Gojaga Nize
JF-Expert Member
- Jul 1, 2015
- 3,177
- 2,548
ggggggggggggg
Weekend njema wapendwa wa mmu;
Nina tatizo linanitatiza.
Sijajua kama huu ni msamiati wa kiswahili au kilugha changu (Kubemenda).
Sijaoa ila nina mtoto na mwanamke ambaye ni mchumba wangu niliemtolea mahari na posa na taratibu zote bado ndoa tu. Na matumiz huwa natuma.
Yeye anaishi mbeya na wazazi wake mi nipo hapa Dar. Mwezi uliopita alikuja kunisalimia na mtoto. Mtoto yuko chini ya mwaka mmoja ila juu ya miezi sita.
Kinachonitatiza ni kuwa, afya ya mtoto sijaridhika nayo kabisa. Kind yuko below standards na alivokuwa mwanzo. Sijamuuliza hadi alipoondoka ila baadae nilikuja kukumbuka kuwa huwa kuna kitu nasikia wanabemendwa hawa yaan kama mama anajihusisha na mapenzi huku ananyonyesha. Mtoto anakuwa mzoofu..
Naombeni wajuzi mnieleweshe, je hisia zangu ziko sahihi kwa nilichokiona kwa mwanangu?
Mtoto ni mchangamfu na yuko vizuri tu ila kamwili ndo kananitatiza.. Sikuona kama ni busara kumuuliza maana angeona mi namwonaje na wakati analea. Mipango ya ndoa inaendelea.
Shikamooni wote mtakaonipa uzoefu katika hili.
mimi mgeni uko ngoja waje kina Evelyn Salt miss chagga watakusaidia ...ila naingia chimbo kusoma kuhusu ilo nitarudi
Mkuu usipende saana kuamini hayo, ulitakiwa umuulize mkeo kwann mtoto ana afya hii! Na sio kumtuhum kwamba amembemenda huenda angekupa maelezo fulan ambayo yangekupa 'insight' fulan kusaidia kujua chanzo cha afya mbaya ya mtoto
Kwanza japo sina uzoefu wa kulea, ila nadhani ulitakiwa umuulize kuhusi diet ya mtoto utaratibu wake, pia maswala ya kumnyonyesha je ananyonya vizuri? Ana tosheka?
Pia nadhani ulitakiwa umpeleke cliniks huko kwa wataalam na kuwaeleza wasiwasi wako kuhusu afya ya mwanao, wao wangekupa jibu sahihi na lenye tija. Zaidi kuliko hapa.
Nakutakia kila la kheri ufunge nae ndoa huyo mwanamke.
Tatizo ni Lishe tu. Hakuna kitu kama kubemendwa. Mama anatakiwa ale vizuri ili atoe maziwa ya kumtosha mtoto. Hali kadhalika pia kama mama hatoi maziwa ya kutosha basi mtoto apewe supplements zinazo kubalika.
Kulea ni project kaka. Unaonaga watoto wetu wanapendeza unafikiri inatokea natural? Toa hela ya kutosha uone kama hajabadilika
mimi mgeni uko ngoja waje kina Evelyn Salt miss chagga watakusaidia ...ila naingia chimbo kusoma kuhusu ilo nitarudi
Ha haaa mkuuu ukimwita Evelyn Salt hakawii kusema ulichapiwa....
Ha haaa mkuuu ukimwita Evelyn Salt hakawii kusema ulichapiwa....
sumbai huyo Evelyn Salt hachelew kusema hivyo
ngoja tumsubiri ila kwa Evelyn Salt namuelewa yupo vizuri
Kwanza hiyo kitu kubemenda huwa haipo, ni story tu ilikua inatumika na wazee ili kuweka discipline kwa mwanamke mwenye mtoto mdogo "watu wasipige"....
Mwanamke akishatumika huko anaogopa kunyonyesha kwa Hofu Ya kubemenda mtoto, sasa kinachomdhoofisha mtoto hapo ni hiyo kuacha kunyonyeshwa. Ni kama story ya mjamzito hatakiwi kula mayai kwamba mtoto atazaliwa hana nywele hiyo kitu haipo ni vitisho tu kuzuia vitu flani flani.
Ulitakiwa umuulize na muongee kuhusu afya ya mtoto na sio kuhisihisi....kulea sio kazi ndogo.
Kwa hiyo kugongwa nje au kugonga nje ruksa tuuu....hamna madhara. Nlikuwa naogopa...ngoja nianze sasa.....
Asante kwa elimu,mwl
kwanza nikuulize huwa unafuatilia maendeleo ya mtoto anapoenda clinic? bila shaka hata huwa haulizi wala hujui mtoto lini anapelekwa clinic, mtoto anakula nini? ukiwa unafuatilia hayo ni rahis kumuuliza kwann mtoto uzito unapungua kila mwez? hapo ndo mwanzo wa kujua tatzo..
ushauri.
fuatlia record za clinic, fuatilia lishe yake.. na pata ushauri kuhusu lishe ipi inamfaa mtoto, na mazingira pia.. pengne mbeya barid limemkataa mtoto.. usipende kutoa maamuz bila kufanya uchunguz wa kina. ni hayo tuuu..