Vipimo vya Malaria vinatofautiana? Hospitali kubwa wanasema Mgonjwa hana Malaria, tumeenda Dispensary amekutwa nayo

Teamanaconda

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
602
563
Kwanza kabsa hongereni kwa kulijenga Taifa.

Mimi nina shida moja ambayo siielewi naomba madokta mnisaidie, kuna hospital moja kubwa tu kila mwanafamilia yangu akienda kupima malaria kwenye hiyo hospital anakutwa hana malaria na wala hana ugonjwa wowote.

Wakati mimi kama mtu mzima naona kabsa huyo mwanafamilia yangu ana dalili za malaria, cha ajabu nikitoka kwenye hiyo hospital na huyo mgonjwa nikienda kwenye dispensary tu ya uchochoroni kupima anakutwa na malaria na akipewa dawa anapona.

Alianza mwanangu, msaidizi wetu,na jana nilimpeleka mke wangu majibu ni hayo hayo lakini tumeenda dispensary ya uchororoni kakutwa na malaria 3 tumepewa dawa na anaendelea vizuri, sasa naomba kuuliza kwa madokta wa humu Jf, je hivi vipimo vya malaria vipo tofauti? Maana tukiendelea hivi kuna siku hii hospital kubwa itakuja kuua mtu
 
Hapo ni maswala ya vipimo wanavyotumia,kuna hospitali vipimo wanavyotumia kama malaria ikiwa chini ya level flani haisomi,na ukienda huko ulikoenda vipimo vyao vyenyewe vinasoma malaria kwenye hiyo level na ndio maana anaonekana na malaria,ngoja waje wataalamu wa afya wenyewe wanajua mambo haya vizuri.
 
Hospitali kubwa ni nini?Ni majengo yake?Ni huduma makini yake?Ni madaktari bingwa wake?Ni wingi wa wagonjwa katika hiyo hospitali?Ni wingi wa wahudumu ambao pengine hawana utaalam wa kutosha na hawako makini?Ni ngazi ya hiyo hospitali?(Hospitali ya rufaa,etc)Ni wingi wa vifaa tiba katika hiyo hospitali?

Hospitali kubwa ni nini/ni ipi?Tupate definition na tuichambue kwanza,kwa sababu hospitali inaweza kuwa ndogo kuliko dispensary za vichochoroni halafu ikawa inaitwa ni hospitali kubwa kimakosa!
 
Mkuu kwa uelewa wangu mimi hospital kubwa kwa huku ninapoishi ni Kama hii ya Rabininsia na hii ya Kitengule,kwa wakazi wa maeneo ya Tegeta nadhani mnazifahamu,
 
Kuna vipimo vya malaria vile kama vya hiv...vile vya kupata majibu haraka haraka.. vile mara nyingi vinasema huna malaria hata kama unayo...ila vipimo vya malaria vile vya kusubiria muda kupata majibu wanaangalia kwenye microscope sijui huwa vinaonesha malaria kama unayo kweli
 
Huyu amejibu vyema na ndivyo ilivyo,
Hapo ni maswala ya vipimo wanavyotumia,kuna hospitali vipimo wanavyotumia kama malaria ikiwa chini ya level flani haisomi,na ukienda huko ulikoenda vipimo vyao vyenyewe vinasoma malaria kwenye hiyo level na ndio maana anaonekana na malaria,ngoja waje wataalamu wa afya wenyewe wanajua mambo haya vizuri...
 
nachoona mimi..

1. Inategemeana na Aina ya kipimo kinachotumika kupimia malaria. Mfano kuna Blood slide for malaria parasite au ni Malaria rapid diagnostic test (mrdt)
Kipimo cha mrdt ni antibody/antigen based hakipo na uwezo wa asilimia 100 kudetect uwepo wa mdudu wa malaria. (Sensitivity)

2. Kama ni unatumia blood slide kuangalia malaria , majibu yake pia yanategemea UTAALAMU wa kuandaa vizuri slide kabla ya kuisoma, uwezo wa MTAALAMU kusoma wadudu na kuwareport, na kureport majibu ya malaria.

