Mtoto kakolea haswaa, hanijui cmjui ila kanipenda

siku si nyingi utaibiwa wewe, mjini hapa.....

Kuna wadada wz mujini wanatumia style hiyo kunasa wanaume wenye fedha..... Shaurilo
 
Mkuu usiwe happy sana coz wote bado hamjaonana, ila mkishaonana ndio nadhani utajuwa kama kuna mapenzi ya kweli msije kimbiana tu hiyo siku ya kuonana
mkuu cjafurahi kwa yeye kunipenda ila naenjoy namna banavyotoa hsia zake, kiukweli huwa nacheka sana, cku uwa inaisha vizuri kwa sababu yake
 
Wewe unamdanganya mwenzio. Hajaona sura yake, hips, na kuonja utamu wake unamshauri afanye kazi chini ya kiwango? Anaweza kuchanganyikiwa na uzuri wake akajituma kikwelikweli ili kumsahaulisha mchumba wake!

Then hayo yatakuwa ni matokeo mengine ambayo hakuyatarajia. Unless otherwise he should stick to the plans za kumuacha huyo mtu.
 
Kijana kuwa mwangalifu, siku hizi ni mbaya mno. Wewe unachat na mtu hata hujawahi mwona kwa nini usifanye mpango ukaonana naye kisha ukatoa uamuzi?

Pengine ni mtu wa karibu sana anaku enjoy au anataka kuvuruga mahusiano yako?


Wadau, wahenga wanasema ukistaajabu ya musa basi utayaona ya firauni, ilikuwa jumatano nimekaa nimetulia ofisini nafanya michakato kiofisi,mara nikaona sms kuisoma ikawa na ujumbe huu "mambo mpendwa nimekumic vibaya mno mpe hi mm" kiukweli nilishangaa why numba ngeni iniandikie hivyo? bila hiana nikanyanyua cm niampigia aliyenitumia nikasikia sauti ya kike inaongea, nikamwambia dada samahani umekosea namba umetuma sms yako kwangu, dada akakubali akasema kweli amekosea lengo lake lilikuwa kumtumia mchumba ake, akaniomba msamaha nikamsamehe kisha nikakata simu, cha kushangaza baada ya kukata simu alibeep tena mara tatu, ah! mi nikaona niachane naye. kesho yake akabeep tena nikamchunia siku ya tatu yake akatuma sms kuniuliza kama mi namfahamu na pia nimtajie jina langu kama ananifaham, mi nilimwambia cmfaham na wala jina lake cjawahi kuliona sehemu hali kadhalika naye akasema hanijuia lakini akasema tunaweza tukawa marafiki, mi nikasema powa tukachati toka saa 8 mbaka saa 11 ndo akatuma sms akasema nisimshangae ameona bora awe muwazi ila amenipenda ghafla japo ana mchumba, ahaa mi nikamjibu "makubwa!" kiukweli alijieleza sana kupita maelezo, mtoto alinimwagia mistari ajabu! nikaanza kujiuliza je ni kweli ananijua au ananijua ila anataka tu kunitania?

sio siri nilihisi kama kuna mchezo nafanyiwa kwasababu sehemu anayotokea ndo huko yupo mtani wangu fulani kwa hiyo nikampuuzia, kesho yake mtoto akaja na swaga zaidi ya jana nikawa nacheka sana huku nikimjibu majibu ya mzaha na ya kumkatisha tamaa. ilipofika jumamosi mara akaniambia mama ake ameugua ghafla presha na amelazwa na kulingana na hali yake hana matumaini kama atapona.kiukweli niliingiwa na huruma nikaanza kumfariji juu ya mgonjwa, ilpofika kesho yake nikamtumia sms ,"vipi best mgonjwa anaendeleaje na wewe umeamkaje?" cikujibiwa, nikatuma sms nyingine best mi nasubiri jibu toka kwako hakujibu, nikakaa kama nusu saa kisha nikapigiwa simu ambyo ilinitaarifu juu ya kifo cha mama wa huyu dada lakini nikpewa taarifa ya nyongeza na ya kushtua kuwa hata yule dadad amelazwa kutokana na mshtuko wa kufiwa na mama yake, hapo tena nikaingiwa na roho ya huruma ilipofika jioni nikampigia cm akapokea mtu mwingine akaniambia mgonjwa hawezi kuongea na mimi. kesho yake nikapiga cm yule dada akaongea na mimi japo kwa shida na akasema wameishazika, sio siri nilikuwa namtumia sms nyingi za kumfariji na nashukuru alifarijika maana ilipofika kesho yake machungu yakawa yamepungua kwasababu hakupata mda wa kuwaza maana mda wote milimkeep bize kwenye chating.

kasheshe lilipoanza ni pale alipoanza kukumbushia sms yake ya kunipenda ghafla, lakini wakati huohuo na mimi bado nilikuwa namtafakari kwanini ananipenda mtu ambaye hajawahi kuniona wala hanijui? sasa ili kujua ukweli nikaamua nimkubalie maana niliona nikimkubalia ndo ataniambia chanzo cha yeye kunipenda ghafla. ni kweli wazo langu lilifanikiwa na nikajua kipindi anachoniambia ananipenda alikuwa ametoka kugombana na mchumba wake ambae wamezaa naye mtoto mmoja, kwa hiyo alinipenda mimi akiwa na hasira, maana bado alionekana kiishara kama anampenda mno bwana ake, lakini tatizo ndo alikuwa ameanzisha mahusiano na mimi.baada ya kugundua hivyo nikaanzisha mchakato wa kumshawishi yeye aendelee na mchumba ake na nikamwambia kuwa wanaume siku hizi hatuna jipya, anaweza akamkimbia yule akahisi anakuja kwangu labda kuna unafuu kumbe huku ndo balaa yaani anakuwa anaruka mkojo na kukanyaga kinye.......,na nilimtamkia kuwa mi nitampenda tu hata akiolewa na kwasababu wamezaa naye mtoto nikamwambia ni vyema waoane ili walee mtoto ktk misingi na malezi mema na mtoto afaidi ule upendo wa babab na mama.da! maskini! ckujua! kumbe ushauri wangu ndo ulniongezea maksi akazidi kunipenda zaidi.

Jamaa yake juzi tu alipoona mchumba ake amebadilika akona asije akamkosa ndo kamtangazia ndoa, amini usiamin kwa maelezo yake ni kuwa hana hamu na huyo jamaa sababu jamaa amezaa pia na mtu mwingine ila hakumwambia na ndo kisa kilichofanya wagombane kwa hiyo hata hamitaji na anatamani akimbilie kwangu sababu hata ndugu zake ni wapambe wa mchumba ake ambaye wamekuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka saba.

kwa kweli tunaitana wapenzi na tunatumiana sms kwa siku zaidi ya mia tano, mimi kwangu naona poa sababu namuenjoy ila yeye ndo yuko serious sana na hii ishu, kinachozidi kunishangaza mwanamke ana wivu na mimi cjapata ona japo nimemwambia nina mchumba ila yeye kasema poa. usiku akiwa hana usingizi huwa ananipigia cm kisha tunaongea mbaka asubuhi kama mapenzi ya wanafunzi yalivyo.saa hizi anafanya juu chini aje anisalimie pamoja na kubadilishana ujuzi wa kiutu uzima.

da! cjafurahi hata kidogo najaribu bado kumkatisha tamaa na kumsihi arudishe moyo kwa bwana ake ila hataki, na mimi tatizo langu ni mdadisi mno yaani nasubiri kuuona mwisho wake ni nini? na pia kwasababu tumekubaliana kuwa ye akubali kuolewa"kitu ambacho kitanisaidia mimi" kisha mimi nitaendelea kuwa naye hata kama kaolewa, hapa tena nadadisi je atawezaje kuwasiliana na mimi na mwisho ataamua nini?

waungwana kwenye cm kanipenda sana, kafa kaoza, muda mwingi anapoteza kuchati na kuongea na mimi kwa simu, usiku huanzisha maneno ya kimahaba kisha husema kuwa eti ananitamani.
 
ni charming... nini? hahaha am jst kiddin dude.
kaka hii makitu ishawahi kunitokea hata mimi, a long tym ex-gf ambaye kashaolewa na kazaa lakini hana furaha na ndoa alianza kunitokea na alikua tayari aombr talaka, kwa busara nikamjibu that aint right....

wee,ile ilikuwa flirting. ama hujui maana ya chit chat?
 
muacha akufuate alafu iringa sasa hivi si ndo msimu wenu wa baridi? luck u blankenti chapa mtu linajileta lenyeweeeeeeeeeeee utafaidije!
 
Miaka yenu mingapi? I mean wewe una umri gani na huyo mwenzio ana umri gani? Nakuwa na wasiwasi isijekuwa ni foolish age..!
 
Same story imenitokea na mimi yapata miezi miwili iliyopita..ila huyu wangu alipoona namdadisi sana amekata mawasiliano..Naye alikuwa na mtoto waliezaa na jamaa yake na kwamba kwa sasa wana ugomvi wameachana.

Kila siku nilkuwa nampiga mitego kwenye simu mpaka kaona hakuingiliki sasa hivi amebadilisha namba.

Chunga sana...mtu gani kwa kipindi kifupi cha msiba wa mama yake karudi in normal state na kuanza habari ya mapenzi. Mjini hapa
Mkuu haya mambo ya social interaction kupitia mitandao/simu ni ya hatari sana kwa wanetu.
 
yaani hapo naona kama nawe umeona umefika .. ila kuwa makini kwa jinsi ya maelezo unaonyesha unamjali huyo kuliko kumjali mchumba wako .. uko kwenye matatizo ya kujitakia na utajilaumu
 
Mkuu haya mambo ya social interaction kupitia mitandao/simu ni ya hatari sana kwa wanetu.

Tena hatari si kidogo..wengi wanaamini ukiongea na mtu usiyemjua kwenye simu/internet anaweza kuwa right person kwake..au tajri fulani hivi..ni kma wanacheza kamari. Wanaamini watu hao ni tofauti na tunawaona mitaani!!

Amini usiamini sasa hivi kwenye inbox yangu facebook kuna mmoja nachat naye..Mwelekeo uleule!!
 
1. Kwasiku mnachati sms 500?
2. Mnaongea na simu usiku kucha?
3. Unamchumba!!

Vp ndugu majukumu mengne yanakwenda kweli, maana hyo spidi mlokuja nayo ni zaid ya "HAPPYNATION"
 
mkuu cjafurahi kwa yeye kunipenda ila naenjoy namna banavyotoa hsia zake, kiukweli huwa nacheka sana, cku uwa inaisha vizuri kwa sababu yake

Aminia mkuu wangu na ndio hivyo, kama ukimuona na umemuona ametulia then kula mzigo tu hamna kulemba kaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom