Mtoto wa kiume kusherekea siku ya kuzaliwa ni kosa?

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,623
5,037
Habari wana JF.

Je kusherekea siku ya kuzaliwa ni kosa?

Nakumbuka nikiwa na umri wa miaka 9 niliwahi kumwambia mshua(Father) kuhusu kusherekea siku ya kuzaliwa nilichokumbana nacho sitokisahau maisha yangu.

Kwanza nilikupokea kipigo cha hatari sana na kunyimwa msosi siku hiyo akiniambia kufanya visherehe sherehe vya kipumbavu ni mambo ya kike/wanawake na siyo vizuri mtoto wa kiume/ mwanaume kufanya sherehe ya kuzaliwa na zinginezo.

Nikiwa naendelea kupata kipigo aliendelea kuniambia haya "mwanaume inabidi unakuwa na fikira kama mwanaume mfano utapataje hela ununue kiwanja ujenge au uwe tajiri mkubwa wewe unaanza kuleta upumbavu"

Hivyo basi, alinifundisha tabia ambayo nikimuona mwanaume anasherekea siku ya kuzaliwa huwa namfikiria kivingine kabisa na kumchukulia kama hajakamilika kama mwanaume.

Je ni nipo sahihi wadau au kuna sehemu nakosea?
 
Huo ulikuwa mtizamo wake yeye, ambao aliamua wewe kama mwanaye ufate anayopenda.

Na labda ulitaka hayo wakati haukujua yeye alikuwa na mipango gani anayofikiria kimaisha, na aliamua kuyapa kipaumbele aliyokutajia sababu hayakumjia kiurahisi. au?

Hivyo sio vibaya kabisa kusherekea siku ya kuzaliwa, kwa binadamu yoyote anapoamua.
 
Kusherekea sio kosa ila watu wana mtazamo tofauti kuhusu hii swala. Kumfanyia mtoto mdogo naona ni sawa

Mimi mwenyewe huwa sifanyi sherehe za birthday mara nyingi ila naitambua kama siku yangu ya kuzaliwa na ni ya tofauti, marafiki hunitumia salamu na nashukuru ila sibadilishi ratiba yangu kwa ajili ya birthday
Hata baadhi ya sikukuu hunipita kama nina mambo mengi ya kufanya

Ila nikiwa katika mood nzuri na mambo yangu yameenda vizuri hapo nafanya party ya kidogo na kuita marafiki
 
Haya mambo ya kufanya sherehe siku ya kuzaliwa naona tumeiga kutoka kwa Wazungu. Kwangu mimi sioni umuhimu wake na hakuna tija yoyote. Huwa sifanyi. Na hata ukinialika nije kwenye sherehe ya eti siku ya kuzaliwa, siji kabisa. Huko ni kupoteza muda na fedha ambazo zingetumika kwenye mambo mengine ya msingi.
 
Kusherekea siku ya kuzaliwa ni mtazamo wa mtu husika,binafsi nina mtizamo kama wa baba yako maana sioni kwanini niifanye sherehe ingawa ata siku ( tarehe) mara nyingi ukumbushwa na msg kutoka kwa marafiki au jamaa zangu.
 
Kusherekea sio kosa ila watu wana mtazamo tofauti kuhusu hii swala. Kumfanyia mtoto mdogo naona ni sawa

Mimi mwenyewe huwa sifanyi sherehe za birthday mara nyingi ila naitambua kama siku yangu ya kuzaliwa na ni ya tofauti, marafiki hunitumia salamu na nashukuru ila sibadilishi ratiba yangu kwa ajili ya birthday
Hata baadhi ya sikukuu hunipita kama nina mambo mengi ya kufanya

Ila nikiwa katika mood nzuri na mambo yangu yameenda vizuri hapo nafanya party ya kidogo na kuita marafiki
Thanks
 
Haya mambo ya kufanya sherehe siku ya kuzaliwa naona tumeiga kutoka kwa Wazungu. Kwangu mimi sioni umuhimu wake na hakuna tija yoyote. Huwa sifanyi. Na hata ukinialika nije kwenye sherehe ya eti siku ya kuzaliwa, siji kabisa. Huko ni kupoteza muda na fedha ambazo zingetumika kwenye mambo mengine ya msingi.
Hakika Mkuu.

Nakumbuka hata nikiwa chuo tuliachana na msichana mmoja hivi kwa sababu yeye alipenda hizo mambo wakati kwangu mimi ilikuwa ni sawa na paka na panya.
 
Back
Top Bottom