Elections 2015 Mtoto wa Celine Kombani amrithi mama yake jimbo la Ulanga

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Mtoto wa aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Ulanga marehemu Celine Kombani ameshinda kura ya maoni ndani ya chama chake CCM hivyo kumrithi mama yake kugombea ubunge kupitia chama chake CCM.

===============================

MOROGORO

HATIMAYE mtoto wa marehemu Selina Kombani ndiye ameibuka mshindi katika kura za maoni za kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Ulanga Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

ambaye ni mtoto wa Kombani wa kwanza aliibuka katika uchaguzi wa kura za Maoni wa CCM uliofanyika jana katika jimbo hilo , nafasi ambayo iligombewa na watu 8.

Akitangaza matokea hayo msiamamizi wa uchaguzi huo, Hamza Mfaume amesema Gooluck aliibuka kidedea kwa kupata kura 731, akifutiwa na Azizi Jawadi aliyepata kura 134, Thabit Dokodoko kura 52, Agustino Matefu kura 41, Wencheslous Ikumla kura 39, Pontian Kipao kura 11, Herrieth Mwakifulefule 9 na Daud Kitolelo 8.

Mfaume amesema katika uchaguzi huo jumla ya kura zilikuwa 1029 , ambapo kura zilizoharibika zilikuwa 4 ambapo kura halali zilikuwa 1025.

Goodluck amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumpa kura nyingi, na kuwaahidi atatekeleza yote ambayo ameahidi na hata yale aliyoahidi marehemu mama yake enzi za uhai wake.

Amesema akipata ridhaa ya kuongoza jimbo hilo atahakikisha anaboresha huduma za Afya, barabara ,mawasiliano simu, elimu na makazi hususani nyumba za walimu.

'' Wananchi wa Ulanga wamenipa ridhaa hii kwa sababu muda kampeni zote za kura za maoni wakati mama akigombea nilikuwa nafanya mimi, nawajua watu kwa sura na majina, na wao wananijua hata utendaji wangu wa kazi''

Amesema atahakikisha analitendea haki jimbo hilo kwa kufanya kazi kwa kasi kubwa zaidi kwa kuzingatia yeye ni kijana na anamudu kasi hiyo.

Marehemu Celina Kombani,alifariki mnamo Tarehe 24/09,nchini India ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Kongosho,alikuwa mgombea Ubunge katika Jimbo la Ulanga Mashariki.

Kombani aliongoza jimbo la Ulanga kwa vipindi viwili mfululizo tangu mwaka 2005 hadi 2015, sambamba na hilo aliwahi kuwa mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania UWT wilaya ya Morogoro mjini kabla ya kushika wadhifa wa ubunge.

Chanzo: Mtembezi
 
Wanaulanga msikubali hilo sio Jimbo la kifalme. Ina maana Ulanga yote haina msomi au mtu yeyote aliyemaliza form 4 au anayejua kusoma na kuandika?

Msikubali, msikubali hii ni fedheha. Haiwezekani hata angekuwa Ukawa, hamna kukubali bora mkose mwakilishi sio ubunge wa kifalme.
 
Haya ndiyo mambo ambayo watanzania wameyachoka na ndiyo maana wanataka mabadiliko, inaonekana kipondo alichowapa mh. Nasari kule arumeru bado hakijawatosha
 
Wanaulanga msikubali hilo sio Jimbo la kifalme. Ina maana Ulanga yote haina msomi au mtu yeyote aliyemaliza form 4 au anayejua kusoma na kuandika?

Msikubali, msikubali hii ni fedheha. Haiwezekani hata angekuwa Ukawa, hamna kukubali bora mkose mwakilishi sio ubunge wa kifalme.
Huyo dogo mwenyewe alishadisko mzumbe, akasepa zake mara naskia yupo nhif
 
Hahah Goodluck! Alikua NHIF na ameoa juzi juzi tu..nilidhani Joe ndiye angerithi, anyways mungu amtangulie!

Joe brazamen Sana ubunge asingeweza acha akomae kiakili kwanza
Akishaacha kushika vikopo Java lounge na kuvaa supra ndio walau atafikiriwa
 
Joe brazamen Sana ubunge asingeweza acha akomae kiakili kwanza
Akishaacha kushika vikopo Java lounge na kuvaa supra ndio walau atafikiriwa

Hahha but hes a nice chap! Saa we jamaa ukiniona si utaniita brother man kumbe kazi nayo fanya ni kuchimba mkaa! Nawaonea huruma mno hasa joe, mtoto wa mama sana dah Rip Celine
 
Siasa za Tz zinakwenda na Sir name hata kwenye soka au muziki (jokes but wakati mwingine inatokea mtu analamba dumbe kwa jina la mtu maarufu)
 
Hahha but hes a nice chap! Saa we jamaa ukiniona si utaniita brother man kumbe kazi nayo fanya ni kuchimba mkaa! Nawaonea huruma mno hasa joe, mtoto wa mama sana dah Rip Celine

Hahaha I know he's such a nice guy lakini kwa ubunge hapana aisee bado Sana ,Mkuu na wewe unavaa supra japo ni mkata mkaa ??
Mie mwenyewe naogesha mbwa ila walau navaa travolta
 
Hahaha I know he's such a nice guy lakini kwa ubunge hapana aisee bado Sana ,Mkuu na wewe unavaa supra japo ni mkata mkaa ??
Mie mwenyewe naogesha mbwa ila walau navaa travolta

Hahah mbwa na travolta? haya nimejiongeza kama ulivyo nisihi uncle kwenye uzi wa "London"
 
Mambo kama haya ni mojawapo ya vitu ambavyo tunatakiwa kuvifanyia mabadiliko. Maana itafikia wakati hii Nchi inaweza kugeuka kuwa ya kifalme kwa kurithishana uongozi serikalini tu. Baba akistaafu anamuweka mtoto wake, mpwa wake, mkewe, mjukuu wake, nk. Sasa si upuuzi huu. Na ndio maana uchumi wa Nchi upo mikononi mwa wachache kutokana na mambo kama haya.
 
Back
Top Bottom