Mtoto wangu ana tatizo gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wangu ana tatizo gani?

Discussion in 'JF Doctor' started by Hmaster, Jun 18, 2011.

 1. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wanaJF!
  Mimi ni baba wa watoto wawili: mmoja ni wa kike mwenye miaka 9 na mwingine ni wa kiume mwenye miaka mitatu na miezi mitatu. Tatizo lipo kwa huyu wa kiume kwani hadi sasa bado hajaanza kuongea wala kufuata maelekezo ingawa ni mtundu sana. Akiwa na miaka miwili na zaidi tulijaribu kumpeleka kwa madaktari kadhaa ili wamchunguze kama ana tatizo lolote, lakini walitujibu kwamba alikuwa hana tatizo lolote katika afya yake. Anasikia vizuri, ana uzito unaoendana na umri wake, kinywa na koo lake havina matatizo yoyote na hivyo kututaka tuwe na subira kwa vile watoto wanatofautiana katika makuzi hata kama watakuwa wamezaliwa na wazazi haohao. Tangu wakati huo hadi leo hajaongeza chochote kwa matamshi ila anaweza kutamka silabi tu kama ma, ba, bi, ta, sa, si, da, chi, nk bila kuziunganisha wala kudhumunia chochote na kwamba akitaka kitu kama maji anamshika mtu mkono mtu wa karibu yake na kumuelekeza kwenye friji au mtungi wa maji. Anafanya hivyo kwa chakula na mengineyo.
  Sasa mimi nina wasiwasi na mwanangu ana tatizo gani linalosababisha achelewe au ashindwe kuongea hadi umri huo? Nawaomba msaada wenu wa kitaalamu au wenye uzoefu na hili mnipe matumaini au uelewa!
   
 2. p

  plawala JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole mzazi
  umeainisha tatizo moja kubwa ni kutoweza kuongea mpaka sasa hv na ana miaka 3
  lingine umesema ni mtundu,unaweza kuelezea utundu huo ukoje,mfano anapenda sana kuchezea vitu?
  je ana tabia fulani inayorudiarudia?yaani anafanya kitu au matendo fulani tena na atena?
   
 3. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Aisee pole sana. Najua kuna watoto wanachelewa kuanza kuongea hasa kama hawana company ya kutosha nyumbani. Ila sina uhakika mtoto anatakiwa aanza kuwa fluent na miaka mingapi. Jaribu kuwaona wataalamu wa watoto hasa wahindi kwani wao wana network wanaweza uizia mdoctor wenzao huko India. Otherwise, jaribu ku google kuhusu child development.
   
 4. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  [h=2]Labda hii itakusaidia (nimecopy online)

  When will my child talk?[/h]
  In my work with families for over 20 years, I have heard this question perhaps more than many others. Often parents wait for language as they would wait on a bus, sensing no control over when it comes. Unlike when a bus comes, the onset of language is usually something parents have influence to a very great extent.
  When do children begin to talk a little? Under usual circumstances, we expect a child's first words around 10-18 months. There is no set time table and many children begin much later and still develop good language for conversation and learning. And, a child may talk with some persons and not others. If a child is not using words to play and get needs met by age two, roughly, we want to look at how he is doing in those skills he needs before language.
  So another common question is, "What does a child need to do before she regularly talks and learns language on her own?"
  After years of interviews with parents, I conclude that many parents believe that language just comes automatically like hair and height, with no special help from families other than general care taking. While it is true that human beings do have a unique ability to talk as part of their genetic programming, language just doesn't happen on it's own; a child needs close contacts with people who do things she can do.
  So, if you are concerned that your child may be slow to talk, I recommend that you do not expect that she is just going to grow into language without your help as she seems to grow into new clothes without specific help.
  To develop a really useful language for friendship and learning, your child needs to get into several habits that we do not often think of as necessary to talk. Some of these habits are playing with people; playing meaningfully with things; imitating; turntaking; staying in interactions; communicating without words; genuinely enjoying contact with people and others.
  Frequently, parents bring me children 3, 4, 5, 6, or years older, who either have not begun talking or talk mainly for themselves. These parents often feel they have done all the regular play and teaching that they gave their other children, and they conclude that something is wrong in the child.
  Some very common parent reports happen over and over with many different kinds of children. "He didn't play like other children." "He pays little attention." "He isn't interested in new things." "He repeats a lot of things." "He gets what he needs by taking us there or making unclear sounds." "He doesn't enjoy close quiet time with people." "He prefers to be alone." "He often ignores people." "He can't seem to keep up with others." All of these common comments by parents reveal a genuine concern, and often anxiety, that their child is not learning to talk.
  So, what's the answer to the question, "When will my child talk?" In my experience following the communication development of children in over 500 families, the answer is-When they develop certain kinds of relationships with people who enter their world and become partners with them at their pace.
  I have encouraged many parents to stop expecting language to come "out of the blue", and instead to look at themselves and the remarkable power they have to help their child to talk. A major goal of mine has been to teach parents what children need to do before language and, just as importantly, to teach them natural ways they can change themselves to help their child learn more with them.
  For this short letter, I will alert you to some very important things both you child and you can do regularly that have helped other children get ready to talk. Notice that when you read the list you may say two things; first, that he and you have done these things already. That may well be true, but at the time your child may not have been ready to make it a habit or not yet done it on a regular, steady basis. Second, you may say, those are baby things my child is a big girl now, and I don't want to go back. My answer to that is that children of all ages can learn things they did not learn at earlier stages if they have enthusiastic partners to support and coach them.
  With the list below, rate yourself and your child from 1-5, with 1 meaning never, 3 indicating occasionally, and 5 showing things you do consistently.
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="width: 50%"]
  WHAT THE CHILD NEEDS TO DO
  [/TD]
  [TD="width: 50%"]
  WHAT YOU NEED TO DO
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 50%"]Play frequently with people[/TD]
  [TD="width: 50%"]Play frequently as your child does[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 50%"]Play meaningfully with things[/TD]
  [TD="width: 50%"]Match child's actions and communications[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 50%"]Imitate others' actions and sounds[/TD]
  [TD="width: 50%"]Wait--give child time to do his part[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 50%"]Take turns[/TD]
  [TD="width: 50%"]Show child a next step[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 50%"]Stay increasingly longer with people[/TD]
  [TD="width: 50%"]Take turns and keep child longer[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 50%"]Use gestures and sounds to communicate[/TD]
  [TD="width: 50%"]Attend to little steps like sounds & gestures[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 50%"]Actively enjoy playing with people[/TD]
  [TD="width: 50%"]Make play more fun than work[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 50%"]Show interest in new things[/TD]
  [TD="width: 50%"]Expect your child to do more[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Previous: What do children need to do before they talk?
   
