Mtu mwenye AKILI ni yupi!!!


BIG X

BIG X

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2011
Messages
777
Points
0
BIG X

BIG X

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2011
777 0
Kuna watu wanabishana hapa. Hivi mtu mwenye AKILI ni yule tu anayefaulu darasani?, Kama hukuwa na uwezo wa kufaulu darasani lakini umefakiwa katika mambo mengine, Je na wewe utakuwa na AKILI!!, Au mtu mwenye AKILI ni wa namna gani.
 
T

TheDealer

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2012
Messages
2,430
Points
1,250
T

TheDealer

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2012
2,430 1,250
MTU MWENYE AKILI NI HUYU HAPA, kwa mtazamo wangu binafsi:
ni yule anaefahamu kuwa yupo sahihi kwa sababu ana sababu sahihi ya kuwa sahihi, na si kwa sababu mtu mwingine kamwambia yupo sahihi.
He/she is right because of his/her facts and not because other people say s/he is right.
 
Jile79

Jile79

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2009
Messages
12,192
Points
2,000
Jile79

Jile79

JF-Expert Member
Joined May 28, 2009
12,192 2,000
Mimi naamini mtu mwenye akili ni yule ambaye ni mwepesi wa kupambanua mambo kwa haraka na kutolea majibu sahihi kwa haraka na mwenye uwezo wa kukabiliana na mazingira yoyote ya kimaisha
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
44,024
Points
2,000
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
44,024 2,000
Mwenye akili ni yule anayejua ni nini dhumuni la yeye kuwepo ulimwenguni.
Pia yule ambaye aliamua kujia kwa sababu alishindwa kujua dhumuni la yeye kuwepo duniani aliitwa hana akili kabisa, licha ya kwamba mimi nilimuona ana akili, ila alikosa bahati.
Akili bila bahati kwenye muda muafaka ni UBATILI MTUPU
 
BIG X

BIG X

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2011
Messages
777
Points
0
BIG X

BIG X

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2011
777 0
Sasa mtu kuwa Professor inatosha kusema mtu huyu ana AKILI hata kama hayo yote kwake ni sifuri!.
 
shuve

shuve

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2012
Messages
312
Points
225
shuve

shuve

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2012
312 225
Nijinc utakavyo itumia ndo utaonekana una akili au laaa! :mad::mad::mad:
 
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
9,245
Points
2,000
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
9,245 2,000
Ni yule mwenye nywele. Akili ni nywele ..........................! Mwe.
 
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
12,290
Points
2,000
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
12,290 2,000
Kuna watu wanabishana hapa. Hivi mtu mwenye AKILI ni yule tu anayefaulu darasani?, Kama hukuwa na uwezo wa kufaulu darasani lakini umefakiwa katika mambo mengine, Je na wewe utakuwa na AKILI!!, Au mtu mwenye AKILI ni wa namna gani.
Mtu mwenye akili ni kama kiongozi mkuu vile!!!!!! Ni lazima uwe na akili sana ya kufikiri na kupambanua mambo haraka maana tunajua kiongozi ndiye anayetoa maamuzi ya mwisho hata kama washauri wanakuwa wameshaandaa but anatakiwa awe na IQ kubwa kuliko hata washauri wenyewe!! Vinginevyo atakuwa anabadili ya ukweli yanakuwa ya uongo au yasiyotekelezeka!!! Bisha!!
 
M

Maamuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2008
Messages
856
Points
225
M

Maamuma

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2008
856 225
Mwenye akili ni yule anayejua ni nini dhumuni la yeye kuwepo ulimwenguni.
Pia yule ambaye aliamua kujia kwa sababu alishindwa kujua dhumuni la yeye kuwepo duniani aliitwa hana akili kabisa, licha ya kwamba mimi nilimuona ana akili, ila alikosa bahati.
Akili bila bahati kwenye muda muafaka ni UBATILI MTUPU
Samahani, naenda nje ya mada.
Kwa faida ya yeyote atakayehusika: Neno MADHUMUNI halina umoja (hakuna neno DHUMUNI), kama ilivyo kwa neno MAFAO - hakuna FAO.
Napenda Kiswahili. Asante.
 
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined
Sep 1, 2011
Messages
3,235
Points
1,195
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined Sep 1, 2011
3,235 1,195
Swali nzuri hili, ngoja tutapata majibu hapa. Tuendelee kusubiri
 
Kichancheda

Kichancheda

Senior Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
142
Points
0
Kichancheda

Kichancheda

Senior Member
Joined Oct 29, 2012
142 0
Kila binadamu amezaliwa na akili. Ila Mtu mwenye akili zaidi ni " PROBLEM SOLVER faster and accuracy" Mtu anayeweza kutatua mambo mbalimbali kwa ufasaha na haraka (Kielimu, Kimaisha etc) Ndio maana watu watu husema anaakili kama computer
 
BIG X

BIG X

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2011
Messages
777
Points
0
BIG X

BIG X

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2011
777 0
Je Mwenye AKILI utamjua kwa anavyoandika hoja yake!!

Kwa kiasi fulani naona tunatofautiana. Kwa mfano kwa kutumia uandishi wa mtu hata hapa JF unaweza ukasema huyu mtu aliyeandika kweli ana akili. Kuna mwingine unasoma unajua kweli hapa hamna kitu. Hapo vipi!!.
 
