Mtoto kakolea haswaa, hanijui cmjui ila kanipenda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto kakolea haswaa, hanijui cmjui ila kanipenda

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mnyikungu, Jun 22, 2012.

 1. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,447
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Wadau, wahenga wanasema ukistaajabu ya musa basi utayaona ya firauni, ilikuwa jumatano nimekaa nimetulia ofisini nafanya michakato kiofisi,mara nikaona sms kuisoma ikawa na ujumbe huu "mambo mpendwa nimekumic vibaya mno mpe hi mm" kiukweli nilishangaa why numba ngeni iniandikie hivyo? bila hiana nikanyanyua cm niampigia aliyenitumia nikasikia sauti ya kike inaongea, nikamwambia dada samahani umekosea namba umetuma sms yako kwangu, dada akakubali akasema kweli amekosea lengo lake lilikuwa kumtumia mchumba ake, akaniomba msamaha nikamsamehe kisha nikakata simu, cha kushangaza baada ya kukata simu alibeep tena mara tatu, ah! mi nikaona niachane naye. kesho yake akabeep tena nikamchunia siku ya tatu yake akatuma sms kuniuliza kama mi namfahamu na pia nimtajie jina langu kama ananifaham, mi nilimwambia cmfaham na wala jina lake cjawahi kuliona sehemu hali kadhalika naye akasema hanijuia lakini akasema tunaweza tukawa marafiki, mi nikasema powa tukachati toka saa 8 mbaka saa 11 ndo akatuma sms akasema nisimshangae ameona bora awe muwazi ila amenipenda ghafla japo ana mchumba, ahaa mi nikamjibu "makubwa!" kiukweli alijieleza sana kupita maelezo, mtoto alinimwagia mistari ajabu! nikaanza kujiuliza je ni kweli ananijua au ananijua ila anataka tu kunitania?

  sio siri nilihisi kama kuna mchezo nafanyiwa kwasababu sehemu anayotokea ndo huko yupo mtani wangu fulani kwa hiyo nikampuuzia, kesho yake mtoto akaja na swaga zaidi ya jana nikawa nacheka sana huku nikimjibu majibu ya mzaha na ya kumkatisha tamaa. ilipofika jumamosi mara akaniambia mama ake ameugua ghafla presha na amelazwa na kulingana na hali yake hana matumaini kama atapona.kiukweli niliingiwa na huruma nikaanza kumfariji juu ya mgonjwa, ilpofika kesho yake nikamtumia sms ,"vipi best mgonjwa anaendeleaje na wewe umeamkaje?" cikujibiwa, nikatuma sms nyingine best mi nasubiri jibu toka kwako hakujibu, nikakaa kama nusu saa kisha nikapigiwa simu ambyo ilinitaarifu juu ya kifo cha mama wa huyu dada lakini nikpewa taarifa ya nyongeza na ya kushtua kuwa hata yule dadad amelazwa kutokana na mshtuko wa kufiwa na mama yake, hapo tena nikaingiwa na roho ya huruma ilipofika jioni nikampigia cm akapokea mtu mwingine akaniambia mgonjwa hawezi kuongea na mimi. kesho yake nikapiga cm yule dada akaongea na mimi japo kwa shida na akasema wameishazika, sio siri nilikuwa namtumia sms nyingi za kumfariji na nashukuru alifarijika maana ilipofika kesho yake machungu yakawa yamepungua kwasababu hakupata mda wa kuwaza maana mda wote milimkeep bize kwenye chating.

  kasheshe lilipoanza ni pale alipoanza kukumbushia sms yake ya kunipenda ghafla, lakini wakati huohuo na mimi bado nilikuwa namtafakari kwanini ananipenda mtu ambaye hajawahi kuniona wala hanijui? sasa ili kujua ukweli nikaamua nimkubalie maana niliona nikimkubalia ndo ataniambia chanzo cha yeye kunipenda ghafla. ni kweli wazo langu lilifanikiwa na nikajua kipindi anachoniambia ananipenda alikuwa ametoka kugombana na mchumba wake ambae wamezaa naye mtoto mmoja, kwa hiyo alinipenda mimi akiwa na hasira, maana bado alionekana kiishara kama anampenda mno bwana ake, lakini tatizo ndo alikuwa ameanzisha mahusiano na mimi.baada ya kugundua hivyo nikaanzisha mchakato wa kumshawishi yeye aendelee na mchumba ake na nikamwambia kuwa wanaume siku hizi hatuna jipya, anaweza akamkimbia yule akahisi anakuja kwangu labda kuna unafuu kumbe huku ndo balaa yaani anakuwa anaruka mkojo na kukanyaga kinye.......,na nilimtamkia kuwa mi nitampenda tu hata akiolewa na kwasababu wamezaa naye mtoto nikamwambia ni vyema waoane ili walee mtoto ktk misingi na malezi mema na mtoto afaidi ule upendo wa babab na mama.da! maskini! ckujua! kumbe ushauri wangu ndo ulniongezea maksi akazidi kunipenda zaidi.

