Mtoto wa Wassira ajiunga Chadema

Karibu CDM Makongoro Wassira,ila angalizo kupeana sio jambo baya,ni kwamba kama umekuja kwa dhati na kwa kuuelewa ukweli CDM ni mahala pake mpaka leo hii na naamini itakuwa ni mahala salama na penye kufaa kufanya kazi za siasa,kuunganisha nguvu na viongozi wetu ili kuikomboa nchi yetu kutoka mikononi mwa mafisadi,na ni sehemu sahihi kwa vijana kutumia fursa na uwezo wao wa kuongoza na kuleta mabadiliko chanya hasa kwa kundi husika.ila sina uhakika na life style ya nyumbani kwenu kwa dingi yako,maana sidhani kama utakuwa tayari kuwa-attack mafisadi wakati dingi ni mchezaji wa timu pinzani,anyway huenda hata yeye alisha kuchana ukweli kuwa ilikuwa ni njaa tu.ila ukiwa kama umekuja kichina for sure CDM hawana uvumilivu na ukiukwaji wa maadili ya chama.wanautamaduni wa kumshughulikia haraka kiongozi au mwanachama wa kawaida pale inapothibitika pasi na shaka umeharibu.
Karibu sana M. wasira,zingatia angalizo nililokupa.
 
yaacheni magugu na ngano yamee kwa pamoja, wakti ukifika tutajua cha kufanya
 
Kwahiyo huyo kijana credential pekee anayoweza kujivunia na ambayo chadema imeiona asset ni utoto wa Wassira!!!

Kuna saying yake ambayo inatoa political advantage, Pasco atanisaidia kuisemea

Leo mtoto wa Romney mfano akimendorse Obama si haba


Ridhiwani Kikwete akijiunga na CDM lazima habari itakuwa 'mtoto wa rais' na ndio maana umefungua habari hii kuisoma
 
Mimi nadhani kila mmoja ana haki ya kutumia nafasi yake ya kidemokrasia, umakini wa cdm ni jinsi ya kuyavumbua mapandikizi na siyo kuangalia mtu alikotokea. Katika familia moja baba aweza kuwa simba na mama yanga. Hii inatokana na tofauti ya kimtazamo
 
Wakuu, kama huwa mnasoma Gazeti la Raiamwema, ile sehemu ambayo Dada mmoja huwa anamwandika barua Mchumba wake Frank, huyo dada hua anajiita Hidaya, nadhani mtakuwa mnaelewa, wahusika wakuu kwenye hiyo makala ambayo hutoka kila wiki ni Waziri mmoja kwenye serikali ya mikiki, mke wa waziri huyo almaarufu kama MB, then kuna Hidaya mwenyewe na binti boss a.k.a BB, mara nyingi sana huyu BB htofautiana sana na baba yake ambaye ni waziri, mtizamo wake saa zote huwa umekaa ni CDM zaidi tu, ninahakika mwandishi wa makala hiyo ameisha fanya research ya kutosha kwenye hizo nyumba za wakubwa na kugundua mengi tu, ukweli watoto wengi wa wakubwa hawakubaliani kabisa na hali halisi ya jinsi magamba wanavyo endesha nchi, nina mfano 1, Kingunge mmoja wa usalama wa Taifa huwa na wakati mgumu sana nyumbani kwake, watoto wake wote incuding mke wake wote damu yao ni upinzani tu, hukia hatua watoto wanamwambia baba yao na kwamba wao ni vidole viwili tu, so please msimhukumu huyu dogo Wasira JR. hiyo ndio hali halisi wakuu, wengine hawawezi kuwa wanafiki, roho zinawauma, kuongelea/kusifikia kitu usicho kiamini, walio wengi hawawezi, maanake unakuwa kama mtumwa hivi, saa zote roho inakusuta!
 
Katika watu wanaikashifu Chadema na kuwa na maneno ya maudhi ni Waziri Wassira. Sasa kwa kuonyesha kuwa M4C haina msamaha hata kwa familia yake mtoto wake aishie USA aitwae Makongoro Wassira amejinga na M4C. Akizungumza wakati anakabidhiwa kadi alisema yeye ni wa kwanza tu kujiunga M4C lakini ndugu zake wote wapo mbioni kujiunga na anadhani baba yake pekee ndie atabaki CCM. Peopleeeeeeeeeeeeeeee power.

IMG_1641.JPG

Viongozi wa Tawi la Chadema Houston wamkabidhi Kadi ya Chadema Makongoro Wassira
Angalia picha hapa CHADEMA USA

Huyu ni lazima apelekwe mstari wa mbele wa mapambano. Si lazima baba akichemka na watoto wawe hivyo, ninataka kuamini kuwa vijana popote walipo wamechoshwa na uvunjivu wa haki za binadamu unaofanywa na watawala wa kaya hii. Pia hii ni dalili kuwa hali huko chama cha magamba si shwari.
 
Kwa jinsi Wasira anavyochukia upinzani sidhani kama hakuna mchezo mchafu unaotaka kuchezwa hapo. Kumbuka hata baba yake aliwahi kutumika kama mamluki ili akavuruge upinzani

Mchezo mchafu umekwama kuchezwa na vigogo wote wa CCM vikiwemo vyombo vya dola ataweza huyu dagaa? Sioni sababu ya kuhofia viumbe wadogo kama hawa.
 
Chadema tuwe makini si kila kingaacho ni dhahabu,tunateswa na shibuda,zzk hatujakoma tu? Tusishabikie kila kitu jemeni

Wewe zitto anakutesa kwa lipi kama sio unafiki wako? Hapo hata kadi huenda huna ushabiki usio natija,huyo Dr Slaa mwenyewe alikuwa gamba zuri mpaka wakammwaga kwenye kura za maoni ndio akahama ccm,zitto ni mfano hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote zaidi ya chadema,kajiunga cdm kikiwa hakina hata mvuto,eti leo hii na wewe unalalamika zitto anakutesa unafiki mbaya sana
 
Baada ya kumwuliza Nape kwa simu juu ya Mtoto aw Wasira, Nape kaniambia eti Huyo naye ni gamba na dizeli chafu ambalo linachimbia kabuki CCM
 
Chadema hawaokotezi ila hao generationext wana mtazamo..."mtu atamwacha baba yake na mama yake na kujiunga CDM mwenyewe"
 
Katika watu wanaikashifu Chadema na kuwa na maneno ya maudhi ni Waziri Wassira. Sasa kwa kuonyesha kuwa M4C haina msamaha hata kwa familia yake mtoto wake aishie USA aitwae Makongoro Wassira amejinga na M4C. Akizungumza wakati anakabidhiwa kadi alisema yeye ni wa kwanza tu kujiunga M4C lakini ndugu zake wote wapo mbioni kujiunga na anadhani baba yake pekee ndie atabaki CCM. Peopleeeeeeeeeeeeeeee power.

IMG_1641.JPG

Viongozi wa Tawi la Chadema Houston wamkabidhi Kadi ya Chadema Makongoro Wassira
Angalia picha hapa CHADEMA USA

Ish!!! Mbona huyo siyo mtoto wa Steven!
 
Back
Top Bottom