Mtoto wa ajabu azaliwa baada ya jaribio la kutoa mimba kushindikana

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Kuna mdada anadaiwa kujaribu kutoa mimba kwa kunywa vidonge vya kutolea mimba....ikagoma ..akaamua kuilea hivyo hivyo leo kazaa mtoto ambaye kawa affected na hizo dawa, Picha nimetumiwa na ndugu yangu ambaye ni nesi yuko hapa Dar".

Mwenye taarifa zaidi juu ya tukio hili tunaomba atusaidie.


Mtoto amezaliwa Machame Moshi, Mama yake ana (16) alikunywa dawa ya kienyeji ili atoe mimba akiwa na miezi minne, aliyempa dawa ni Dada yake (Dawa alipewa na mganga wakienyeji lakini mimba haikutoka bali aliendelea na ukuaji kama kawaida hadi leo).

=======================

UPDATES;

JamiiForums: Picha Imeondolewa kwani haifai.
 
daaahhh...sijui kama ataweza kuishi huyo mtoto,huruma sana aisee
 
We ndo mleta mada kisha unadai mwenye taarifa zaidi atuletee. Basi wataje majina waje na hizo taarifa, au la tuwekee picha ya hicho kiumbe ili uthibitisho upatikane wa habari uliyoleta.
 
tatizo ni kwamba mna tabia za kuamsha hisia za watu basi tu. Mara kwa hisani ya jf picha imeondolewa haifai, haifai kwa nani?? Mbona aliyeipiga hakuzimia tuzimie sisi wa kuona?? Kwa hisan ya walengwa rudisheni hiyo picha msime, ukiiangalia ni uamuzi wako mwanyewe kwani ni mbaya. Mtu aamue mwenyewe kuangalia, ili iwaogopeshe wadada wanaofikiria hata dakika hii kwenda kutoa mimba
 
Na iwe fundisho mnateleza pekupeku halafu mnataka kukimbia majukumu
 
We ndo mleta mada kisha unadai mwenye taarifa zaidi atuletee. Basi wataje majina waje na hizo taarifa, au la tuwekee picha ya hicho kiumbe ili uthibitisho upatikane wa habari uliyoleta.

mkuu Makene picha ipo
 
Last edited by a moderator:
Siyo kweli...huu ni ugonjwa wa ngozi tu,ni Genetic disorder,Unaitwa kitaalamu "harlequin ichthyosis"
Uki-google unaweza ona picha zake
 
hivi nyie moderators Wa jf wakati mwingine mnakuwa kama mnavuta bhange.. hiyo picha hata kama ingekuwa Mbaya kiasi gani mnaitoa ya kazi gani? hao wenye hizo tabia watajifunzaje? always naamini watu wanajifunza kupitia makosa ya wengine.. sasa Kwa style hii mnatoa mafunzo gani kwa jamii? rudisheni hiyo picha bhana..
 
Back
Top Bottom