MTU akifa anakwenda wapi?? Eleza unaelewa nini.

MTU akifa anakwenda wapi?? Eleza unaelewa nini.

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2011
Posts
3,768
Reaction score
5,634
Kwa takwimu ambazo hubadikikabadilika kulingana na mazingira, watu 150000 hufariki kila siku hapa duniani au kwa maana rahisi kila sekunde moja watu wawili hupoteza uhai.

Kifo umekuwa ni gumbo kwa watu wengi hususani
makanisani, misikitini, kwa wapagani, masinagogini, wanasiasa, mila na desturi, wasomi n.k

Mfano:
1. Wapo wanaosema anakwenda mavumbini na hata lolote wala hajui chochote, tena Hana tofauti na mzoga wa mnyama yoyote ila pumzi ni upepo tu unakoma basi. Kusubiri kiyama/ufufuo.

2. Hubadilika na kuwa mijusi, ng'ombe, wadudu, paka etc hivyo unapoua viumbe hivi unaua watu.

3. Mwili unarudi kwenye vumbi Roho/nafsi inamrudia Mungu huko unaweza kuwa na utashi tena kanakwamba huyu MTU kubadilisha form na sayari tu.
4. Hulala, baada ya kuzikwa akimwagiwa maji anashtuka na kuanza kujibu maswali na kichapo kikali pale alipokosea watk akiwa hai.

5. Kunasehemu wako wafu/pagatori huko wametulia wengine wanateseka. Ila sisi tulio hai twaweza kuwaombea wakapunguziwa adhabu au hata kuamishwa kwenda sehemu bora zaidi.

6. Wanapotea milele hakuna uwezekano wa kurudi au kuhuishwa tena.

7. Ni kitendawili tunamuachie muumba mwenyewe maana hapo alituacha bila jibu. Hilo ni group lililochanganyikiwa na kukosa jibu sahihi.

8. Tunamzika lkn baadae anakuwepo tu ktk mfumo tusiomuona lkn hata ukimuona hashikiki. Ila ukitesa watoto wake atakuja akuadhibu au anaweza kufanya chochote cha kukuathili wew ulie hai.

9. Wako makabulini tu, wanapiga stories tena ukikosea ukapita usiku unaweza kudhuliwa na hao maiti maana umewaaribia maongezi yao.

10. Kifo hakuna uhusiano wowote na imani wala Mungu. Ila ni Matokeo ya tabia nchi au mambo ya kimazingira tu.

.......
N.k


Wew unaamini nini na kwa uthibitisho UPI au hoja IPI.
 
Back
Top Bottom