
  Unapoendelea kujifunza Neno la Mungu utaona kwamba hakuna popote katika Biblia ambapo neno "nafsi" linahusianishwa na "kutoweza kufa" au "kuishi milele." Badala yake, Maandiko yanasema kwamba nafsi inaweza kufa. (Ezekieli 18:4, 20) Kwa hiyo, katika Biblia mtu ambaye amekufa huitwa ‘nafsi iliyokufa.'-Mambo ya Walawi 21:11.

  MAANA YA "ROHO"

  Hebu tuzungumzie jinsi Biblia inavyotumia neno "roho." Watu fulani hufikiri kwamba "roho" ni neno lingine linalomaanisha "nafsi." Lakini, si kweli. Biblia inaonyesha wazi kwamba "roho" na "nafsi" ni vitu viwili tofauti. Vinatofautianaje?
  Waandishi wa Biblia walitumia neno la Kiebrania ru′ach au neno la Kigiriki, pneu′ma waliporejelea "roho." Maandiko yenyewe yanaonyesha maana ya maneno hayo. Kwa mfano, andiko la Zaburi 104:29 linasema: "[Yehova] ukiiondoa roho [ru′ach] yao, wanakata pumzi, na kurudi katika mavumbi yao." Andiko la Yakobo 2:26 linasema kwamba "mwili bila roho [pneu′ma] umekufa." Katika andiko hilo "roho" inamaanisha kile ambacho huupa mwili uhai. Bila roho, mwili umekufa. Kwa hiyo, katika Biblia neno ru′ach halitafsiriwi tu "roho" bali pia "nguvu" au kani ya uhai. Kwa mfano, Mungu alisema hivi kuhusu Mafuriko ya siku ya Noa: "Ninaleta gharika ya maji duniani ili kuharibu kutoka chini ya mbingu wote wenye mwili walio na nguvu [ru′ach] za uhai ndani yao." (Mwanzo 6:17; 7:15, 22) Hivyo, "roho" inarejelea nguvu isiyoonekana, inayotendesha viumbe vyote vilivyo hai.
  [​IMG] Nafsi na roho hutofautiana. Mwili unahitaji roho kama vile redio inavyohitaji umeme ili kufanya kazi. Kwa mfano, unapotia betri katika redio na kuiwasha, nguvu zilizo katika betri huiwezesha redio kufanya kazi. Hata hivyo, redio haiwezi kufanya kazi bila betri. Hali kadhalika, redio ambayo imeondolewa kwenye umeme haiwezi kufanya kazi. Vivyo hivyo, roho ni nguvu ambayo hutendesha mwili wetu. Kama umeme, roho haiwezi kuhisi wala kufikiri. Ni nguvu isiyo na utu. Lakini bila roho au kani ya uhai, "tunakata pumzi na kurudi kwenye udongo," kama mtunga-zaburi alivyosema.

  Andiko la Mhubiri 12:7 linasema hivi linapozungumzia kifo cha mwanadamu: "Mavumbi [mwili wake] huirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho yenyewe humrudia Mungu wa kweli aliyeitoa." Roho au kani ya uhai inapoondoka mwilini, mwili hufa na kurudi ulipotoka, yaani, kwenye udongo. Vivyo hivyo, nguvu ya uhai hurudi ilipotoka, yaani, kwa Mungu. (Ayubu 34:14, 15; Zaburi 36:9) Hiyo haimaanishi kwamba nguvu ya uhai huenda mbinguni kihalisi. Badala yake, inamaanisha kwamba mtu akifa, tumaini lolote la kuishi tena linamtegemea Yehova Mungu. Ni kana kwamba uhai wake uko mikononi mwa Mungu. Ni kupitia nguvu za Mungu tu ndipo roho au nguvu ya uhai inaweza kurudishwa ili mtu aweze kuishi tena.

  Inafariji kama nini kujua kwamba hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya kwa wote wanaopumzika ndani ya "makaburi ya ukumbusho!" (Yohana 5:28, 29) Wakati wa ufufuo, Yehova atamfanyizia mwili mpya yule anayelala katika kifo na kuuhuisha kwa kutia roho, au nguvu ya uhai ndani yake. Itakuwa siku ya shangwe sana.
   
 6. Sashel

  Sashel JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MTU ni mjumuiko wa roho, nafsi na mwili. ukiondoa roho inabaki maiti, roho ni hiyo pumzi ya Mungu iupao mwili uhai, roho haionekani bali mwili ndio unaoonekana- roho huongea japokuwa unaweza ukawa upo kimya lakini unaisikia inaongea na hapa ni tofauti na kuwaza wewe mwenyewe...sijui kama huwa inakutokea..unaweza kusikia jambo halafu ukawaza kichwani na kufanya maamuzi lakini roho akawa hakubaliani nayo na unahisi kama kuna mtu ndani anakukataza binafsi hiyo nime-experience sana. Hivyo mkuu MTU sio kitu kimoja bali ni: roho +nafsi+mwili= MTU
   
 7. Chambo81

  Chambo81 JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana Waridi,wakati naendelea kutafakari nagundua kua mtu alianza kuwepo kabla ya uumbaji wa seli na mwili ndio maana hivi vyote vikifa tunaviita mwili wa fulani utazikwa....bado naona kuna kitu zaidi ya huu mwili uumbwao na seli ambacho kinamiliki au kilimiliki mwili huu ambacho ndio MTU MWENYEWE....napata logic kidogo ulipozungumzia Roho na Uhai ingawa bado haipo clear sana labda naomba unifafanulie zaidi kuhusu uhai/roho kwa sababu huu uhai na roho alipewa au anavyo mtu....SO HIKI KILICHOPEWA UHAI NA ROHO NI KITU GANI??????

  Hata wewe kuna wakati unasikitika roho ya mtu ikipotea aidha kwa ajali au kuuawa na kama ambavyo tumeona juzi Roho za watu zikipotea kwa ajali ya meli....Jiulize hawa watu ambao hizi roho ni zao ni kitu gani?au ni nini??Daaah nashindwa kujua kama mimi ndo mzito kuelewa au hii kitu haieleweki.....

  Tuendelee kutafakari kwa pamoja mwisho wa siku kinaweza kueleweka!!!
   
 8. Chambo81

  Chambo81 JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Daah Sashel unakaribia sana kwenye kile kitu ambacho kipo kwenye akili yangu kilichonipelekea kuuliza swali hili....hua na experience sana kile kitu una-experience...nafikiri roho na nafsi ni kitu kimoja ambacho hatujui tukiite vipi kwa sababu maneno nayo ni limit tosha kwa sababu kuna hali nyingi mtu unazipata lakini huwezi kuweka katika maneno na hata ukiweka kwenye maneno haiwezi kumaanisha exactly vile unavyofeel...

  Ila mwili mmmmh unasupport tu ndo maana hata tukipata ajali miili yetu ikaharibika vibaya na hata kukatwa viungo vyetu haitubadilishi kua kitu kingine,tunaendelea kuwa watu!!!Kwa hiyo nadhani utu unaweza kuuexperience na hauelezeki,ni kama vile mtu anaekula chungwa anavyoshindwa kukuelezea ladha ya chungwa analokula zaidi ya kusema tu tamu au chachu unless akukatie kipande uonje mwenyewe.

  Na ukionja unaweza ukacomment tofauti na vile alivyokusimulia...so ni vipi tuta-expirience huu utu kwa kukusudia and not for granted!!!?????
   
 9. K

  KakaNanii JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2012
  Joined: Sep 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mtu ni kile unachofikiri ndo wewe !
   
