Mtoto atekelezwa

Mjukuu.Slim

Member
Nov 18, 2015
31
35
Mtoto huyo pichani katelekezwa na Mdada haifahamiki kama ni mzazi wake au Mlezi tu.Dada huyo alikodi bajaji huko maeneo ya yombo makangarawe na baada ya hatua chache dada huyo alimuamuru dereva huyo asimame ili ampitie rafiki yake ndipo akashuka nakutokomea kusikojulikana nakumuacha Mtoto huyo akiwa na dereva bajaji asijue hatma yake.Mtoto huyo yupo polisi chang'ombe kahifadhiwa kwa yoyote anaemfahamu awe rafiki, ndugu au jirani afike kituoni chang'ombe kwa kumsaidia mtoto huyo.
 

Attachments

  • 1451801594301.jpg
    1451801594301.jpg
    23.9 KB · Views: 37
Can the TVs in tz put the baby's PIC or video on the breaking news?? Please can someone do it. We who went through labour pain know how it pains to watch and read such sad news.
 
Wanaweke si marafiki wazuri hata kidogo, wapatapo hali ngumu huangalia maslahi binafsi. Dah ngoja niishie hapa maana asifie
mvua.........
 
Wito kwa dada zangu.

Zaeni kwa malengo tafadhalini, maisha ni magumu hakuna mfano.mpaka wanaume wanatafuta namna ya kuhifadhiwa.
 
Can the TVs in tz put the baby's PIC or video on the breaking news?? Please can someone do it. We who went through labour pain know how it pains to watch and read such sad news.
Nimekuelewa kwa sababu umeandika kiswahili...
 
Wito kwa dada zangu.

Zaeni kwa malengo tafadhalini, maisha ni magumu hakuna mfano.mpaka wanaume wanatafuta namna ya kuhifadhiwa.
kwani umeshajua kisa kilichopelekea huyo mama kutelekeza mtoto? Unajuaje kama alizaa kwa malengo ila sasa lengo limelengwa akaingia kwenye sononi au unusu kichaa au hali iliyomfanya mwisho wake wa kufikiri uishie hapo alipoishia? Mi nashukuru hata kamuacha kwenye mikono ya dereva wa bajaji. Mwingine angenyonga atupe kwenye choo cha shimo.
 
Kila baya Ni baya tu, hakuna afadhari hapo, hiyo mama alidhamilia alichokifanya kwa akili take timamu wala hakufanya bahati mbaya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom