Mtoto.

Mtoto.

Globu

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
9,093
Reaction score
2,604
Mtoto katoka shuleni huku analia, alipofika nyumbani. Baba yake akamuuliza ''unalia nini'? MTOTO '' Nimepigwa na mwalimu na nimeambiwa twende wote shuleni''. Wakaenda shuleni na wakaingia ofisini. MWALIMU ''Karibuni, mtoto wako tumemuuliza Nairobi iko wapi kashindwa, ndio maana tumemchapa'' Baba akamgeukia mtoto wake na kumpiga vibao, akamwambia ''mpumbavu mkubwa, kila siku nakukataza kuchezea vitu vya watu hukomi, haya NAIROBI ya mwalimu umepeleka wapi'?
 
Duh mshua ni mbulula square, naye anastahili kichapo toka kwa teacher
 
hahahahahahaha.....dingi noma.

  • :target:
 
Ha ha haaa!nadhani mzee alisoma chini ya mwembe,embe likidondoka mapumziko,mvua ikinyesha likizo na jua likiwakali mwisho wa vipindi!!..
 
Inaonesha huyo mtoto ni mtukutu sana,inawezeka aliiba Nairobi ya mwl akasahau alikoificha ndio maana hasemi.Hapo mkong'oto tu na atasema alikoipeleka.
 
Hata mie naafiki mtoto anajua NAIROBI iliko,maana hata baba yake anfahamu utundu wa mwanae ndio maana alimkataza kuchezea vitu vya watu ikiwamo NAIROBI!
 
Kupoteza NAIROBI si mchezo, lazima ale kichapo. Teh teh teh teh teh teh teeeeeeh, mimi nilivunja assemble walimu walikomalia mpaka nikalipa
 
Back
Top Bottom