Wazazi waonesha cheti cha kuzaliwa mtoto wao anaitwa FISTON MAYELE, wakutana na MAYELE original wapiga naye picha

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,300
5,434
1d8bb421-1f18-4832-bc2b-8673a562bb64.jpg

025d21b3-72cd-4f4b-a352-81d82d655280.jpg


Familia moja Jijini Mwanza imeonesha jinsi ilivyo na mahaba na mshambuliaji Fiston Mayele wa Klabu ya Yanga, baada ya kumpa jina mtoto wao linaloendana na mchezaji huyo raia wa DR Congo.

Kwa ufupi ni kuwa mtoto huyo naye anaitwa Fiston Mayele, siyo kwamba ni jina la utani, HAPANA, ni jina hali halisi.

Mashabiki hao wakiwa na cheti halisi cha jina la mtoto huyo kinachosomeka Fiston Mayele walionesha hadharani na pia wakapata nafasi ya kukutana na Mayele mwenyewe original kisha kupiga naye picha na kumbeba mtoto huyo.

Mayele alikuwa Mwanza pamoja na timu yake ambapo walicheza mechi dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mei 28, 2022.

Mama mzazi anaitwa Sundi John Kalumbi wakati jina la baba mtu ni Victor Maguta Ndulu, wakazi wa Nyamagana. Mtoto huyo alizaliwa Januari 17, 2022.
 
wangemvua mtoto kofia ili aonekane vzuri. Akiwa mkubwa aje ateteme kama mayelle
 
Angemuita jina mojawapo kati ya Fiston au mayele. Hii itakuja kuleta shida mtoto majina yakianza kutumika kwenye mfumo wa majina 3, au mayele akikorofishana na timu au akitimkia simba
 
Angemuita jina mojawapo kati ya Fiston au mayele. Hii itakuja kuleta shida mtoto majina yakianza kutumika kwenye mfumo wa majina 3, au mayele akikorofishana na timu au akitimkia simba
Mfumo wa majina matatu ndio upi huo? Mtanzania anatumia majina yake yote aliyosajili.

Ukiwaona, Ramadhani, Mwinshehe Ditopile Mzuzuri.
 
Kwa wanaofahamu Waarabu Huwa Wana majina mara mbili Mbili ingawa si Wote, utasikia Kuna Fulani bin Fulani au pia ujurikana kama Fulani bin Fulani.
Kwa hiyo huyo msukuma hapo ni mwarabu?

Umeona habari kabisa hapo imeeleza hilo jina limeandikwa official kwenye birth certificate na bado unaona hiyo ni sawa na bin fulani bin fulani?

Mi naona tu hii ni nature ya mashabiki wa Yanga kutoweza dhibiti hisia zao wanapo face nyakati za furaha na kujikuta wamefanya maamuzi ambayo ya ajabu au hadi pengine kufikia hatua kujidharilishia utu wao

 
Back
Top Bottom