 10. Sashel

  Sashel JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Chambo, we have been created and programmed that way...we just experience it we can not turn it on and off, its like air you cant see it but you constantly breath in and out!
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Majibu

  Mwili wa binaadamu ndio nafsi, Nafsi inaweza kuwa hai au isiwe hai (mfu). Biblia inasema baada ya Mungu kumpulizia pumzi adamu hapo mwanaadamu akawa nafsi iliyo hai, hivyo state aliyokuwa nayo Adam kabla hajapuliziwa pumzi na Mungu ni nafsi ambayo haikuwa na uhai.

  Pumzi aliyopuliziwa adamu na Mungu ni hii tunayotumia sasa, ndio maana mwanaadamu akishindwa kuvuta hewa ama akikosa hewa anakufa.

  Roho, note kwamba kuna roho wa Mungu na Roho wa Shetani, Roho ni Nguvu inayoendesha ubongo wa Mwanaadamu. Roho wa Mungu huuendesha ubongo wa Mwanaadamu kufikiri yaliyo mema,kutenda yaliyo mema, na zaidi, kujua yaliyo mema ndio maana ulimwengu mzima umetahayari, zaidi ya asilimia 99 ya wanaadamu hawaelewi kabisa kabisa Mungu ni nini? wishes zake ni zipi? Histrory ya matendo yake nini?

  Japo haya yote kayaweka in writing kwenye Biblia, ndio maana leo tuko hapa tunajadili sisi ni nini, very interesting, ukiangalia tofauti ya majibu yatakayokuwa yanaporomoshwa hapa utashangaa, kwamba mwanaadamu na uwezo mkubwa tunaouonyesha sasa kama kutengeza ndege, computer, simu, magari, internet nk sisi wenyewe hatujui tumetengenezwa vipi. The reason to this ni kwamba hatuna roho ya Mungu, we can not understand his word. Hii ndio roho wa Mungu, Roho mtakatifu. Clean spirit.Bila Roho wa Mungu binaadamu ni doomed. Ndio Maana Yesu, alisema NI MSAIDIZI.

  Roho wa Shetani
  Utuongoza kwenda kinyume na Mungu, au kinyume hata na utashi very basic wa kibinaadamu.uovu na ujinga vyote ni zao la nguvu ya shetani ambayo ndio inaongoza the majority of world pupulace.

  Roho wa Mungu VS Roho wa Shetani
  Hizi hazikai pamoja, Mwanaadamu ama ataongozwa na Roho wa Mungu au ataongozwa na Roho wa Shetani period. Majority wanaongozwa na roho wa Shetani.

  N.B

  Roho ni upepo. I mean it has a form of wind.

  Mfalme Daudi, Baada ya kutafakari sana uumbaji wa Mungu, alilazimika kusema I AM WONDERFULLY MADE.

  We real a very wonderful creation.

  Bye.
   
 12. Sashel

  Sashel JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  well sangarara,

  huo ni ufahamu wako usio sahihi. MTU ni roho, nafsi na mwili, ukiondoa kimoja wapo kati ya hivyo hakuna mtu. Hewa tuipumuayo sio pumzi ya Mungu hii ni oxygen na inaweza kutengenezwa na wanadamu, pumzi ya Mungu ni nguvu- ndiyo roho inayofanya mwili huu wa nyama uwe hai. Unasema spirit has a form of wind!? si kweli maana roho haina form /umbile ndio maana Roho mtakatifu anatwajwa kama moto, maji, upepo wa kisulisuli nk. Mleta madaa alitaka kujua Mtu ni nini?..wewe umechanganya na habari za shetani na roho zilizoasi (mapepo) ambapo yote hayo mwanzo wake ni Mungu maana shetani aliumbwa na Mungu pia na alikuwa mbele zake akitoa sifa kabla ya kuasi, hizo zote ni roho hazina miili yenye nyama. Sitakuita mwongo bali usiyefahamu; I recomend you to re-read your bible na usomapo mwombe Mungu akupe uafahamu ili usisome kama gazeti.
   
 13. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Uko mbali sana na uelewa wa haya mambo.
  Uko tayari tufanye back up ya arguments zetu kwa kufanya reference kutoka kwenye Biblia?
   
 14. Sashel

  Sashel JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nakuhakiki ya kuwa siko mbali kama unavyofikiri, Ok unakaribishwa
   
 15. Sashel

  Sashel JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa kuanzia tu mwanzo wa kuumbwa mwanadamu; Mwanzo: 2:7 BWANA, Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; akawa nafsi hai-Mavumbi ya nchi na Pumzi ya uhai. Hakuna kitu kingine kilichitiwa ndani ya mwanadamu. Mchanganiko huu wa Mavumbi na Pumzi ya uhai (roho) ilifanyika nafsi hai -Ayubu anaisema'roho ya Mungu' kuwa' Roho ya Mungu i katika pua yangu' (Ayubu. 27:3). Wakati mwanadamu anapokufa pumzi yake hutoweka na mavumbi yaliyobakia (mwili) huwa nafsi iliyo kufa. Zaburi 146:4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake hupotea.

  Kuhusu dai lako kuwa roho ina umbo kama upepo: soma (Kumb 4:15) Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile Bwana aliyosema nanyi kutoka kati ya moto. (Mdo 2:2-3) Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao; nachataka ujue ni kuwa pumzi ya Mungu (roho) ni nguvu ya Mungu itoayo uhai kwa viumbe haina form/ umbile
   
 16. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Sasa upepo/wind unaumbile gani?
   
 17. Sashel

  Sashel JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Labda nikukumbushe sehemu ya post yako:

  'N.B
  Roho ni upepo. I mean it has a form of wind.'

  Naamini hata wewe unajua kuwa upepo hauna form maana hauonekani lakini tunauhisi, kwa maana yako wewe ni kuwa roho yupo kama upepo na si vinginevyo kitu ambacho si kweli, bali kuvuma kama upepo ni moja ya kujidhihirisha kwake kama vile ilivyotokea wakati wa pentekoste - ulikuwa ni uvumi kama wa upepo kisha zikatokea ndimi za moto..so huwezi sema ni upepo kwasababu huvuma kama upepo au ni moto kwakuwa alionekana kama ndimi za moto.
   
 18. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Naomba nikuulize Swali. Kisha nitarudi hatua kwa hatua kwenye references ulizofanya, nimeagiza Biblia ije mara moja.
  From common sense point of view.
  Wote tunajua kazi ya kila kiungo kwenye mwili wa binaadamu na mahusiano baina ya kiungo na kingo yalivyokuwa well connected.

  Naomba uelezee hii structure ya Mtu ni ROHO, NAFSI NA MWILI. Clearly utuonyeshe roho ni nini na nafasi yake ni ipi katika ukamilifu wa mtu, ufanye hivyo juu ya Nafsi na Mwili pia. Ukifanya reference uonyeshe ile ambayo kwa kiwango kikubwa sana inasupport argument yako in persepective.

  Nadhani huu ni mtiririko mzuri wa hoja.
   
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Inaonekana neno FORM ndio linakusumbua, MATTER, LIQUID AND AIR. unapopinga kwamba ROHO sio upepo alafu unasema huvuma kama upepo unanichanganya, na hapo Bado ninajiepusha kuipin point blunder kubwa sana ya haya mambo ambayo unaipigia chepuo.

  Please get back to the Basic question I have just asked.
  Naomba uelezee hii structure ya Mtu ni ROHO, NAFSI NA MWILI. Clearly utuonyeshe roho ni nini na nafasi yake ni ipi katika ukamilifu wa mtu, ufanye hivyo juu ya Nafsi na Mwili pia. Ukifanya reference uonyeshe ile ambayo kwa kiwango kikubwa sana inasupport argument yako in persepective.
   
 20. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye Bold nani au nini kikawa nafsi hai?.
   
Loading...