 5. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Pole mkuu.
  Nafikiri usijenge hofu kuwa labda kijana atakuwa bubu.
  Nyumbani kwetu sisi wazee walikuwa wanasema, mtoto anachelewa kuongea kwasababu hajaona haja ya kuongea. Kwa hiyo mara nyingi mtoto ambaye amechelewa kuongea, walikuwa wanambadilisha mazingira, kama vile kwenda ugenini kwenye nyumba zingine, au kuona vitu ambavyo alikuwa hajaviona kabla. And it used to work. Unashangaa tu mtoto anatamka maneno ambayo ulikuwa hujamsikia kabla.
  Vinginevyo jaribu kucheza naye sana, na mvumilie kwa sasa.
  Ushauri huu si wa kitaalam. Ni maoni tu from experience.
   
 6. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole mkuu, nina imani ataongea tu. Zidisha maombi na kama utaweza mbadilishie mazingira, mtafutie shule ajichanganye na watoto wenzie ataongea tu.
   
 7. usofu

  usofu Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Pole mkuu, mm pia imewahi kunitokea. Mtoto wangu amezaliwa bila matatizo yoyote but amechelewa sana kuongea nimehangaika nae sana hosp. Ila nilichokifanya nilimuanzisha chekechea akiwa na miaka minne na alikuwa hawezi kutamka neno hata moja. Nikaona mabadiliko akawa anatamka but kwa shida sana, cha ajabu alipofikisha miaka sita akili ikafunguka kwa kasi nikaamua nimuanzishe primary na sasa yupo darasa la tano.Hivyo mkuu jitahidi kwenda nae taratibu atafunguka tu na usisahau kumshirikisha MUNGU.
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole sana kaka ila jaribu kumpeleka shule akacheze na wenzie kwa masaa kadhaa utaona mabadiliko,,, kuna play school nyingi tu mpeleke atachangamkaa tuu
   
 9. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru sana wote mliochangia mada yangu. Ninaahidi kuyafanyia kazi yote mliyonishauri nikiamini yatamsaidia mwanangu. Mungu awabariki!
   
 10. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama walivyoishauri wengine, shule ni dawa kwake, anapokuwa na interaction na watoto wenzie itasaidia kuongea. Pia pengine hapo home kwako hana interaction na watoto wengine, hiyo pia huchangia sana kuchelewesha kuongea kwa baadhi ya watoto. Kama madaktari walikuambia hana tatizo basi come down tu ataongea tu.
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,120
  Likes Received: 6,600
  Trophy Points: 280
  Ataongea kitu, usianze kuwa na wasiwasi, watoto wote ni wa MUNGU mwenyewe, hivyo mwambie unachotaka afanye kwa mtoto wako na atafanya kwa jina la YESU KRISTO.
   
 12. A

  Aine JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwanza muombe Mungu amfungue, huyo si bubu kabisa kwani ameshaanza kutamka baadhi ya maneno. Amechelewa kuongea tu ila kwa msaada wa Mungu ataongea. Ila kama wewe ni mkristo mpeleke sunday school kanisani walimu wa watoto watamfundisha na kumuombea, pia muanzishe shule (baby class) akiwa na wenzake kule shule wakiwa wanacheza atajifunza kuongea kama wenzake na atabadilika tu, ila muombee kila siku usichoke Mungu atamfungua tu. Hata mtoto wa jirani yangu ana miaka karibu mitano haongei vizuri yaani hatamki vizuri maneno na wakati mwingine unaweza usimuelewe anaongea nini, lakini kadiri siku zinavyoenda ana-improve kidogo kidogo
   
Loading...