Tatizo pingili katika uti wa mgongo inaonekana umepinda tatizo limekuja gundulika mwaka jana bint akiwa ameshakua mkubwa, hivyo alitakiwa kufanyiwa operation, na matibabu anahudhuria Muhimbili. Sasa kwakua yupo form four wakashauriwa kuna dawa atumie then baada ya kumaliza paper arudi kwa ajili ya operation (japo operation wanasema itahitaji umakini mkubwa kwa sababu mtoto anaweza aka paralize ama akasafiri, ni 50/50). Imekua ni mtihani kwa familia maana kila akirudi shule siku kadhaa tu hali ile inamtokea, kupoteza fahamu kabisa.