Mtu mwenye AKILI ni yupi!!!

Mtu mwenye AKILI ni yupi!!!

Mkuu BIG X,

Karibu kila mtu huzaliwa na "akili"..nikimaanisha uwezo wa kufikiri.Lakini mara baada ya kuzaliwa kuna tofauti zinaweza kujitokeza(hata kwa wale waliozaliwa siku moja na maeneo sawa).

Kuna makundi mawili unayoweza kusema ya "watu wenye akili"

Mwenye akili-I (Smart, Intelligent)
Hii huelezea uwezo wa ubongo wa mwanadamu katika kufanya kazi(Person's mental ability).Na hapa ndipo pale tunaposema "fulani ana akili"..yaani mwanafunzi fulani ana akili.Hii ni kutokana na ufahamu, ujuzi(knowledge, skills).

Aina hii ya watu wenye akili, hutokana na kusoma, kujikumbusha, na kufaulu hasa kwa mitihani ya mambo yale yaliyosomwa kabla.

Katika kipimo cha Intelligent Quotient(IQ), kuna madaraja(grades) mbalimbali hasa kutokana na Ufahamu, usomi(Knowledge) ambayo mtu anayo tayari.

Mwenye akili-II (Busara,Hekima):
Huyu anakuwa na uelewa, na mambo yake yako kimpango, mkakati, hata kama ni jambo dogo au katika mazingira magumu...yaani, uwezo wa kufanya maamuzi(hasa magumu) na kuamua kufanya jambo(ukiwa na sababu kwa nini unafanya, muda gani, kwa namna gani), na ushauri.

Pia aina hii ya "akili" hutokana na kuishi muda mrefu, uzoefu mwingi/mkubwa mazingira mbalimbali.mf. mara kadhaa watu husemai wazee wanahekima/busara(hasa kutokana na uzoefu wa mambo aliyowahi kuona/kusikia/kufanya kabla ya wale aliowatangulia)..hata kama hakuwahi kuwa shule.

Hivyo basi makundi yote haya tunawaita wenye akili, ikiwa kundi la kwanza hutegemea kuwa na uwezo kwa ufahamu ulioupata tayari na kundi la pili kutokana na uzoefu.Hata hivyo baadi ya watu huweza kuwa katika makundi yote.

Kwahiyo we unasema watu waliokula chumvi nyingi wana akili zaidi!!!.
 
watu wengi wanachanganya mambo mawili ambayo ni AKILI NA KUWA NA MALI (TAJIRI). Akili mtu huzaliwa nazo na utajiri mtu hazaliwi nao.akili kisayansi hutegemea wingi wa GREY MATTERS kwenye ubongo wa binadamu. wengine grey matters ni kidogo hivyo na akili yake huwa kidogo na wengine grey matters ni nyingi na hivyo ubongo wake huwa na uwezo mkubwa ambayo tunaita akili.Mfano rahisi ni kama CHIP ZA SIMU.kuna simu zinaweza kutunza majina 400 tu na nyingine zinaweza kutunza majina 1000! ndio akili ya simu.
Utajiri kwa upande mwingine unategemea mambo mengi sana pamoja na akili.utajiri hutegemea pia bahati.unaweza kucheza bahati nasibu ukapata utajiri ingawa una akili kidogo au grey matters za ubongo wako ni kidogo. unaweza ukashinda medali ktk olympic ukapata fedha nyingi na ukawa tajiri.unaweza kuiba mali kwa watu wengine ukawa tajiri.kifupi ni kwamba asili mia kubwa ya wenye akili wana nafasi ya kuwa matajiri lakini mtu asiye na akili atategemea zaidi nguvu yake na BAHATI ili atajirike

Hizo grey matters sijaelewa mkuu, ila nilichoelewa ni kwamba wewe unafananisha AKILI na hard-drive ya computer yenye uwezo wa kutunza kumbukumbu zaidi. Kwahiyo wewe mtu mwenye AKILI ni yule mwenye uwezo wa kutunza kumbukumbu.
 
Kuna watu wanabishana hapa. Hivi mtu mwenye AKILI ni yule tu anayefaulu darasani?, Kama hukuwa na uwezo wa kufaulu darasani lakini umefakiwa katika mambo mengine, Je na wewe utakuwa na AKILI!!, Au mtu mwenye AKILI ni wa namna gani.

Ni yule anayehifadhi vijisenti vyake Uswiss au visiwa vya Jersey.

Kuna na yule anaedai 10% ili akupatie "deal"

Ama mtu asiye na akili ni yule anayegawiwa ahadi hewa na umaskini. Lakini bila kujitambua anakuwa ni mgongo/ngazi ya wajanja kujipatia "kura/kula".
 
mwenye akili ni mtu anayeunda tume ya kufanya uchunguzi, na ripoti ikiandaliwa anaipokea mbele ya waandishi wa habari.Ripoti itawekwa maktaba ya ofisi.hapo kazi ya muunda tume itakuwa imeisha.
 
mwenye akili ni mtu anayeunda tume ya kufanya uchunguzi, na ripoti ikiandaliwa anaipokea mbele ya waandishi wa habari.Ripoti itawekwa maktaba ya ofisi.hapo kazi ya muunda tume itakuwa imeisha.

nadhani hata jinsi mtu utakavyoandika hapa, inatosha kujua kama we una AKILI au huna!!.
 
Cha kwanza kabisa mwenye akili ni mtu amchaye Mungu kwa kuchukia uovu,kumpenda Mungu na kutii neno lake, pili Mwenye akili ni yule awezaye kutawala nafsi yake. au pia naweza kusema mwenye akili ni yule mtu ambaye ana thamani(hajauza thamani yake).

Akili ni roho inaweza kuibiwa kama unavoweza kuibiwa thamani ya pesa rohoni na mwishowe ukapata hasara kwa namna ya ajabu. hivyohivyo akili ya mtu inaweza kuibiwa ikatumika pengine na wewe mwenyewe ukawa mtu wa kuluwaluwa tu,na kutafuta shortcut ili kurudia utukufu wako wa mwanzo.

Njia mojawapo ya kuibiwa akili na kupoteza thamani yako ni hii hapa:
-Aziniye na mwanamke hana akili kabisa,afanya jambo la kuangamiza nafsi yake.
 
Kwahiyo we unasema watu waliokula chumvi nyingi wana akili zaidi!!!.

Hayo ni maneno yako, SIJASEMA hivyo katika maelezo yangu...either ulitaka iwe hivyo au umenielewa hivyo.

Hapa ninaweza kusema nakosa maneno ya kueleza kwa kiswahili(either kwa mimi mwenyewe kutokujua au kutojitosheleza kwa maneno ya kiswahili).

Kama tukisema kwa lugha ya kiingereza tunamaanisha INTELLIGENCE..the one's(person's) mental ability to understand(+/-reasoning)...also can be one's ability to manipulate things from acquired knowledge.
-Remember the key point here is KNOWLEDGE.
Na ndio maana tunapima IQ(Intelligence quotient), Intelligence tests na kuna kuwa na grade mbalimbali.

"Waliokula chumvi"..hawa "watu" husema wana akili(kutokana na maamuzi, from "reasoning" pia, na UZOEFU...kuna msemo unasema youngster know every rule/principle, but oldman know exceptions..meaning kwa vijana wanaweza kujua hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa kwa sababu hii na hii, lakini "mla chumvi" kutokana na umri anajua njia mbadala ambao hizo (principles) zinaweza kuepukwa na bado kufikia lengo hilo hilo au zaidi.
Hawa tunawaita wana hekima/busara...hasa kutokana na kufanya maamuzi, ila they are WISE(have wisdom) but not intelligent.

The bottomline is Wisdom comes with AGE(life experience as you apply in decision making)..na hakuna kipimo chake tofauti na Intelligence, sasa kwa kiswahili wote tunawajumuisha kwa pamoja(and that's where confusion is).

So, answering your question NO, siyo kila wazee wana "akili".
 
Kwenye utajiri akili huwa ina play part ndogo mno,nafasi kubwa inachukuliwa na bahati,and then akili inatake place to remain number one.
 
kwahiyo ili uwe na AKILI si lazima uwe umekula chumvi nyingi!!.
 
Ukimwona mwenye akili utajua tu, mambo yake yamekaa vizuri hategemei cheti cha darasani. Mwenye akili akifanya ufisadi Hali bila kunawa, na si rahisi kumgundua.
 
kila binadamu ni mtu mwenye akili,lakini tofauti huja kama anaakili timamu,au akili isiyotimamu,akili ya kuchanganua mambo au la, akili ya uelewa au ugumu wa kuelewa,.
 
Back
Top Bottom