FikraPevu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2010
- 303
- 236
Mtu mmoja wamefariki dunia na wawili kujeruliwa katika ajali iliyotokea katika eneo Kikatiti jijini Arusha iliyohusisha lori lililobeba matofari kuyagonga magari sita yaliyokuwa mbele yake.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema chanzo cha ajali hiyo iliyotokea jana saa 2:30 usiku ni lori iliyokuwa imebeba matofali ilifeli breki ikiwa katika mteremko maeneo ya Kikaticha ambapo liligonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake.
Amesema gari hilo liligonga gari aina ya Kruger ambayo ilikuwa ikiendeshwa na mzee aliyejulikana kwa jina la Carol Melkizedeck (70) ambaye alifariki muda mfupi na kusababisha foleni katika eneo hilo baada ya magari yaliyokuwa yamegongwa kufunga barabara.
Aidha, Kamanda Mkumbo ameeleza kuwa baada ya gari iliyokuwa imebeba matofali kuyagonga magari hayo ilipinduka na kuingia mtaroni, ambapo dereva na msaadizi wake walijeruliwa na kukimbizwa hospitalini.