Mtoto wa miezi mitatu hakui

RUJEINER

Senior Member
Jan 18, 2018
129
152
Habari zenu.. natumain ni wazima wa afya na wale wagonjwa poleni Mungu atawaponya.

Nina mtoto wa miezi mitatu huyu mtoto shida yake kwenye ukuaji yaan haongezeki kilo..alipata shida kidogo wakati alipozaliwa alikua hataki kunyonya ila baada ya wiki moja mbele alianza kunyonya..kwa sasa ana kilo 4 tu.

Ushaur wenu nifanye nini ili mtoto huyu aongezeke na akue.

Asanten.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Atakuwa ananyonya afu hashibi,mwanzishie maziwa ya kopo ataongezeka kilo.Na mama asiwe mvivu kumnyonyesha.
Habari zenu.. natumain ni wazima wa afya na wale wagonjwa poleni Mungu atawaponya.

Nina mtoto wa miezi mitatu huyu mtoto shida yake kwenye ukuaji yaan haongezeki kilo..alipata shida kidogo wakati alipozaliwa alikua hataki kunyonya ila baada ya wiki moja mbele alianza kunyonya..kwa sasa ana kilo 4 tu.

Ushaur wenu nifanye nini ili mtoto huyu aongezeke na akue.

Asanten.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile ap
 
Mkuu kwanza pole Sana kwa Hilo tatizo hakika inaumiza mama kumuona mwanae hasongi mbele iatika ukuaji lakini hiyo itapita Ni suala la muda tu.

Mimi pia niliwahi kupata hyo shida mwanangu alozaliwa na 2.8kg lakini maziwa yalikauka akawa hakunyonya akarudi Hadi 2.1kg Sasa Yani kuirudisha Ile afya ilinigarimu muda mrefu kidogo Hadi anafika miez minne ana kilo5.5. nilikua najitahidi Sana kumnyonyesha kila wakati na Mimi nilikua nakula vyakula vingi kuhakikisha maziwa yanakua na virutubisho.

Ushauri wangu Kama mtoto hasumbui kwa kulia unaweza kutulia tu ataendelea vizuri lakini kama unataka uhakika zaidi wa afya ya mtoto mpeleke kwa wataalam wa watoto
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom