Mtoto wa kike anaanzia umri gani kutobolewa masikio?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Nimekuwa nikiona watoto wakike wakiwa wametoboa masikio kwa ajili ya urembo, swali ninalouliza ni Je, ni umri gani unafaa kuanza kumtoboa mtoto masikio?

Na je kuna umuhimu wowote ule wa kufanya hivyo (kumtoboa mtoto masikio)?
Vipi kama akiachwa mpaka akue ndiyo ajitoboe mwenyewe, kuna madhara yoyote yale kwa Msichana?
 
Umri wowote unaotaka wewe hata siku hiyo hiyo aliyozaliwa japo kuna ka maumivu Fulani wakati wa kutoboa. Nakushauri usimtoboe mpaka awe mkubwa aamue mwenyewe.
 
asipopenda kuwa mlimbwende? mwache afanye uamuzi kumhusu atakapokuwa tayari kufanya hivyo
 
Sisi kwetu tunatobolewa mwezi mmoja baada ya kuzaliwa.... Imekua kama tradition
 
Sawa tu na tohara,wewe unaona ni wakati gani ni muafaka wa kuondoa ile kitu kwa mwanao wa kiume akishazaliwa?
 
Bora umtoboe akiwa mdogo..... Rafiki zangu wengi ambao hawakutoboa walitamani wangekua wametobolewa tangu zamani
 
Huwa naona watoto wadogo tayari wameshatobolewa naona kama hakuna umri maalumu
 
Nimekuwa nikiona watoto wakike wakiwa wametoboa masikio kwa ajili ya urembo, swali ninalouliza ni Je, ni umri gani unafaa kuanza kumtoboa mtoto masikio?
Na je kuna umuhimu wowote ule wa kufanya hivyo (kumtoboa mtoto masikio)?
Vipi kama akiachwa mpaka akue ndiyo ajitoboe mwenyewe, kuna madhara yoyote yale kwa Msichana?
Mkuu, leo hukwenda LUMUMBA nini? Naona umekuja na mada ya kifamilia zaidi. Hongera kwa kulea ka binti.
 
umri wowote unaotaka wewe hata siku hiyo hiyo aliyozaliwa japo kuna ka maumivu Fulani wakati wa kutoboa.nakushauri usimtoboe mpaka awe mkubwa aamue mwenyewe
Naunga mkono hoja hapo mwishoni.
 
Usithubutu kutoboa masikio - unatengeneza malango ya mazimwi-mambo ya ritual hayo unknowingly
 
Hivi vitu kwa zamani vilitokana na tamaduni za makabila, makabila kama ya Kimasai waliwatoboa watoto wa kike wakiwa wadogo. Dhima ya utoboaji kwa wanawake ni kuongeza nakshi ya urembo, ila kikawaida utoboaji kwa mtoto wa kike unafaa zaidi akiwa bado mdogo hasa kuanzia mwezi mmoja ama miwili na kuendelea.
 
Back
Top Bottom