Mtoto wa Mkulima analima wapi?

Huyo anafaa kukodiwa kwa ajili ya kulia misiba ya wanene lakini si kusimamia maendeleo, hawezi kabisaaaaaaaaa!
 
pm gani anavaa tshirt ya tusker bwana huyu ni mnywaji sio mkulima, huyu ameshamaliza kulima sasa hivi anavuna. Nashut down
 
anavuna posho laki 200,000 kila siku bila jasho angekuwa mtoto wa mkulima si angekataa
 
Kila mtu anataka VX V8 wakurugenzi pale wizarani,mawaziri wote wanalilia mashangingi mimi nashangaa kabisa waziri mkuu akilialia bungeni.
 
Analima pale mjengoni maana ndio anaongoza vikao vya kuongeza posho, yeye mwenyewe anaita hizo posho ni urinaji wa asali, na ana nguvu zaidi kwenye kushauri viongozi wa upinzani waende mahakamani na wala sio kwenye chama chake.
 
Mkulima gani huyu anayelialia kila wakati badala ya kufayna maamuzi ya maendeleo.................uwezo wote kikatiba anao lakin sijui anasubiri aje autumie wakati gani?
 
Salamu wana JF,

Kila kukicha majina wa sifa yanaibuka. Siku moja likaibuliwa jina la 'Mtoto wa Mkulima' maana yake ikiwa ni kuwajali wakulima wa Tanzania na watu wengine wenye kipato cha chini, hii ilitokea mara baada ya kupendekezwa, kupitishwa na kuapa kuwa kiongozi mkuu wa serikali bungeni.

Tumaini la watanzania likawa ni kuwa na maisha bora mara baada ya kuongozwa na mtu (maskini) mwenzao. Tofauti na ilivyotarajiwa mtoto wa mkulima hajulikani analima wapi au anawalimia wakina nani?. Kwanini haonekani hata shambani wakati watu wanauana Arusha, migodi ya madini inaua watu, mkuu wa bunge anapandisha posho, vigogo wanatibiwa India, madini yanaibwa, matunda yanaozea shambani kwa kutaja machache. Mtoto wa mkulima kweli anasimamia shamba la baba yake, ameshindwa au amelewa ulanzi?

Ushauri wangu kwake ni kumtaka asimame pamoja na maskini wenzake aseme sasa basi, sisi tunajiweza kwasababu tuna raslimali tunazo za kutosha............!

Wengi hjatukumuelewa!!
Yeye alisema ni MTOTO WA MKULIMA,
Hakimaanisha yeye ndio mkulima,
Ye ni fisadi tu kama wengine, ila babaake ndio mkulima!!
Umeelewa sasa??
 
Ana chuo chake cha VETA maeneo ya mikwambe kigamboni kinaitwa MKULIMA VOCATIONAL TRAINING CENTRE.
 
pm gani anavaa tshirt ya tusker bwana huyu ni mnywaji sio mkulima, huyu ameshamaliza kulima sasa hivi anavuna. Nashut down

4.jpg


1+%252815%2529.jpg
 
Asante sana kwa respondingi zetu nzuri, hii inaonyesha wazi kwamba baadhi ya waliojiita / wanaojiita na watakaojiita watetezi wetu si watetezi. Nimependa sana mawazo yenu na nimependa zaidi aliyeweka picha, hii inadhititisha kwamba mtoto wa mkulima alilewa na nahisi anaendelea kulewa kama nilivyohisi.
 
Back
Top Bottom