Mtoto wa kiume, msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa kiume, msaada

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kaitaba, May 3, 2010.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Rafiki yangu wa karibu amenijia na shida yake, imenishinda nimeona niilete kwenu, nayo ni;

  Amebahatika kupata mali za kutosha, lakini bahati mbaya ana watoto wa kike tu, na mkewe amefungwa kizazi kutokana na kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua mala 3,

  Anataka apate watoto wa kiume japo wawili kwa njia yoyote ile, iwe ya kuokota mtoto wa kiume, kuzaa na mtu yeyote mradi mtoto akizaliwa awe wa kiume au vyovyote vile.

  Tunamsaidiaje?
   
 2. C

  Cozcoz Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wenye uwezo mjitokeze ili mapenzi yake yatimizwe!!!
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,775
  Trophy Points: 280
  hatuko Jf kushabikia uzinzi hata mara moja
  mkeo kafungwa kizazi mtoto wa nini.na nakuhakikishia kama mungu wa nazareti akiwa hai
  kama mali unaona zinamfaa tu MTOTO WA KIUME NAKUTANGAZIA KUZAA WATOTO WA KIKE
  hadi mwisho wako na kukuahikishia wa kike ndio watakaonda kuchambua mali zako

  UZAE NA BAAMEDI/BEKI TATU/HAWARA YOYOTE MWAMBI KWA ALIVYOANZA NAMTANGAZIA KUMALIZA
  WA KIKE KAMA ATATHUBUTU KUZINI....NENDEN MKAMUULIZE MFANYABIASHARA SUNDA WA ARUSHA SWALA LA WA KIKE NA WA KIUME
  ANAMJUA MUNGU NI NANI ALIFIKIRI MUNGU NI SUNDA UNAAMUA ANAVYOTAKA
   
 4. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Anayemjua Mungu hawezi kuhandika namna hii, kama hujaelewa thread unaweza kusoma upya, hapa kinachotakiwa ni msaada wa aina yoyote, mfano, unaweza ukawa na yatima, au mtoto aliyeokotwa jalalani wazazi wake hawajulikani, mkaenda kwenye vyombo vinavyohusika, akakabidhiwa au vyovyote vile, sio lazima njia moja wewe uliyoiona, tujaribu kujibu hread za wenzetu kwa nidhamu sio kama huyu jamaa,

  Nami kwa jina Mungu wangu aliye hai namuombea mema ajifunze jinsi ya kuchangia mada sio kukurupika.
   
 5. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kama shida yake ni mtoto wa kiume tu na yuko yaari hata kuokota basi aende mahosipitaliniau usitawi wa jamii ambako wanatunzwa watoto wengi tena wazuri sana waliotelekezwa na mama zao au watoto yatima aka adopt. Kama wewe ni Mwisilamu unaweza kuoa mke mwimgine ukajaribu bahat. Kama wewe ni Mkristo kumbuka kwamba ni kosa na tena ni dhambi mbele za MUNGU kuzaa/kuzini nje ya ndoa. HATA HIVYO NAPENDA KUMKUMBUSHA HUYO NDUGU KWAMBA MWANAUME NDIE ANAYE DETERMINE JINSIA YA MTOTO. HUYU BWANA ANAWEZA KUOA HATA WAKE KUMI LAKINI BADO AKAENDELEA KUPATA WATOTO WA KIKE TU
   
 6. Tshala

  Tshala JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 246
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kama anataka kwa njia yeyote ile basi hata ya ku adopt ni better, maana huyo mama hataiwezekana tena na kwenda kuzaa nje ya ndoa haitakuwa vema, while makubaliano ya kufunga kizazi wote waliafiki. After all mtoto ni mtoto haijalishi kike au kiume.
   
 7. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Napenda kuwashukuru wote waliochangia mada hii, ila ningependa mnisaidie namna ya kuadopt, maana nimeona wengi wameshauri hivyo.
   
 8. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  jamani kwa kweli nimeboreka na inanitisha kwamba katika kizazi hiki bado kuna watu wa mawazo haya. yani kweli hao watoto wa kike hawana haki ya kurithi hizo mali hadi wawe wa kiume? naomba niwe tofauti this is unfair and an insult, kwa mkewe, kwa hao watoto wake wa kike na hata kwa Mungu wake. Mungu ndo muamuzi mtu azae mtoto gani. Kama haridhiki kiasi hicho aadopt mtoto wa kiume lakini mkewe anaweza kummistreat huyo mtoto akijua anakuja kurithi mali za wanae. da hii imeniumiza personally aisee.
   
 9. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaitaba,umemuonaje ndugu Capt Didy????
  Maoni yangu,kama mchangiaji mwingine alivyosema-Capt Didy-USIWE UNAKURUPUKA,kama uko busy usiandike-soma tu uende zako.
  Kwako Kaitaba, kwa ulivyosema ina maana huyo rafiki yako wa karibu anachoangalia ni jinsia tu?Akiwa Mchina, Germany,American etc sawa. Maana nina source Albania hawana gharama yoyote,ili mradi ukamchukue mwenyewe.
  Nawakilisha.
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Huyo nae mtoto ni mtoto mie sina msaadahapa ..naona ana matatizo
   
 11. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  carmel-Is it mentioned anywhere kuwa Kaitaba anataka mrithi au sisomi vizuri?? Jamani kuhitaji boys and girls wakati mwingine sio sababu ya kurithi tu???Badilikeni mnatufuingiza akilini mambo ambayo hatunayo!!!dooooooooooooh!
   
 12. Mama Brian

  Mama Brian JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya mambo ya mtoto wa kiume au wa kike yamepitwa na wakati yuko dunia gani huyo?hizo mali awape hao hao watoto wake wa kike aliojaliwa na Mwenyezi Mungu.
   
 13. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  huyu mtu wako kabla ya kupewa ushauri katika hili anatakiwa kufanyiwa maombi kwanza! kwa nini haridhiki kupata watoto wa kike tu
  amini nakwambia, kama mungu hajapanga upate mtoto wa hautakuja kupata kamwe hata uoe wake 20! na hata kuadopt mimi simshauri,
  kwani huyo mtoto ndy awe mteule?....au?!! huu ucheshi, kwa nini asiwaamini hao watoto wake wa kike? amini nakwambia, mtoto wa kike anaweza
  kukufaa kuliko wa kiume! kauli za huyu jamaa zinaonesha hawaamini wala kuwajali watoto wake aliojaliwa na mungu. Mke wangu anatarajia kujifungua mwisho wa mwezi huu, hatujaenda kumchungulia mtoto kwenye camera za mionzi, akizaa mtoto wa kike nitafurahi sana na kumwita AIDA , akizaa mtoto wa kiume furaha yetu haittakuwa tofauti na wa kike, tutamwita TAMILA Jr.
   
 14. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,804
  Likes Received: 6,314
  Trophy Points: 280


  Kaitaba, jamaa yako anataka apate mtoto wa kiume ili AMUACHIE HIZO MALI ZAKE???

  Au anataka awe na mtoto wa kiume ndani ya nyumba tu? - kama ni hii, anaweza kwenda kuadopt kama wanavyoshauri wengine.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,359
  Trophy Points: 280
  Kuna jamaa Dar alikuwa anataka watoto wawili tu yeye na mkewe. Naddhani waliassume kwamba wangejaaliwa mtoto mmoja wa kike na mwingine wa kiume na hivyo kufunga kazi. Lakini mipango ya Mungu ilikuwa tofauti na ya kwao na hivyo watoto wote wawili walikuwa ni wasichana. Basi wakandelea kujaribu kwa matumaini ya kuja kupata angalau mtoto wa kiume mmoja. Sasa wana watoto sita wote wa kike na plan yao ilikuwa ni kuwa na watoto wawili tu. Ukijaaliwa watoto hata wasichana ushukuru Mungu maana kuna wengi duniani wanajitahidi kwa udi na uvumba hata kupata mtoto mmoja tu lakini bila mafanikio. Jamaa anaweza kwenda nje na huko akaendelea kupata watoto wa kike hakuna guarantee yeyote ile.

  Mchango wangu wa thumni.
   
 16. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #16
  May 17, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama ni mali atawapa wote, ila wasi wasi wake ni kwamba, hawa watoto wa kike wanaweza kuolewa na hizo mali zake zikasambaratika zote, lakini wa kiume ataoa na kuishi pale pale na kuziangalia vizuri mali hizo.
   
 17. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  u said it well cis, kama ana wanawake tu, waume zao ndo watakuwa wanaye wa kiume. Mshukuru Mungu kaka kwa kuwapata hao maana kuna wanaohangaika mchana na usiku kutafuta mtoto lkn hawapati!
   
 18. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  mwambie akubali matokeo!
   
 19. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  naona kweli mnahitaji msaada ndugu zangu.
  Hakosi mtoto akienda ustawo wa jamii. wana watoto kibao wanaohitaji walezi.
  au mseme mnataka kumsaidia mwenzenu aende nje ya ndoa ili apate watoto watakaompa hedeki baadae.
   
 20. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  agawe mali zake kwa watoto wake wa kike wote, itakayobaki ataaadopt mtoto wa kume nae apewe kilichobaki! hivi jamani kuwa na mtoto wa kiume ni muhimu sana? mi nilifikiri mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu kila aliekupa awe wa kike au wakiume kaona ndie anakufaa! ni jambo la kushukuru sana je hao wasio na watoto wasemeje kama ss tunachagua na jinsia tutakayo?
   
Loading...