Mtoto Kufia Tumboni: Sababu ni zipi?

Mtoto Kufia Tumboni: Sababu ni zipi?

Kwetu abortion ni kufa au kuharibika kwa kiumbe kabla ya wiki ya 28 ya ujauzito kwa sababu kwa mazingira yetu hatuwezi kutunza watoto wali chini ya umri huo wakakua hata kama watazaliwa hai.

Mkuu, kuongezea..hivi sasa Tanzania wameweza kumudu watoto walio na chini ya wiki 28 ya umri wa mimba na wakaishi, Muhimbili(wiki 27), na wawili wa wiki 26 pale Bugando.
 
Donyongijape,

Pole, majibu mengi yamekwishatolewa, nami ningeongezea,

Mtoto kufia tumboni, husababishwa na sababu nyingi, zikiwamo matatizo ya damu, hasa kundi!, magonjwa(mengi yakiwa ni ya zinaa), magonjwa mengine ambukizi (mfano Malaria), Ajali, Magonjwa ya 'mtindo wa maisha'..mf. Kisukari, moyo, Shida katika viungo vya uzazi na mfuko wake (mf. kuachia/kulegea kwa kondo la nyuma)...ingawaje kwetu huku sijakutana na utafiti wa namna hiyo lakini wamekuwepo baadhi ya wagonjwa ambao kujitokeza mara moja kwa tatizo hili (kumeendelea kujirudia).n k.

Mara nyingi tunaposea mtoto amefia tumboni, tunaongelea muda wa mtoto ambaye KAMA angezaliwa angeishi! Hivyo basi uhusiano unakuwepo kati ya mtoto mfu(IUFD) na mimba kutoka(Abortion).

Kujikinga:

Hapa Tanzania (sawa sawa) na nchi nyingine duniani, tunakuwa na kliniki ya wajawazito, tofauti ni kwamba, wanawake wengi (wajawazito) wamekuwa wakipuuzia/kutojali kliniki hizi.Mojawapo ya faida ya kliniki ni kugundua maendeleo ya mtoto, mama mtarajiwa, mipango ya kujifungua (ajifungue kwa njia gani, wapi, lini, ajiandaeje?n.k).Pili wajawazito wenye matatizo mbali mbali ya kiafya (huweza kuangaliwa kwa ukaribu zaidi(kuwasisitizia dawa, kuwaanzishia wale wenye uhitaji).

Hivyo, njia bora ni ya kutambua mwenendo wa kliniki, mhudumu wa afya agunduapo tatizo kwa viashiria vyake, huweza kusaidia.

Uwapo nyumbani, mjamzito anaweza kusikia mtoto 'kucheza', hii ni kishiria kisichohitaji kupima, lakini mtoto awapo mfu(siku mbili) za kwanza huendelea kusikia bado akijigeuza na hivyo, umakini unahitajika wakati mtu agunduapo kucheza kwa mtoto kumepungua.

Maelezo mengine mengi mazuri yametolewa na madaktari na wadau wengine hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
Wengi wamekujibu kisomi kuönyesha utade wao,ngoja mie nikujibu kikawaida,sababu zinazosabisha kufa kwa kiumbe b4 EDD.
1.Pressure(HBP)
2.JOTO TUMBONI.
 
Next time wife akishka ujauzito inabidi aende clinic mara kwa mara,kuzuia pressure kuna dawa inabid awe anakunywa ambazo kina ZeMarcopolo na Riwa wanazijua na kuzuia joto tumboni kuna dawa za kienyeji za kunywa kama maji hv kuna mama yupo kinondoni karibu na american chips anauza
 
Mkuu King kong III,

itabidi nikutafute unipeleke kwa mama wa kinondoni akanipe taaluma.
 
pole sana,mimi mwenyewe yalinikuta mwezi january this year,i felt so terrible yani,waliniwekea vidonge fulani (sijavijua jina) down there kila baada ya masaa mawili hadi nilipojifungua kawaida!mimi mtoto alijinyonga na kitovu,na alifariki siku tano before!pole sana I know what are you going through.
 
Pole sana mkuu.

Sisi wengine tunatafuta elimu tu, hatuna a wala be ya udaktari.

Ila kitu kimoja kimenisukuma kuwauliza madaktari ZeMarcopolo, Riwa, HIPPO. Kuna ushauri gani mkiwakuta wazazi wanatofauti kwenye rhesus factors? Manake ndio washakuwa pamoja tena, kuna utaalam wa kuwawezesha kupata mtoto, hasa kwa nyumbani TZ?
 
