Donyongijape
JF-Expert Member
- May 28, 2010
- 1,497
- 815
Habari ya kwenu wanaJF.
Kwa kweli nimepatwa na majonzi makubwa leo baada ya kupata taarifa kutoka kwa daktari kuwa taarifa ya ultra-sound inaonyesha mwanangu niliyekuwa nikimtegemea kuwa firstborn amefariki tumboni mwa mama yake. Mpaka sasa bado kiumbe hakijatolewa. Naomba maombi yenu kitoke salama.
Wana JF, nimekuwa msomaji wa baadhi ya post za kitabibu humu na mara nyingi zimekuwa msaada kwangu. Naamini mara hii pia nitapata msaada.
Nawaombeni mnisaidie niweze kujua nini hasa husababisha tatizo hili?.je ni lishe, mikao, mlalo au nini hasa?. Pia kichanga kinaweza kufia tumboni kuanzia wakati gani?. I mean miezi mingapi?.Maana wa kwangu amefariki akiwa ametimiza miezi 9 na EDD ilikuwa ni kesho tarehe 19.
Naomba mnisaidie na mengineyo katika suala hili ili huko mbeleni lisije kujirudia kwangu (hata pia kwa faida ya wengine watakaofuatia thread hii).
Wasalaam!
UPDATE:

Niwashukuru sana ndg. Mwalu , kiwaki , Isaac Chikoma , gody , measkron ,ZeMarcopolo , md4doctor2000, grand-mal , hippocratessocrates , charminglady, Cathode Rays, Smile, Mwasi,King Kong III , Masuke , Kamanda Moshi , prax , Dina , Akili Unazo na wengineo kwa pole zenu, Maombi yenu, Darasa/shule mliyonipa, Ushauri wenu pamoja uchokonozi wa baadhi yenu ambao umenifanya nipate maarifa zaidi kutoka kwa madaktari wa JF.
Jana, mke wangu aliweza kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya kuwekewa vidonge na baadaye maji ya Uchungu. Kichanga kilikuwa ni cha kiume. Tunamshukuru Mungu kwa mama kuweza kujifungua salama bila kuchanika.
WanaJF Doctor, Madaktari wote TZ na wenzangu wengine, kwa kweli baada ya kupata tatizo hili kumenifanya niwe so much curious. Kwa hospitali hii niliyokuwepo ambayo ipo hapa hapa Dar Es Salaam, tena kubwa tu, wikiend hii pekee kulikuwa na akina mama wanne ambao vichanga vyao vimefia tumboni. Last two weeks kulikuwa na cases kama hizo sita. Kwa hiyo kwa mwezi wa tano tu ni vichanga atleast 10 vimefariki tumboni kwa mama zao kwa hospitali hii. Hapo hujaongelea Hospitali ya Mwananyamala, Amana, Temeke, Muhimbili na privates nyingine hapa DSM. Potelea mbali hospitali nyingine huko mikoani, wilayani, kwenye kata, na hata majumbani.
KIMSINGI, nimeona kuwa tatizo hili ni kubwa sana sana. Na nina ukakika kwa nchi zilizoendelea jambo kama hili kwa ukubwa huu lazima wangekuwa wamepata utatuzi wake mapema.
Mimi natoa RAI kwa Madaktari, Wanafunzi wa Udaktari, Wizara na Asasi za Afya kufanya utafiti wa kina kujua Magnitude ya Hili tatizo na nini zinaweza kuwa sababu za msingi kutokea kwa MAZINGIRA YETU. Labda nipo outdated, lakini naona kuwa ni mhimu sana kuwa na majibu sahihi juu ya hili katika MAZINGIRA YA NCHI YETU, la sivyo vijana wataendelea kuteketea kabla hata hawajazaliwa.
Niwashukuru tena kwa kujitoa kwenu na kunipa majibu na ushauri mzuri katika mada hii.
Asanteni.