  Jamaa yake juzi tu alipoona mchumba ake amebadilika akona asije akamkosa ndo kamtangazia ndoa, amini usiamin kwa maelezo yake ni kuwa hana hamu na huyo jamaa sababu jamaa amezaa pia na mtu mwingine ila hakumwambia na ndo kisa kilichofanya wagombane kwa hiyo hata hamitaji na anatamani akimbilie kwangu sababu hata ndugu zake ni wapambe wa mchumba ake ambaye wamekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka saba.

  kwa kweli tunaitana wapenzi na tunatumiana sms kwa siku zaidi ya mia tano, mimi kwangu naona poa sababu namuenjoy ila yeye ndo yuko serious sana na hii ishu, kinachozidi kunishangaza mwanamke ana wivu na mimi cjapata ona japo nimemwambia nina mchumba ila yeye kasema poa. usiku akiwa hana usingizi huwa ananipigia cm kisha tunaongea mbaka asubuhi kama mapenzi ya wanafunzi yalivyo.saa hizi anafanya juu chini aje anisalimie pamoja na kubadilishana ujuzi wa kiutu uzima.

  da! cjafurahi hata kidogo najaribu bado kumkatisha tamaa na kumsihi arudishe moyo kwa bwana ake ila hataki, na mimi tatizo langu ni mdadisi mno yaani nasubiri kuuona mwisho wake ni nini? na pia kwasababu tumekubaliana kuwa ye akubali kuolewa"kitu ambacho kitanisaidia mimi" kisha mimi nitaendelea kuwa naye hata kama kaolewa, hapa tena nadadisi je atawezaje kuwasiliana na mimi na mwisho ataamua nini?

  waungwana kwenye cm kanipenda sana, kafa kaoza, muda mwingi anapoteza kuchati na kuongea na mimi kwa simu, usiku huanzisha maneno ya kimahaba kisha husema kuwa eti ananitamani.

  UPDATES:
  Wakuu bado tunaendelea na huyu mtu, siku ile wakati napost hii ishu nilikaa masaa machache tukagombana na kupigana kibuti kisa eti kwanini niliongea na simu mda mrefu, kweli niliongea na simu kama lisaa limoja hivi so yeye kila akinitafuta aliona simu inatukika ndo akakasilika na akazima simu huku akiwa amenitumia sms za kuniacha eti nifute namba yake kwenye simu yangu.

  siku ya pili yake mi nikamtumia sms kumuuliza je anatania au yuko serious?, akasema yuko serious na hataki kuendelea na mimi maana ananiona mi kama mtu wa totoz sana, nilijifanya namuomba msamaha kwa mda mrefu japo sikuwa na kosa, he! si ndo akakomaa, mwisho na mimi nikamwambia simuhitaji coz ana wivu sana bora aende. alikubali kishujaa akidhani natania, yakapita masaa matatu mwenyewe akaanza kunitumia sms za kichokozi ambazo mi ckuzijibu, ilpofika jioni akaamua apige simu, mi nikaipokea eti akaniuliza niko wapi? mi nikamwambia niko mtaani nafanya zoezi la kumsahau akakata simu.

  ilipofika jioni kama saa moja nikaanza kupokea sms za kashfa kutoka kwake, eti woo nimezoea kuwachezea washamba wenzangu wa iringa ye cmwezi mara ooh! kama sina kazi nirudi kijijini nikarime na kashfa nyingine nyingi huku akinilaumu eti nimemtukana, kama kawaida yangu mi ckumjibu chochote, ilipofika kesho yake akaendelea tena kunitukana nikamuuliza kulikoni why ananitukana? akasema eti nicmfanye yeye mtoto mdogo akasema eti nimetumia namba ngeni kumtukana yeyey, kitu ambacho ckukifanya, nikamwambia una uhakika na hayo uanyosema akasema nicmzingue ana uhakika kuwa ni mimi maana mwenye namba yake tuliyegombana ni mimi tu. ah! mi nikamwambia sasa nimechoka kama vp tusitumiane sms yoyote.
  ilipofika juma tatu akaniambia nimbadilishie password za email niliyomfungulia, bila kinyongo mi nikambadilishia kwa kuweka namba yake ya simu.

  baada ya kumbadilishia email ghafla akaniomba nimtumie picha yangu bila shida mi nikamtumia, alipoziona ghafla akaanzisha mawasiliano tena kwa kasi huku akinisifia kuwa ninaonekana mtundu kwenye yale mambo mara ohoo! umbo langu linamhamasisha kuwa na mimi mara ohoo! naonekana nina busara na hekima hivyo anahisi mi ndo chaguo lake. Ilipofika jumanne na mi nikamuomba anitumie picha yake, akaanza mara ohoo! nimefanana na ray c mi nikamuuliza kitabia? akasema umbo, mara ye ni mnene kiasi hapo nikaona ameanza kujishtukia basi mwisho nikamwambia sina shida na hiyo picha ye akasema hamna atanitumia tu hata kama sitaki.