Kutofautiana Rh sio tatizo kwa mume na mke na pia sio tatizo kubwa kwa mtoto wa kwanza.

Tatizo linaweza kutokea kwa mtoto wa pili na kuendelea.

Kwa vile siku hizi akina mama wengi wanahudhuria clinic ya wajawazito huweza kutambulika mapema makundi yao ya damu na hatua stahiki kuchukuliwa.

Kuna aina mbalimbali ya ushauri wa jinsi ya kuwasaidia mama wa Rh negative. Njia inayopewa nguvu zaidi ni utaratibu wa kuwachoma mama hawa sindano ya anti D antibodies week ya 28 ya ujauzito. Iwapo mjamzito atafanyiwa procedure yoyote kuanzia second trimester pia anapewa antibodies.

Mtoto akizaliwa anapimwa kundi lake la damu. Iwapo atakuwa Rh pozitive basi mama anapewa tena antibodies. Zipo sehemu ambazo wameamua hawampi tena mama baada ya kujifungua iwapo walishampa awali antibodies. Dozi hii ya baada ya kujifungua inatolewa kabla hayajaisha masaa 72 baada ya kujifungua. Baada ya hapo inakuwa "too late"...
 
Mkuu naona wengi wameshakupa majibu hapo juu!naloweza kuongezea ni je wawezaje kupunguza chance ya kutokutokea?
1. Ultrasound unapohis/kujua ni mjamzito,hii itasaidia kujua kama cervix imefunga,mimba imekaa wapi na kwa msomaji mzuri wa ultrasound like DR. Bashiru (RPI) angekuambia hata level ya fluid (amniotic fluid)itakuwaje huko mbeleni
2.Kuchek vipimo vya damu RH -VE au +VE, magonjwa kama kisukar wakat wa ujauzito nk!
3. Ultrasound kila baada ya miezi 2 ni muhimu sana maana hii itakusaidia kujua ukuaji wa mimba na kama placenta bado iko hai au la!pia itakuonyesha position of the cord (kitovu) kama kimemnyonga mtoto au kiko sawa.
Kama utahitaj ufafanuz mwingine unaweza ukauliza tena!

Kamanda Moshi..nashukuru kwa maoni yako pia nampa pole mleta mada..Kumbuka mungu ndie mtambuzi wa yote hayo hata kabla ya ufahamu wetu.
Kwako Kamanda Moshi maoni yako yanaongelea watu walio karibu na hospital au vituo vya zahanati vilivyo bora ambavyo hivyo vipimo vinapatika pia na wakazi wa maeneo hayo wanakipato cha kuweza kuvipata.Kwa mimi ambaye ni balozi wa wanakijiji wangu ambao hawapo mazingira vifaa vya Utrasound havipo ni kitu gani kinaweza wasaidia?
Asante
 
Kutofautiana Rh sio tatizo kwa mume na mke na pia sio tatizo kubwa kwa mtoto wa kwanza.

Tatizo linaweza kutokea kwa mtoto wa pili na kuendelea.

Kwa vile siku hizi akina mama wengi wanahudhuria clinic ya wajawazito huweza kutambulika mapema makundi yao ya damu na hatua stahiki kuchukuliwa.

Kuna aina mbalimbali ya ushauri wa jinsi ya kuwasaidia mama wa Rh negative. Njia inayopewa nguvu zaidi ni utaratibu wa kuwachoma mama hawa sindano ya anti D antibodies week ya 28 ya ujauzito. Iwapo mjamzito atafanyiwa procedure yoyote kuanzia second trimester pia anapewa antibodies.

Mtoto akizaliwa anapimwa kundi lake la damu. Iwapo atakuwa Rh pozitive basi mama anapewa tena antibodies. Zipo sehemu ambazo wameamua hawampi tena mama baada ya kujifungua iwapo walishampa awali antibodies. Dozi hii ya baada ya kujifungua inatolewa kabla hayajaisha masaa 72 baada ya kujifungua. Baada ya hapo inakuwa "too late"...

Asante kwa maelezo...Swali la nyongeza, sindano anayochomwa mama baada ya kujifungua ni kwa ajili ya uzazi ujao, if any, au ni muendelezo wa treatment ya uzazi huu wa sasa? Nauliza hivi coz kuna mtu namfahamu amepoteza watoto wawili, wa kwanza alifanikiwa kufikisha miezi miwili, wa pili akiwa na ujauzito wa miezi 7....Na kwa watoto wote yeye alikuwa muhudhuriaji wa kliniki, kwa sababu anajielewa state yake.
 
