Kalpana
JF-Expert Member
- Jun 16, 2017
- 26,833
- 50,015
Kama ni mtoto wa kwanza wamama wengi huwa hatujui kunyonyesha vizuri watoto. Ila baadae nilipofundishwa wtt wangu walofata walikua wana gain haraka sana. Unachotakiwa kufanya usimnyonyeshe mtoto ziwa moja dkk chache mara ushamwamishia tena upande mwingine. Maziwa yamegawinyika mara mbili kama sikosei fore milk na maziwa yanayofata. Ya mbele yanajaa maji tuu hivyo ukimnyonyesha hayo ya mbele utaona kama ameshiba ila sio kushiba vzr amejaza tuu maji hayana virutubisho muhimu na sio mazito so hakikisha mtt ananyonya ziwa moja hata kwa dkk 15 mpk yale maziwa ya nyuma yaliyo mazito na yenye wingi wa protini yaishe. Hata kama akionekana ameshiba muache kidogo kama dkk tano then arudie ziwa lile lile mpk uone limenywea. Kama hili lingine litakua limevimba sana maziwa yamejaa sana unaweza anza kwa kuyakamulia nje then ndo umpe anyonye sasa ili asipaliwe na hayo maana hutoka kwa kasi. Jaribu hivyo kama hufanyi hivyo.