3. huko uchochoroni sometimes huwa wanatumia mpaka Expired reagents, kits zilizo nje ya muda wa kufanya kazi... kupimia ambazo Kwa namna moja ama nyingine husababisha Positive results ambayo tunaita "false positive results".

4. Inaonekana ukienda hospitali unakuwa tayari na majibu yako kichwani kitu ambacho c sawa. Inaonekana unapenda positive mkuu ndo unaona hii hospitali ni nzuri.

5. huko uchochoroni sometimes wakikupa majibu Positive jumlisha na dozi ya dawa kwao wanapata faida (Kibiashara japo Kwa upande mwingine ni utoaji huduma za afya ) pia wanafanya uendelee kuwaamini, halafu hata hiyo system ya kureport malaria Kwa kutumia namba kama 1,2,3 cjui 4 ...WHO walishashauri isitumike na sehemu nyingi haitumiki lakini huko "uchochoroni " ulikosema ,bado inatumika.

6. sio kila homa ni malaria mkuu. sema unachokipata sometimes ni psychological treatment. unatibiwa kulingana na ulipolalia wewe kwamba "hii najua Tu ni malaria yangu" ...

mtaalamu sahihi si yule anaetoa majibu mengi ya Positive au mengi ya Negative ila ni Yule anaetoa majibu SAHIHI.
 
Hata mimi niliumwa sana mwaka jana nilikwenda rabininsia mara 3 hawaoni kitu ila bi mkubwa anasema hiyo malaria nilimgomea nikiamini ile hospitali kubwa bwana kuna mama akanishauri nenda toifo ni dispensary ndogo ipo njia ya kwenda tegeta kituo cha polis walinikuta na malaria na nilipoanza dose nilkapata nafuu na kupona kabisa.

Yani kuna vipimo hizi hospitali kubwa wanatumia ambavyo havitoi majibu ya kweli na wataua watu kweli.
 
Hii kitu mimi pia iliwahi kunikuta kwenye Ugonjwa wa Typhoid,Hospitali kubwa nilioenda walipima kila kitu wakasema hamna tatizo,nikashangaa nilipopima malaria kwenye maabara ndogo ya binafsi naambiwa ninayo,na nilipoanza kutumia tu dawa hali yangu ikaimarika...
 
Hata mimi niliumwa sana mwaka jana nilikwenda rabininsia mara 3 hawaoni kitu ila bi mkubwa anasema hiyo malaria nilimgomea nikiamini ile hospitali kubwa bwana kuna mama akanishauri nenda toifo ni dispensary ndogo ipo njia ya kwenda tegeta kituo cha polis walinikuta na malaria na nilipoanza dose nilkapata nafuu na kupona kabisa.

Yani kuna vipimo hizi hospitali kubwa wanatumia ambavyo havitoi majibu ya kweli na wataua watu kweli.
Mkuu hospital ni hiyo hiyo sema sikutaka kuitaja,mimi ilibidi niende dispensary ya Arafa pale Tegeta msikitini,na nimejaribu kufanya utafiti nikaona sio peke yangu anaelalamika kuhusu ili tatizo,
 
Serikali imeleta vipimo vya MRDT ambavyo kusoma ni mpaka mtu awe na Malaria nyingi...ila Dispensary nyingi hawatumii hivyo maana kwao ni hasara hivyo wanatumia B/S(Blood Smear)..yaani wanachukua kioo na wanapaka damu yako kwa kioo kuna process zinafuata kisha wanaangali kwenye microscope.

Ila pia kuna baadhi ya Dispensary hata kama huna malaria watakupa tu ili wauze dawa kua makini..unakuta dispensary kila ukienda malaria haipandi wala haishuki hata ukienda mara 10 ndani ya mwezi utaambia una malaria 2 au 3
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom