Kijana kijana
JF-Expert Member
- Mar 11, 2018
- 2,546
- 2,625
Uko sawa miss chura unachosema.Aaaah Mkuu vitu vya mtoto ukisema ununue utachezea tu hela Na kujaza nyumba bure.huyu wala hasukumi vitu yeye anakimbia tu ovyo
Huwezi kumnunulia mtoto gari ajifunze kutembea.
Mbona kutambaa alijifunza bila gari au kitu chochote?
Katika maisha ukiona kuna jambo unalikosea sana basi jua kwamba upo katika steji kubwa ambayo hayo makosa yatakufanya uwe mtatuzi hapo baadae.
Ndiyo maana wazee wetu walikaa sana katika ndoa zao kwasababu walikosea na kukoseana sana katika ndoa baadae wakawa wanajua namna gani ya kuyamaliza matatizo kwa kuwa walishayapitia na kupata uzoefu kwayo
Sasa huyo mtoto anaanguka anguka(anakosea kosea kwa kujifunza kutembea)
Jua hapo hiyo ndo steji kubwa na ya mwisho ambayo kaifikia Mkuu.
Au kuna kupaa baada ya kutembea?
Bila shaka hiyo ndo steji ya mwisho kwa maana ni steji kubwa ambayo akiiweza tu basi atadumu nayo mpaka anazeeka lakini kaifuzu tokea utotoni.
Hivyo dada yangu Kukosea kwake saaaana kutembeaa huku anaanguka wallahi isikupe taaabu kabisa,jambo lingine ni kuwa mtoto wako usimuinue anapoanguka utamdomaza kiakili.
Kumbuka anapoanguka ukamuacha ujue atajifunza na kuinuka.
Akianguka ukamuinua utakuwa umenyima haki yake ya kujifunza kuinuka pale anapoanguka.
Mwishowe atakuja kutembea(kujua)alafu akianguka(akikosea)atakuwa hajui namna ya kuinuka(kurekebisha kosa)
Kwani mtu sahihi ni yule anayejua kwamba akikosea vipi afanye kurekebisha tatizo.
Hivyo basi wakati wa utoto wa mwanao mtengenezee mazingira ya kuwa ni mtoto mwenye akili ya juu kwa kutomuangaliaa saana.
Acha ajifunze mambo mbali mbali katika dunia yake.
Ukimjali sana umkataze kila kitu utamjengea mazingira ya kutokukumbana na changamtoto.