MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,607
Mama mmoja alikuwa na mtoto mmoja wa kiume mtundu ajabu. Mama akaamua ampeleke kwa mchungaji kufunzwa dini na maadili.
Wakiwa kanisani, mchungaji badala ya kumpa mawaidha juu ya uwepo wa Mungu, akamwuliza mtoto moja kwa moja.
Nimeambiwa na mama yako kuwa wewe umtundu sana, "Unamjua Mungu wewe?" Mtoto hakujibu. Mchungaji akaendelea kuuliza, "Niambie, Mungu yuko wapi? Mtoto hakujibu
Baada ya kuuliza swali lile lile mara kadhaa bila jibu, mchungaji akahamaki na kumwuliza kwa hasira na sauti kubwa.
"Sema. Mungu yuko wapi?"
Masikini yule mtoto akaogopa na kukimbilia nyumbani mbio. Mama kuona vile akamwuliza,"Kwa nini umerejea toka kanisani?"
Mtoto akajibu huku analia, "Mungu amepotea mchungaji anahisi nimemuiba mimi".