Mtoto anachemkaaa akipimwa hana malaria....

Mimi sio mganga wala daktari, dawa za michango kwa watoto hupatikana kwenye maduka ya dawa za asili au wamasai (haswa mama yo-yo)
Mkuu wew ndio dokta sasa.

Nisaidie mkuu na mm nizijue dawa za kutibu hilo tatizo angalau kwa majina.

Maana hata mm nafahamu hilo tatzo madaktar wengi hawalijui na huwapa watto wengi dawa kwa kuhis ni tatizo jingine na kushindwa kujua ni nn tatizo kwa mtto.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msaada wenu wapendwa mwanangu ana miezi 5 amekuwa akisumbuliwa na homa yaan anakuwa na joto kalii kichwani mikononi na tumbo ila kila nikienda hospital mtoto hana malaria. Japo mwanzo nilimkuta damu kimepungua sana akapewa dawa kwa sasa damu ni 12.3 na hana
Tatizo jingine je shida yaweza kuwa nini?
Mkuu homa na joto la mwili kuongezeka ni dalili ya mabadiliko flani Katika mwili au kwa kibaiolojia tunaita "stimuli",mabadiliko haya yanaweza letwa na sababu mbalimbali ikiwemo magonjwa,maambukizi,mabadiliko ya tabia ya nchi au hali ya hewa,n.k.Hivyo basi ni vyema umpeleke mtoto hospitalini na apimwe vipimo Vingi,tofauti na kawaida yetu wabongo kuishia kupima malaria na UTI tuu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hukamaliza kuandika lakini joto zaidi ya degree 37 si hali ya kuiacha kwa muda mrefu.

Kama una feni muwashie
Mmkande kwa maji ya baridi
Punguza nguo ikiwezekana abaki na nepi
Mpe Panasonic au paracetamol

Hahah!!!

Hapo penye mtoto apewe "Panasonic"...khaaa nimejikuta nimecheka mno!!!

Si ajabu sasa hivi mtoto anasokomezwa mdomoni kimusic system au kieletronic device chochote cha Panasonic...
 
Hahah!!!

Hapo penye mtoto apewe Panasonic...khaaa nimejikuta nimecheka mno!!!

Si ajabu sasa hivi mtoto anasokomezwa mdomoni kimusic system au kieletronic device chochote cha Panasonic...
Ni paracetamol mkuu
 
Mtoto mwenye umri huo miezi mitano joto huletwa na utokaji wa meno, so mpe panado mpunze nguo, mkande kidogo, usitumie feni maana feni huleta kifua kikali
 
Tafuta msspecialist wa watoto akina DR,Massawe,maana ushauri mwingine mmmm!
naungana na aliyekushauri kupima UTI
iliwahi kunisumbua sana kwa mwanangu.
 
Msaada wenu wapendwa mwanangu ana miezi 5 amekuwa akisumbuliwa na homa yaan anakuwa na joto kalii kichwani mikononi na tumbo ila kila nikienda hospital mtoto hana malaria. Japo mwanzo nilimkuta damu kimepungua sana akapewa dawa kwa sasa damu ni 12.3 na hana
Tatizo jingine je shida yaweza kuwa nini?
Sababu kubwa 3 zq mtoto mchanga kuchemka sana:
1. Malaria(maleria)
2. Pneumonia(vichomi)
3. UTI(maambukizi kwenye njia ya mkojo).

NB: (a) sio kila homa ni malaria. Peleka hospitali huyo.
(b) wazazi wengi huwa wabishi sana kukubali watoto wao wachanga wapimwe mkojo, hawaamini kama wanaweza umwa UTI, wanaona ni kitu cha ajabu. Itakuwa ni ajabu kama kuna mwanaJF mwenye fikra za namna hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hukamaliza kuandika lakini joto zaidi ya degree 37 si hali ya kuiacha kwa muda mrefu.

Kama una feni muwashie
Mmkande kwa maji ya baridi
Punguza nguo ikiwezekana abaki na nepi
Mpe Panasonic au paracetamol
Mfumo wao wa upumuaji haujakomaa. Anaweza kupata mafua na almonia ( almonia kama nimekosea spelling)

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani hapo kwenye "Panasonic" na " Almonia" 🤣🤣🤣 Dah you made my tired day
 
Upo wapi? Kama Dar jaribu kumpeleka kwa Hassanali....ana bei kubwa sana lakini yupo makini sana sana kwenye diagnosis na tiba.

Mtoto wa miezi 5 bila shaka vimeno pia vinaanza kutoka. Hii kwa uzoefu wangu ina uhusiano mkubwa na homa. Ni muda ambao mtoto anaweka vitu mdomoni (kupooza muwasho wa meno yanavyopasua fizi).

But vyovyote vile kama hakuna emergency usimpe dawa yoyote (hata panadol!) mpaka ushauriwe na daktari.
 
Kwanza pole sana, kutokujua tatizo inaumiza na kusumbua sana.
Je mtoto anatapika?

Mara nyingi viral au bacterial infection husababisha joto kupanda sana, unaweza kumpa dawa za kutuliza maumivu (Panadol au Paracetamol) akikaa hata lisaa limoja haliishi, joto linapanda tena.

Wengi wanapewa antibiotic wakifikiri wanatibu UTI au infection lakini tatizo haliishi. Kwanza usimfunike nguo ikiwezekana mwache na nepi tu pia uwe unamkanda na kitambaa cha maji baridi kushusha joto.
Akaangaliwe infection imetokea wapi, anaweza kuwa hawezi kunyonya vizuri kwa kuwa na vidonda au michubuko kwenye kinywa au aangaliwe masikioni pia.

Mungu akutangukie na apate uponyaji upesi mkuu.
Asante sana ndg yangu mwanangu kwa sasa hajambo alikuwa na U.T.I
 
Back
Top Bottom