Elections 2015 Mtoto wa Celine Kombani amrithi mama yake jimbo la Ulanga

Kwani ni urithi hivi vyeo kumbe. Mgimwa, wa Arumeru na sasa Ulanga, ndo maana wana ng'ang'ania ushindi kwa gharama zote
 
wanaulanga msikubali hilo sio jimbo la kifalme. Ina maana ulanga yote haina msomi au mtu yeyote aliyemaliza form 4 au anayejua kusoma na kuandika?

Msikubali, msikubali hii ni fedheha. Haiwezekani hata angekuwa ukawa, hamna kukubali bora mkose mwakilishi sio ubunge wa kifalme.

wewe lofa kweli kweli. Ata mwalimu wako alipata shida sana maana inaonekana wewe nunda. Wanamjua kazi yake. Waache jembe kisa mama yake alikuwa mbunge? Hata marekani hawafanyi hivyo, ndio maana nimesema wewe ni lofa na unafikiria kutumia masaburii.
 
Hilo ni jiwe la kwenye Giza ..

That is an open secret ... Huko Kwao na Ndugu za marehemu ndio walalalamika chini chini ...waambieni waache kulalamika

Bahati nzuri nakufahamu wewe ni mtu wa namna gani najua umepitiwa tu utakapo pata muda wa kutafakari utajua nilichokuwa naamanisha.
 
tatizo sio kugombea hebu tuambie alishiriki kura za maoni? na kama alishiriki alishika nafasi ya ngapi? ukinijibu tutaenda sawa ukishindwa utakua mmoja wao unaesubiri baba afe chama kikupe fadhila


~NA LATIFA GANZEL, MOROGOROHATIMAYE mtoto wa marehemu Celina Kombani, Goodluck Milinga, ameibuka na ushindi katika kura za maoni za kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Ulanga Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Milinga, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Celina (aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma), aliibuka na ushindi huo jana, katika uchaguzi wa kura za maoni wa CCM uliofanyika katika jimbo hilo. Nafasi hiyo ilikuwa ikiwaniwa na watu wanane.
Akitangaza matokea hayo, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Hamza Mfaume alisema Milinga aliibuka kidedea kwa kupata kura 731, akifutiwa na Azizi Jawadi aliyepata kura 134.
Wengine na kura zao katika mabano ni Thabit Dokodoko (52), Agustino Matefu (41), Wencheslous Ikumla (39), Pontian Kipao (11), Herrieth Mwakifulefule (tisa) na Daud Kitolelo (nane).
Mfaume alisema katika uchaguzi huo, kura zilizopigwa zilikuwa 1,029, ambapo nne ziliharibika, hivyo halali zilikuwa 1,025.
Kwa upande wake, Milinga aliwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumpa kura nyingi na kuwaahidi atatekeleza yote ambayo aliahidi na hata yale aliyoahidi marehemu mama yake enzi za uhai wake.
Alisema akipata ridhaa ya kuongoza jimbo hilo, atahakikisha anaboresha huduma za afya, barabara, mawasiliano ya simu, elimu na makazi hususan nyumba za walimu.
“Wananchi wa Ulanga wamenipa ridhaa hii kwa sababu muda wa kampeni zote za kura za maoni wakati mama akigombea, waliniona nafanya mimi, nawajua watu kwa sura na majina na wao wananijua hata utendaji wangu wa kazi,” alisema
Alisema atahakikisha analitendea haki jimbo hilo kwa kufanyakazi kwa kasi kubwa zaidi kwa kuzingatia yeye ni kijana na anamudu kasi hiyo.
Celina alifariki dunia Septemba 24, mwaka huu, nchini India, alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya kongosho. Alikuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Ulanga Mashariki.
Aliongoza jimbo la Ulanga kwa vipindi viwili mfululizo tangu mwaka 2005 hadi 2015. Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Morogoro mjini.
 
Mtoto wa aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Ulanga marehemu Celine Kombani ameshinda kura ya maoni ndani ya chama chake CCM hivyo kumrithi mama yake kugombea ubunge kupitia chama chake CCM.

===============================



Chanzo: Mtembezi

Kwani alie kua wapili katika kura zamaoni yupo wapi? Yeye ndo angefaa kurithi mikoba jamani. Ccm bwana kwakupeana ulaji ni kiboko.
Watu hawakumchagua yeye, na najua alijuwepo shindi wa pili.
 
Huyu kijana nadhani ni mbunge kilaz.a kuliko wote ndani.Hona hoja kabisa.Tangu bunge lianze yeye ni kuropoka tu.Kupitia kwake nimeridhika kwamba Tanzania hatuna bunge,tuna watu wanaokaa pamoja kupiga meza kupitisha hoja za serikali.Godlucky alipendekezwa na CCM kugombea ubunge baada ya mama yake kufariki dunia.Na kwa kuwa watanzania bado tumeelemewa na ujinga bado wapiga kura hawakuona wagombea wengine matokeo yake ni haya..Inakera sana
 
Wa kuwalaumu ni wapiga kura.Ni dhahiri wapiga kura wengi wa Ulanga wana upeo mdogo.
 
Upo sahihi,Ila wapiga kura wake wameshajua kua walipotea,2020 lazima wamchinjie baharini..
 
Cv yake mie nimeingalia hata siielewi. Design hapo kati kwa miaka kadhaa alikuwa amesimama bila maendeleo ya shule wala kazi. Huenda ndio alikuwa anakariri mistari ya bongo flavor anayoiabudu kuliko mashujaa wetu
 
Back
Top Bottom