Mtoto Huyu Anauzwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto Huyu Anauzwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 10, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  <table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
  [​IMG]
  Mtoto huyu anapigwa mnada na baba yake</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Thursday, May 27, 2010 12:13 AM
  Mtoto huyu wa kichina akiwa amefungwa minyororo kwenye mlingoti wa alama za barabarani, anapigwa mnada barabarani na baba yake ambaye ameamua kumuuza ili akatumike kama mtumwa.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Mtoto wa Kichina mwenye umri wa miaka minane akionyesha wazi hofu iliyotanda uso wake, alisimama pembeni ya barabara akiwa amefungwa minyororo na baba yake ambaye alikuwa akijaribu kumuuza mtoto huyo kwa kupiga kelele kama wauza mitumba.

  Baba wa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Yong Tsui aliweka meza ndogo mbele ya mtoto huyo akiandika jina, umri na uwezo wa kufanya kazi wa mtoto wake ambaye aliamua kumuuza kama mtumwa.

  Baadhi ya watu waliojitokeza kumnunua mtoto huyo walimuuliza baba yake kiasi cha chakula ambacho mtoto wake anaweza kula, swali hilo liliwakasirisha wasamaria wema ambao walianza kumshushia kipigo baba wa mtoto huyo.

  Polisi waliwahi kumuokoa Yong kabla hajauliwa na wakazi wa jimbo la Wuhan, lililopo ukanda wa kati wa China.

  Polisi walimchukua mtoto huyo ambaye hivi sasa anapewa matunzo na serikali. Baba wa mtoto huyo aliwaambia polisi kuwa mama wa mtoto wake alifariki miaka mitatu iliyopita na tangu wakati huo amekuwa akipata tabu kumpa matunzo mtoto huyo.

  "Hana kazi, nyumba wala pesa, anasema kwamba hakuhitaji pesa kwa kumuuza mtoto wake alikuwa akijaribu kumtafutia maisha bora mtoto wake", alisema mmoja wa maafisa wa polisi.

  Yong alisema kwamba alisoma habari ya mtoto wa China, Cheng Jingdan, mwenye umri wa miaka miwili ambaye baba yake alikuwa akimfunga minyororo kwenye mlingoti wakati akiwa kazini kwa kuhofia watu wasimuibe mtoto wake.

  Mtoto Cheng alichukuliwa na wasamaria wema na kupewa maisha bora baada ya picha yake akiwa amefungwa kwenye minyororo iliposambazwa kwenye vyombo vya habari.

  Yong kwa kujaribu kumuuza mtoto wake alitegemea bahati kama hiyo ingemdondokea na mtoto wake lakini matokeo yake aliokolewa na polisi kutokana na kipigo cha wananchi wenye hasira.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; text-align: center; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;">
  </td></tr></tbody></table>
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Huu ni ucheshi!
   
 3. Nyaralego

  Nyaralego JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2010
  Joined: Nov 13, 2007
  Messages: 732
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ukatili...
   
 4. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  inawezekana, unaweza kuwa ni mkanda wa picha tu, au inawezekana..ulaya mashariki wanawake wanauzwa sana kwenda kuwa makahaba ulaya magaribi...duniani kuna kila aina ya uovu hata ambao haujawai kuuona..
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  human trafficking..ni aina mpya ya utumwa unaopigwa vita.
   
 6. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ni kweli ngoshwe, human trafficking ina kua kwa wingi sana, the leading country in africa is nigeria, nchi zile za ulaya mashariki iliyokuwa ndani ya urusi ya zamani, hii kitu iko juuu sana kwasababu ya umasikini....nchi za far east kama hizo iko juu pia...ila iyo ya hapo, nafikiri ilikuwa movie tu, human trafficking hufanywa kwa usiri mkubwa na huwa iko kwenye network kama ilivyo biashara ya madawa ya kulevya, sio open market kihivyo...kwa mwaka inaingiza kama 7 trillion dollars dunia nzima...hakuna duniani wanafanya kweupe ivyo...haipo kabisa...

  china kuna wizi wa watoto wa hali ya juu kuliko sehemu zote duniani, kwasababu mtoto akiibiwa mdogo wa umri huo, akija kuwa mkubwa huwezi kumtambua kabisa, si wanafanana...
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wamechanganyikiwa tu hao!!:sick:
   
Loading...