Mtu kujipima mwenyewe UKIMWI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtu kujipima mwenyewe UKIMWI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 10, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  IDHAA YA KISWAHILI / Masuala ya Jamii[​IMG]
  [h=4]Masuala ya Jamii Dw[/h][​IMG]
  [h=2][/h]

  Marekani imetangaza kuwa inaruhusu kuuzwa kwa chombo cha kupima virusi vinavyosababisha UKIMWI kwa binaadamu vya HIV. Chombo hicho sawa na kijisanduku kidogo kitawasaidia Wamekani kujipima wenyewe HIV majumbani .
  Badala ya utaratibu wa sasa wa kwenda hospitalini na katika vituo maalumu vya Afya kutambua afya zao. Kiongozi wa Mamlaka ya Chakula na dawa wa taifa hilo (FDA) na Kampuni iliyofanikisha kutengeza kikasha hicho ya OraSure Technologies cha kupima virusi vya HIV1 na HIV2, kwa pamoja wanasema hatua za tekinolojia hiyo ni kubwa katika kupambana na maambukizi ya UKIMWI.
  [​IMG]Alama ya kuonyesha kujali na kujikinga na UKIMWI

  Ute na mate kuchukuliwa kutoka mdomoni
  Wamesema anachotakiwa mtu kufanya ni kuchukuwa ute au mate yaliyopo katika kinywa chake kwa kutumia vifaa maalumu na kusugua katika fizi za juu na chini kisha kuweka ute huo katika kipimo ambapo baada ya dakika kati 20 na 40 jawabu hupatikana
  Kifaa hicho kinatarajiwa kupatikana kwa matumizi mwezi oktoba mwaka huu kwa wauzaji wa maduka ya rejareja zaidi ya 30,000 watakaokuwa na uwezo wa kuuza kifaa hicho ambacho kinaweza kuwa msaada wa kupunguza kufunga safari kwenda vituo vya afya kupima.
  Mamlaka ya chakula na madawa ya taifa hilo imesema ni kweli kifaa hicho kinauwezo wa kupima ukimwi lakini katika watu 12 watakaopima mtu mmoja kuna dalili ya kuwa na majibu chanya wakati hana virusi vya ugonjwa huo ambao ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vya watu wengi duniani.
  Ufanisi wa kipimo hicho
  Lakini ufanisi wake ni kwa asilimia 92 wakati asilimia 8 inayobakia ndipo anaweza kupatikana mtu mmoja kuwa na majibu chanya wakati majibu yake ni hasi. Huwezo wa kifaa hicho unawekwa wazi kuwa unaweza kutambua aina mbili za virusi vya UKIMWI yaani HIV namba 1na HIV namba 2 ambavyo hapo awali ilikuwa vigumu kuweza kutambua kwa kipimo kimoja.
  Hali ya kwenda kwa wataalamu wa Afya kupata uhakika wa kupima haiepukiki kwani katika kila anayepima anashauriwa kuwaona wataalamu hao kuhakikisha suala hilo kwani si uhakikia wa asilimia100.
  Maoni juu ya utafiti mwingine
  [​IMG]Mtu akiwa ameshika kopo lenye vidonge vya kuongeza maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI

  Kulingana na utafiti mwingine uliofanya juu ya huwezo wa kipimo hicho unasema wazi kuwa kati watu 5000 wanaopima ni mtu mmoja tu anatapa majibu yasiyo sahihi kwa ungowa huo, ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Taifa hilo wanasema wanakubaliana nalo.
  Naye msemaji wa kampuni hii ya OraSure Technologies anasema bei ya kifaa hicho ni sawa na Euro 17 ambayo sawa na shilingi 3400 za Kenya na sawa na shilingi 34000 za Tanzania.
  Wakati huo huo Rais na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hii Douglas Michels anasema kifaa chao kitawasadia mno watu kupima na kutambua hali ya maambukizi ya UKIMWi kwa amani wakiwa nyumbani na wataklwenda kuwaona madaktari pale watakapo takiwa kufanya hivyo kwa matibabu zaidi.
  Kulingana na kituo cha Kupambana na Kujikinga na Mangojwa cha Marekani mpaka sasa nchi hiyo ina watu milioni1.2 wanaoishi na virusi vya HIV ambapo katika kila Wamerekani watano mmoja hatambui uzima wahali yake ya afya kama ana virusi hivi au la,huku kila mwaka watu 50,000 wanaambukizwa virusi vinayosababisha UKIMWI.
  Mwandishi:Adeladius Makwega/AFPE.
  Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman
   
 2. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Labda kinacho ku fascinate hapa ni kutumia mate badala ya serum/blood. Hizo Rapid Test kama SD bioline "Test yourself" zimejaa kwenye ma pharmacy hapa Tanzania, na watu wamekuwa wakizinunua na kujipima wenyewe Tofauti ni kwamba inabidi utumia damu Yaani una PRICK kwenye finger tip kama vile unavyopima malaria.

  All in all kabla ya kukubaliwa Tanzania lazima Kifannyiwe validation na Research Insitutions mbalimabli kama vile MUHAS, NIMR, IHI, KCMC, CUHAS etc
   
Loading...