Sindano ni prevention kwa ajili ya kizazi kijacho.

Sababu za watoto kufa zinaweza kuwa nyingi. Mama akiwa Rh neative haimaanishi sababu nyingi zinakuwa hazipo.

Kuna ugonjwa unaitwa anti phospholipid syndrom ambao sisi Bongo huwa hatucheck lakini pia ni sababu inayojitokeza mara nyingi.
 
Niwashukuru sana ndg. Mwalu , kiwaki , Isaac Chikoma , gody , measkron , ZeMarcopolo , md4doctor2000, grand-mal , hippocratessocrates , charminglady, Cathode Rays, Smile, Mwasi, King Kong III , Masuke , Kamanda Moshi , prax , Dina , Akili Unazo na wengineo kwa pole zenu, Maombi yenu, Darasa/shule mliyonipa, Ushauri wenu pamoja uchokonozi wa baadhi yenu ambao umenifanya nipate maarifa zaidi kutoka kwa madaktari wa JF.

Jana, mke wangu aliweza kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya kuwekewa vidonge na baadaye maji ya Uchungu. Kichanga kilikuwa ni cha kiume. Tunamshukuru Mungu kwa mama kuweza kujifungua salama bila kuchanika.

WanaJF Doctor, Madaktari wote TZ na wenzangu wengine, kwa kweli baada ya kupata tatizo hili kumenifanya niwe so much curious. Kwa hospitali hii niliyokuwepo ambayo ipo hapa hapa Dar Es Salaam, tena kubwa tu, wikiend hii pekee kulikuwa na akina mama wanne ambao vichanga vyao vimefia tumboni. Last two weeks kulikuwa na cases kama hizo sita. Kwa hiyo kwa mwezi wa tano tu ni vichanga atleast 10 vimefariki tumboni kwa mama zao kwa hospitali hii. Hapo hujaongelea Hospitali ya Mwananyamala, Amana, Temeke, Muhimbili na privates nyingine hapa DSM. Potelea mbali hospitali nyingine huko mikoani, wilayani, kwenye kata, na hata majumbani.

KIMSINGI, nimeona kuwa tatizo hili ni kubwa sana sana. Na nina ukakika kwa nchi zilizoendelea jambo kama hili kwa ukubwa huu lazima wangekuwa wamepata utatuzi wake mapema.

Mimi natoa RAI kwa Madaktari, Wanafunzi wa Udaktari, Wizara na Asasi za Afya kufanya utafiti wa kina kujua Magnitude ya Hili tatizo na nini zinaweza kuwa sababu za msingi kutokea kwa MAZINGIRA YETU. Labda nipo outdated, lakini naona kuwa ni mhimu sana kuwa na majibu sahihi juu ya hili katika MAZINGIRA YA NCHI YETU, la sivyo vijana wataendelea kuteketea kabla hata hawajazaliwa.

Niwashukuru tena kwa kujitoa kwenu na kunipa majibu na ushauri mzuri katika mada hii.
Asanteni.
 
Sindano ni prevention kwa ajili ya kizazi kijacho.

Sababu za watoto kufa zinaweza kuwa nyingi. Mama akiwa Rh neative haimaanishi sababu nyingi zinakuwa hazipo.

Kuna ugonjwa unaitwa anti phospholipid syndrom ambao sisi Bongo huwa hatucheck lakini pia ni sababu inayojitokeza mara nyingi.

Asante kwa elimu. Kikwetu kwetu walikuwa wana-rule out kuwa ndio sababu, kiasi kwamba na yeye muhusika ameshajichukulia kuwa ndio hivyo (muwe mnawakansel wateja wenu basi, wakati mwingine mnawaacha wakiwa wamekata tamaa)....ntafanya h/work ya kucheki hiyo syndrome uliyo-refer hapa ni nini nayo.
 
Niwashukuru sana ndg. Mwalu , kiwaki , Isaac Chikoma , gody , measkron , ZeMarcopolo , md4doctor2000, grand-mal , hippocratessocrates , charminglady, Cathode Rays, Smile, Mwasi, King Kong III , Masuke , Kamanda Moshi , prax , Dina , Akili Unazo na wengineo kwa pole zenu, Maombi yenu, Darasa/shule mliyonipa, Ushauri wenu pamoja uchokonozi wa baadhi yenu ambao umenifanya nipate maarifa zaidi kutoka kwa madaktari wa JF.