  ilipofika jana jumatano asubuhi akaniambia kuwa leo lazima nikutumie nikamwambia itavyokuwa poa, ilipofika mchana akasema tumbo linamuuma, mi nikaona hivi ni viteteo ili asinitumie picha. ilipofika saa moja akasema cafe kuna foreni sana so hana uhakika kama atafanikiwa kunitumia, mi nikamwambia ikiwezekana poa isipowezekana powa, ilipofika saa mbili akaniambia amenitumia tiyali kwa email yangu. nilifungua email yangu kweli nikakuta picha yake na mtoto wake, ha haaaaaaaa! ni wa kawaida sana hafanani na sauti yake, ni mweupe mnene kidogo.

  kiukweli hajanivutia, but still namuenjoy ili nione mwisho wake, nimemwambia kuwa mi nahiji mtoto sa yeye atawezaje kunizalia wakati anatarajia kuolewa na huyo mchumba wake? kasema hilo kwake ni dogo sana atanizalia tu hata akiolewa tena atahakikisha mtoto wa ndani ya ndoa atakuwa wangu, maana yeye tiyari kisha zaa na huyo anayetaka kumuoa. nilichokiona kwenye mapenzi ya huyu mwanamke na jamaa yake yawezekana yamekaa kikiloni mno, hawana jipya kwenye ndoa zao namaanisha jamaa kajisahau sababu anauhakika kwa kuwa kasha mzalisha hivyo hana ubunifu wa namna ya kumjali na kulinogesha penzi lao.

  pia nataka nihakikishe kama ni tapeli au la ndo maana simkatishi tamaa, nitawajuza wanajamvi

   
 2. asrams

  asrams JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 4,026
  Likes Received: 1,396
  Trophy Points: 280
  Hahaha duh,


  Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  Mmh! Lucky me foolish age ilinijia vizuri!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,879
  Likes Received: 83,359
  Trophy Points: 280
  unaye huyo...hataachana nawe mpaka kieleweke lol!
   
 5. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,142
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  mmh!!!.....
   
 6. Kitoabu

  Kitoabu JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 5,765
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  Mbona hizi bahati hazinotekei mimi Jaman, hata kukosea namba Jaman, we king'asti embu jikoseshe namba ijipige kwangu
   
 7. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Changu hilo kuwa makini mpwa asije akakumalima
   
 8. N

  Neylu JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kaka kuwa mwangalifu kwa hili jambo.. Hii kitu mliyoianzisha itawa cost, trust me.. Tena ukimuendekeza atakuharibia kwa huyo mchumba uliye naye.. Ungekuwa huna mchumba ingekuwa poa ila.... WATCH OUT..
   
 9. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  Una umri gani?
   
 10. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Same story imenitokea na mimi yapata miezi miwili iliyopita..ila huyu wangu alipoona namdadisi sana amekata mawasiliano..Naye alikuwa na mtoto waliezaa na jamaa yake na kwamba kwa sasa wana ugomvi wameachana.

  Kila siku nilkuwa nampiga mitego kwenye simu mpaka kaona hakuingiliki sasa hivi amebadilisha namba.

  Chunga sana...mtu gani kwa kipindi kifupi cha msiba wa mama yake karudi in normal state na kuanza habari ya mapenzi. Mjini hapa
   
 11. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,350
  Likes Received: 2,688
  Trophy Points: 280
  hahaha this dude is in deep shit lol
   
 12. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  King'asti nnakupenda sana tu mine through jf. Nina gelofrend lakini simtaki, nakutaka wewe.

  Sent from my nokia ya toch c12
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,350
  Likes Received: 2,688
  Trophy Points: 280
  ni charming... nini? hahaha am jst kiddin dude.
  kaka hii makitu ishawahi kunitokea hata mimi, a long tym ex-gf ambaye kashaolewa na kazaa lakini hana furaha na ndoa alianza kunitokea na alikua tayari aombr talaka, kwa busara nikamjibu that aint right....
   
 14. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kilichobakia ili kumkatisha tamaa ni kuwa mzembe kunako sita kwa sita, onesha 10% efficiency, hakyanani ataondoka tu.
   
 15. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,447
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  king'ast muelewe huyu
   
 16. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,447
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  update za usiku huu ni kwamba kamenimwaga eti kisa kameona nimeongea na mtu lisaa lizima, ha ha haaaaaaaaaaaa! inafurahisha sana
   
 17. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,447
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  mi ni miaka 27 tu ndo anataka kuniua jamani
   
 18. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Nahisi hata huo msiba wa Mama yake haukutokeo kipindi mnaanza mahusiano ya kwenye simu ila Mama yake hata kama kweli kavuta, ni muda umepita. Na huyo si kwamba kafa kaoza kwako, ila kwa kuwa mjini ni shule, huyo alishahitimu mafunzo yake na sasa yuko kazini.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 19. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,447
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  kama yuko kazini mi niko kazini zaidi yake, alipolala mi ndo nilipoamkia, hata hanipi shida, but pia nimemwambia kuwa mi maskini kabisa, ila hajakata tamaa anataka afunge safari kutoka dar kuja iringa
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  mabreka haya..
   
Loading...