Mtoto wa Wassira ajiunga Chadema

Mtoto wa Wassira ajiunga Chadema

Tyson kabla ya kurudi ccm alikuwa mbunge kupitia upinzani, alitenguliwa ubunge na mahakama baada ya warioba kumpinga. njaa tu ndio ilimrudisha ccm.
 
itv:dr. slaa amewakabidhi kadi za chama watoto wa wassira Esta wassira na lilian wassira waliohamia chadema leo kwa kudai wamevutiwa na sera hasa m4c na kwamba awajal ukada wa mzee.
 
Wangeniomba ushauri ningewaambia huu si wakati wa kuingia katika siasa kwa umri wao kwasababu hawatanufaika zaidi ya majina yao kutumika kisiasa kuvutia wengine. Kwani si lazima niwe mwanachama wa chadema,ccm au cuf hasa ukizingatia siasa zao za kuchafuana majukwaani, mwanasiasa anataja mabaya ya kingine mara 24 halafu mazuri ya chama chake kataja mara mbili sasa hapo siasa yenye mtizamo wa kitaifa iko wapi?

Kwahiyo ni vema ukabakia kuwa mpiga kura usiye na upande kwa sasa ili utendee haki nafsi yako na niwe huru na kura yangu moja mwaka 2015.

Huu ni msimamo wangu binafsi, unaweza kunikosoa hasa ukiwa mshabiki wa siasa za watu binafsi.
 
Wengi watakuja na hata hivyo UKWELI siku zote haijawahi kushindwa na ubatili kama ilivyo ya ccm!
 
Wekeni picha,nataka jua kama wamefanana na mzee au
Angel
Hii ni below civilization, una maana gani kutaka kuwadhalilisha hawa mabint, wewe una uzuri gani? Heshima ni kitu cha bure, hata kama humpendi baba yao, hawa haiwahusu ni dhambi kumbwa kuwaingiza.
 
wamesha faidi jasho la walala hoi!!!! ndo wakuja kujfcha chadema! .............poa2 wakaribie
 
Hata Wasira siyo mwana ccm, nani hajui hilo?
 
Hawa Chadema ni kuokoteza watoto wa vigogo tu sasa

Mwenzangu unamaanisha ni kosa gani mtoto wa mtumishi wa serikali au chama kingine kujiunga na CHADEMA? kila mtu ana haki sawa kuchagua chama anachoona kinaendana na fikra zenye kuleta maendeleo katika jamii ya watanzania.
Do not judge a book by its cover!!!
Hiki ndo ninaipendea Tanzania tunaanza kukua kidemokrasia, kila mtu ana haki ya kutoa duku duku lake.
 
Sio mabinti wa Wasira (waziri wa mahusiano) bali ni mabinti wa mdogo wake wasira aitwae George Wasira.
 
Back
Top Bottom