ahaaaaa.. ila jamani majanga loh! ishakula kwake hivokubali yaishe kwani yanini kugombea ng'ombe asokuwa wako hata kama alifungwa kwenye zizi lako??
huku kote ni ku-kompliketi maisha,Dah! jibu la moja kwa moja sitakupa mzee, lakini mwambie mkapime DNA ili uondoe wasiwasi wako.
View attachment 115258
ahaaaaa.. ila jamani majanga loh! ishakula kwake hivo
ila inauma ujue ! huyu mama nimemkubalisasa unafikir atafanyeje kama hali ndo ishakuwa hivyo??
mimi nakwambia achen wanawake wapewe matiti vifuani, tena acha wanaume wayachezee tu lkn wasitake kuyafunua kuona kilichoo ndani watakufa.
roho ya mwanamke ikisha gilibiwa ni zaid ya biological weapon ama virus vya botulism
kwa huyu mwanaume aachane sijui nakupima DNA ajikalie pemben ampishe mwenye nguvu apite.
kwann bwana kujifanya mjinga ulinde utu wako?
ila inauma ujue ! huyu mama nimemkubali
Kama alivyosema gfsonwin wanawake wacha wabaki kuwa wanawake. Wakiamua kubadilika utajuta kumfahamu. Na Ukweli ni kwamba anaejua mtoto ni wa nani na mama maana yeye ndo anajua alipata huo ujazito lini na ni nani alihusika. hivyo akishasema mtoto sio wako huenda ikawa kweli kabisa hivyo ni bora kumuachia kwani mtoto kama ni wako ni wako tuu. kumbuka damu haipotei
hayajawahi kunikuta, lakini ninahisi vyte ni sawa tu. ninaamini mtu akisingiziwa mtoto akamtunza siku akija kuambiwa sio wake atapata fedheha na moyo utaumia kiasi kwamba ataona bora huyo mtoto asingekuwepo.ni kama mwanamke kuwa na boyfriend wakategemea kuoana, amekuja kujitambulisha kwenu halafu wiki moja tu baada ya kujitambulisha unasikia taarifa za harusi kuwa yule mwanaume anafunga ndoa na mwanamke mwingine....ile aibu alivyokuja kujitambulisha, utaeleza nini kwa watu? aibu tupu. na kwa mtoto hivyohivyo, pengine ulishajulikana wewe ndio baba yao, siku watu wanajua hukuwa baba yao...ni fedheha sana.Hivi ulishawah kuwaza hivi kipi kinauma mtoto azaliwe afe ama mtoto azaliwe halafu uambaiwe wewe sio baba yake?
Hata mama anaweza asijue baba ni nani.
Hebu fikiria, mwanamke kat.ombwa na wanaume watatu katika span tuseme ya wiki moja. Na katika hiyo wiki ndo alipopata ujauzito.
Sasa nambie, yeye kama mama atajua ni nani kati ya hao watatu waliom.----- ndo baba?
Hawezi! Hivyo mkata mzizi wa fitna na genetic test tu.
hayajawahi kunikuta, lakini ninahisi vyte ni sawa tu. ninaamini mtu akisingiziwa mtoto akamtunza siku akija kuambiwa sio wake atapata fedheha na moyo utaumia kiasi kwamba ataona bora huyo mtoto asingekuwepo.ni kama mwanamke kuwa na boyfriend wakategemea kuoana, amekuja kujitambulisha kwenu halafu wiki moja tu baada ya kujitambulisha unasikia taarifa za harusi kuwa yule mwanaume anafunga ndoa na mwanamke mwingine....ile aibu alivyokuja kujitambulisha, utaeleza nini kwa watu? aibu tupu. na kwa mtoto hivyohivyo, pengine ulishajulikana wewe ndio baba yao, siku watu wanajua hukuwa baba yao...ni fedheha sana.
kwani logic ya kufanya genetic test ni ipi??
na je wafikir itabadili matokeo??
to me wala hakuna haja ya kufanya, huyu aloanzisha balaa lake aondoke nae najua mtoto kama ni damu yangu hatapotea atarudi tu.
Kuna wanawake wengine ni watesaji tu, sasa inamuhitaj mwanaume ambaye ana maamuzi magumu kumudu mwanamke kama huyu.
Hakuna fedheha kutunza mtt ukaja siku ukaambiwa sio wako. manake hapo mwenye makosa sio wewe uliyelea. Kuna baadhi ya wanawake ili kuish nao unahitaj kuwa na roho ngumu tu
kudanganywa sipendi kabisa,,,,,,,,,Kinachouma na kutia fedheha ni kule kudanganywa. Tena kudanganywa kwa muda mrefu. Wewe unapenda kudanganywa?
Hakuna mtu anayependa kudanganywa hususan kwenye mambo kama hayo ya watoto. Mtoto ni mtoto tu na kulea kwa hiari huku ukiujua ukweli, hiyo kwa wengi huwa haina shida.
mi naona kama ni ufala wa mwanaume! usibishane na sixth sense!Mama akikuthibitishia kuwa mtoto si wako na anapofikisha miaka.10 anambadilisha na jina ufanyeje? Ikizingatiwa siku zote ulikuwa na wasiwasi?
kudanganywa sipendi kabisa,,,,,,,,,
lakini linapotokea swala kama hili nngeomba poo kwanza kisha nianze kuushirikisha ubongo wangu vyema.
ngoja nikue mfano mdogo, baba mmoja aliwah kulea mtoto asokuwa wake kwa muda mrefu, lkn huyu mama alipatia mimba ndani ya ndoa, so kichaga wakasema mtoto anayezaliwa ndani ya ndoa either katoka kwa mwanaume mwingine ama la unatakiwa umlee.
Huyu baba hakuwa anajua lolote juu ya mtoto na hata hivyo hakukuwa na significant difference kati ya watot alozaa kwa huyu baba na huyu wa nje.
Ikatokea siku huy baba akawa anaumwa kalazwa eurology unit kcmc, ilipofika siku ya upasuaji wakasema anahita damu so mwanae alokuwepo karibu ndie huyu ikabidi aambiwe aka donate damu kwa baba. maskini yarabi wee mtoto kupimwa damu yake na ya baba ni tofauti kabisa wakashangaa mbna kwa group alonayo mama na group alonayo mgonjwa haiwez kuwa na mtoto wa damu group tofauti?? Dr mmoja ndugu wa mgonjwa ndiye aliyegundua. Si akavujisha siri bhana, huwez kuamini huyu baba mgonjwa aliliskia kabla hata hajaruhusiwa pale hosp. Huyu mzee akiwa wodini yule mtoto alikuja kumkalizia alipomwona tu alimwambia mwambie mama yako akuonyeshe baba yako, na labda nisirudi nyumban ila nikirudi nyumban sitak kukukuta na wala usije hosp kuniona tena.
huwez kuamini kweli huyu baba wala hata huko nyumban hakurud alikufa akiwa na kinyongo sasa kweli unafikir alitumia busara?