Mtu kuwa na kende (Testis) moja je ni tatizo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtu kuwa na kende (Testis) moja je ni tatizo?

Discussion in 'JF Doctor' started by Ulimbo, May 4, 2012.

  1. Ulimbo

    Ulimbo JF-Expert Member

    #1
    May 4, 2012
    Joined: Aug 14, 2009
    Messages: 678
    Likes Received: 41
    Trophy Points: 45
    Wana JF, naombeni msaada wenu kwa anayejua. Kuna mtoto wa kiume alizaliwa na kende (Testis) moja ndo inaonekana. Sijui ili linaweza kuwa tatizo kwake kiafya au haina tatizo; na kama ni tatizo nini kifanyike?
     
  2. brazilian

    brazilian JF-Expert Member

    #2
    May 4, 2012
    Joined: Feb 10, 2012
    Messages: 607
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 0
    Kende moja halina shida mradi lisiwe na tatizo kiafya. linafanya kazi kama kawaida. taabu yake na lenyewe likiathirika maaana hakuna spare.
     
  3. vicent tibaijuka

    vicent tibaijuka JF-Expert Member

    #3
    May 4, 2012
    Joined: Mar 22, 2012
    Messages: 276
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 0
    inabidi kachunguzwe hospital. kwa kifupi ni kwamba wakati mtoto anakuwa tumbono mwa mama kende huwa tumboni mwa mtoto, lakini baada ya muda fulani (kama week ya 5-8) hushuka, ila kuna wengine huwa hazishuki, ndo maana baada ya kuzaliwa mtoto hospitalini laziwa akaguliwe ile mifuko ya kende kama zote zimo. na kama zinakoeskana, lazima wasubiri kama week 4 hivi kuona kama zinashuka, la sivyo hufanyiwa operation ili kuzishusha. kama kendo moja hiyo itafanya kazi ni vizuri, lakini katika uychunguzi wengi wamegundua huweza pata matatizo katika uzazi, au ile kende iliyobaki ndani kuleta matatizo. lakini kama hata kule ndani haipo basi hakuna matatizo yatakuwa niu maumbile yake tu. cha muhimu nenda kwanza hospitali kwa uchunguzi na ushauri.
     
  4. Ulimbo

    Ulimbo JF-Expert Member

    #4
    May 4, 2012
    Joined: Aug 14, 2009
    Messages: 678
    Likes Received: 41
    Trophy Points: 45

    Nashukuru kwa ushauri wako, na nitaufanyia kazi
     
Loading...