Kuhusu kama ni wapenzi au la, imenikumbusha enzi za kusoma kitabu cha Wakati Ukuta, wakati mhusika mmoja alisema hakuna urafiki kati ya mtoto wa kike na wa kiume. Kwenye mila zetu hasa katika mazingara ya vijijini, watu huwa wanachanganyikiwa ukimpeleka rafiki wa jinsia tofauti. Nilihisi kuchanganyikiwa huko kutokana na baadhi ya maswali ya babu.Kwa mfano, babu aliuliza swali kuwa je unafaidika na kuwa na binti yetu huko kwenu? ( kijana alijibu kwa njia ambayo mimi nilidhani amekwepa swali. Alisema kitu kama oh ni vizuri kuwa binti anasoma na anajitahidi. ( sijui hiyo lugha lakini binti ndiye aliyekuwa anatafsiri maswali ya babu yake.)
Na kuna mahali kijana anasema kuwa aliogopa babu asije akamuweka kwenye spot.
So in my opinion there is something cooking, I just don't know whether it is a cup of tea or sufuria la makande.