Tape measure
JF-Expert Member
- Nov 26, 2015
- 1,972
- 3,509
Wapedwa wanajukwaa, binti yangu ana umri wa mwaka mmoja na miezi mitano, alizaliwa akiwa na afya tele kwa maana hakuwa na ugojwa wowote, mama yake alifanikiwa kumnyonyesha miezi sita ya mwanzo bila kumpa chochote, alipofikisha miezi sita alianzishiwa chakula na mama yake hajaacha kumnyonyesha mpaka mda huu.
Mwanzoni mwa mwaka huu mtoto alipatwa na homa kali sana ,nilimpatia dawa za kushusha homa bila mafanikio ikabidi nimpeleke hospital kwa dakitari bingwa wa magojwa ya watoto, kufika kupimwa mtoto joto lilisoma 39.6 digree za centigred ikabidi achomwe diclofenac kwanza ndo aanze kupatiwa matibabu, Dr alimwandikia kupimwa malaria, mkojo na pia alifanyiwa full blood picture, majibu yalipotoka mtoto hakua na malaria, mkojo haukua na maambukizi, hakuonyesha maambukizi kwenye damu ila damu yake ilikua chini 10.4, niliambiwa kwa majibu yale ya vipimo kwa vyovyote japo vipimo havijaonyesha lakini lazima mtoto atakua na infection nilipewa amoxclav na pcm ,pia nilishauriwa swala la lishe ili kupandisha damu ya mtoto.
Baada ya kutumia dawa mtoto alipona ila alidumu katika hali hiyo kwa mwezi mmoja tuu, akapatwa tena na homa nikamrejesha hospital kwa Dr. Yuleyule kufika akamwandikia kupimwa malaria, mkojo na full blood picture tena, majibu kutoka hakua na infection yeyote na damu yake ilionekana kuongezeka kidogo mpaka 10.6 Dr akasema kwa homa mtoto aliyokua nayo lazima atakua na infection akamwandikia dawa ya juu zaidi third generation antibiotic siikumbuki jina, mtoto alpotumia dawa akaonekana kupona.
Leo ni kama mwezi tuu umepita tangu atumie dawa ameanza kuchemka vibaya sana, nashidwa kuelewa nifanye nini na afanyiwe vipimo gani ili ugojwa unaomusumbua malaika wangu ufaamke, napata shida kua naenda hospital na kuishia kupewa antibiotics tuu ambazo huonyesha kumtibu ila mwisho wa siku homa hurejea.
Mtoto anaonekana mwenye afya, amechangamka, hana mafua wala kikohozi.
Msaada kwenu wanajukwaa maana ili jambo linaonekena kua ni changamoto sasa.
Natanguliza shukurani.
Sent from my OPPO A57 using JamiiForums mobile app