Makene

Makene

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,478
Points
1,195
Makene

Makene

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,478 1,195
kila kiumbe hai kina akili, ila uwezo wa kuchanganua mambo katika mahusiano na mazingira yao ndio inaweka tofauti katika uwezo wa matumizi ya akili.
Watu wanaoelimishwa katika nyanja fulani ya elimu na kufanikiwa kuwaridhisha wale wanaowafunza au kuandaa mitaala, haiwafanyi wawe na akili kuliko uwezo wao.
Watu wenye uwezo mkubwa wa akili ni wale wanaovumbua mambo yanayowezesha unafuu wa kiutendaji au kuboresha hali za mazingira na ubora wa maisha , hao tunaweza sema wana uwezo wa juu wa kutumia akili.
Msomi anafanya matumizi ya akili za wengine sio kwamba ana akili sana.
 
F

Fursa Pesa

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2012
Messages
2,649
Points
2,000
F

Fursa Pesa

JF-Expert Member
Joined May 30, 2012
2,649 2,000
Ni yeyote yule anayejitambua kwamba yeye ni nani yuko wapi na kwanini awepo kwa ajili ya nani ili iweje wapi na lini alafu iwe nini.


Kila mtu anazo akili kwani hata kwa wale ambao tunasema ni wendawazimu wao wanajiona si wendawazimu ingawa tofauti kubwa ni mazingira. Kwa mfano wazungu siku zote utuona sisi wafrika kama vile hatuna akili timamu kutokana na masuala fulanix2,lakini sisi wafrika nasi kwa namna yetu tunajiona kwamba ni wenye utimamu kwelix2.anyway ni mada nzuri,asante kuwasilisha.
 
MZIMU

MZIMU

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
4,078
Points
1,225
MZIMU

MZIMU

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
4,078 1,225
mtu mwenye akili ni yule ambae anaejua kua mazingira yake yanahitaji nini ili aweze kuyatawala. Na kueweza kutawala mazingira yake kwa mafanikio, na sio vinginevyo.
 
H

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2012
Messages
3,601
Points
1,195
H

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2012
3,601 1,195
Mkuu BIG X,

Karibu kila mtu huzaliwa na "akili"..nikimaanisha uwezo wa kufikiri.Lakini mara baada ya kuzaliwa kuna tofauti zinaweza kujitokeza(hata kwa wale waliozaliwa siku moja na maeneo sawa).

Kuna makundi mawili unayoweza kusema ya "watu wenye akili"

Mwenye akili-I (Smart, Intelligent)
Hii huelezea uwezo wa ubongo wa mwanadamu katika kufanya kazi(Person's mental ability).Na hapa ndipo pale tunaposema "fulani ana akili"..yaani mwanafunzi fulani ana akili.Hii ni kutokana na ufahamu, ujuzi(knowledge, skills).

Aina hii ya watu wenye akili, hutokana na kusoma, kujikumbusha, na kufaulu hasa kwa mitihani ya mambo yale yaliyosomwa kabla.

Katika kipimo cha Intelligent Quotient(IQ), kuna madaraja(grades) mbalimbali hasa kutokana na Ufahamu, usomi(Knowledge) ambayo mtu anayo tayari.

Mwenye akili-II (Busara,Hekima):
Huyu anakuwa na uelewa, na mambo yake yako kimpango, mkakati, hata kama ni jambo dogo au katika mazingira magumu...yaani, uwezo wa kufanya maamuzi(hasa magumu) na kuamua kufanya jambo(ukiwa na sababu kwa nini unafanya, muda gani, kwa namna gani), na ushauri.

Pia aina hii ya "akili" hutokana na kuishi muda mrefu, uzoefu mwingi/mkubwa mazingira mbalimbali.mf. mara kadhaa watu husemai wazee wanahekima/busara(hasa kutokana na uzoefu wa mambo aliyowahi kuona/kusikia/kufanya kabla ya wale aliowatangulia)..hata kama hakuwahi kuwa shule.

Hivyo basi makundi yote haya tunawaita wenye akili, ikiwa kundi la kwanza hutegemea kuwa na uwezo kwa ufahamu ulioupata tayari na kundi la pili kutokana na uzoefu.Hata hivyo baadi ya watu huweza kuwa katika makundi yote.
 
Last edited by a moderator:
J

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Messages
2,764
Points
2,000
J

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2012
2,764 2,000
watu wengi wanachanganya mambo mawili ambayo ni AKILI NA KUWA NA MALI (TAJIRI). Akili mtu huzaliwa nazo na utajiri mtu hazaliwi nao.akili kisayansi hutegemea wingi wa GREY MATTERS kwenye ubongo wa binadamu. wengine grey matters ni kidogo hivyo na akili yake huwa kidogo na wengine grey matters ni nyingi na hivyo ubongo wake huwa na uwezo mkubwa ambayo tunaita akili.Mfano rahisi ni kama CHIP ZA SIMU.kuna simu zinaweza kutunza majina 400 tu na nyingine zinaweza kutunza majina 1000! ndio akili ya simu.
Utajiri kwa upande mwingine unategemea mambo mengi sana pamoja na akili.utajiri hutegemea pia bahati.unaweza kucheza bahati nasibu ukapata utajiri ingawa una akili kidogo au grey matters za ubongo wako ni kidogo. unaweza ukashinda medali ktk olympic ukapata fedha nyingi na ukawa tajiri.unaweza kuiba mali kwa watu wengine ukawa tajiri.kifupi ni kwamba asili mia kubwa ya wenye akili wana nafasi ya kuwa matajiri lakini mtu asiye na akili atategemea zaidi nguvu yake na BAHATI ili atajirike
 

Forum statistics

Threads 1,296,584
Members 498,672
Posts 31,253,077
Top