Jana, mke wangu aliweza kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya kuwekewa vidonge na baadaye maji ya Uchungu. Kichanga kilikuwa ni cha kiume. Tunamshukuru Mungu kwa mama kuweza kujifungua salama bila kuchanika.

WanaJF Doctor, Madaktari wote TZ na wenzangu wengine, kwa kweli baada ya kupata tatizo hili kumenifanya niwe so much curious. Kwa hospitali hii niliyokuwepo ambayo ipo hapa hapa Dar Es Salaam, tena kubwa tu, wikiend hii pekee kulikuwa na akina mama wanne ambao vichanga vyao vimefia tumboni. Last two weeks kulikuwa na cases kama hizo sita. Kwa hiyo kwa mwezi wa tano tu ni vichanga atleast 10 vimefariki tumboni kwa mama zao kwa hospitali hii. Hapo hujaongelea Hospitali ya Mwananyamala, Amana, Temeke, Muhimbili na privates nyingine hapa DSM. Potelea mbali hospitali nyingine huko mikoani, wilayani, kwenye kata, na hata majumbani.

KIMSINGI, nimeona kuwa tatizo hili ni kubwa sana sana. Na nina ukakika kwa nchi zilizoendelea jambo kama hili kwa ukubwa huu lazima wangekuwa wamepata utatuzi wake mapema.

Mimi natoa heko kwa Madaktari, Wanafunzi wa Udaktari, Wizara na Asasi za Afya kufanya utafiti wa kina kujua Magnitude ya Hili tatizo na nini zinaweza kuwa sababu za msingi kutokea kwa MAZINGIRA YETU. Labda nipo outdated, lakini naona kuwa ni mhimu sana kuwa na majibu sahihi juu ya hili katika MAZINGIRA YA NCHI YETU, la sivyo vijana wataendelea kuteketea kabla hata hawajazaliwa.

Niwashukuru tena kwa kujitoa kwenu na kunipa majibu na ushauri mzuri katika mada hii.
Asanteni.

Tunashukuru kama process imeenda salama, tunawatakia afya njema.

Kwa statistics zako, inaonekana tatizo sio dogo.....I wish wamama wote wangekuwa wanapatiwa masomo haya mapema, sijui huko pembezoni na challenges zake hali ikoje.
 
Kamanda Moshi..nashukuru kwa maoni yako pia nampa pole mleta mada..Kumbuka mungu ndie mtambuzi wa yote hayo hata kabla ya ufahamu wetu.
Kwako Kamanda Moshi maoni yako yanaongelea watu walio karibu na hospital au vituo vya zahanati vilivyo bora ambavyo hivyo vipimo vinapatika pia na wakazi wa maeneo hayo wanakipato cha kuweza kuvipata.Kwa mimi ambaye ni balozi wa wanakijiji wangu ambao hawapo mazingira vifaa vya Utrasound havipo ni kitu gani kinaweza wasaidia?
Asante

asante mkuu, njia rahisi kabisa ya kujua Afya ya Mimba hata kama uko kijijini ni kujifahamu wewe mwenyewe. Namaanisha mama Mjamzito ajifahamu yeye mwenyewe vizuri. hii anaweza kufanya kwa kusikiliza movement za mtoto Tumboni. Kwa kawaida kila ndani ya Lisaa 1 mtoto lazma/huwa anacheza kuanzia kwenye wiki ya 16 au wengine wanaanzia wiki ya 22.
Ni lazima mtoto acheze tumboni wakati utakapokuwa unakula chakula. sasa kama hutasikia akicheza wakati ukila basi hiyo ikufanye kutafuta msaada wa hospital/daktari mapema. kwa namna yeyote kama hukusikia movement ya mtoto (above 16 Weeks/22Weeks) ndani ya saa 24, basi fika kituo cha afya mara moja kujua nini ni tatizo.
pia level ya Amniotic fluid sometime is an indication/gives posibilities ya cord kumnyonga mtoto, (kama fluid ni nying AFI 20-24 (Polyhydramnios) kwa mimba ya wiki za 20 mpaka 35 hivi) maana kama una fluid nying tumboni basi itaruhusu movement nyingi za mtoto na wakati huo huo kutoa nafasi/uwezekano wa kitovu kumfunga shingoni. Hii unaweza kuigundua kwa mama kuwa na tumbo kubwa sana kuliko umri halisi wa mimba (provided sio Mimba ya Mapacha).
kwa vipimo vya damu ni lazima uende kituo cha afya.
 
nashukuru kwa mada nzuri wadau..ila nikisoma hapa nasikia tumbo lote linatetemeka
 
Back
Top Bottom