Mtoto afichua siri nzito. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto afichua siri nzito.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ZENITH, Apr 25, 2012.

 1. ZENITH

  ZENITH JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 732
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 60
  Nikiwa njiani kurudi ofisini nilikutana na umati mkubwa wa watu wakilifuata kwa nyuma gari la polisi.Hii ilikuwa maeneo ya Ifunda-iringa.Polisi pamoja na umati wote huu walikuwa wametoka kufukua kaburi la mtu aliyezikwa kwa siri kwenye shamba la migomba miaka mitatu iliyopita. Watuhumiwa wakuu wa haya mauaji ni mke wa marehemu pamoja na kaka wa marehemu.

  Inasemekana aliyetoa hii siri ni mtoto mdogo wa miaka mitano na nusu ambaye anasema aliyashuhudia haya mauaji na aliona pale mwili wa baba yake ulipofukiwa.Mauaji haya yalitokana na tamaa na wivu wa kaka mtu kutokana na eneo la mdogo wake kutumiwa na makampuni ya simu kujenga minara. Mdogo wake akawa akipata donge nono kila mwisho wa mwezi kutoka makampuni haya.Kaka mtu akamshauri shemeji yake wamtoe uhai mumewe.

  Baada ya mauaji kufanyika na kumzika kisirisiri mumewe,kaka mtu akaanza kuishi na shemejiye kama mke na mume na kuendelea kuzifaidi pesa za makampuni ya minara ya simu. Baada ya kupita siku nyingi bila kumuona mume wa huyu mama,watu walimhoji huyu mama wasipate jibu la kueleweka. Kilichowastua na kuwapa mashaka ni malalamiko ya mtoto mdogo wa familia akinung'unika kwa kusema,"mama alimuua baba na kumfukia migombani usiku".Haya maneno yaliwashawishi majirani kuwaita polisi na kwenda pamoja na yule mtoto pale migombani na hatimaye kufanikiwa kufukua mifupa inayosadikika kuwa ya binadamu.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Imekula kwao hao,USD 500 za kila mwezi zimewatoa roho.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Motive ya mauaji ilikuwa mapenzi ama hela za minara ya simu?
  Manake kama ni hela hakukuwa na sababu ya mama kumuua mumewe ili akafaidi hela na shemeji yake tena kwa kuishi nae same house.
   
 4. B

  Bi. Mkora JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Unamtoa roho mdogo wako kwa ajili ya pesa? Na mke anashiriki kumuua mumewe? Mwe kama kuna kujibu kwa mungu sijui watu kama tutaweza kujibu huko.
   
 5. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,078
  Trophy Points: 280
  duh hii kali, wacha akakutane na pilato
   
 6. ZENITH

  ZENITH JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 732
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 60
  Mi nahisi pia hawa watu walikuwa ni wapenzi toka enzi za uhai wa marehemu.
   
 7. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Si wote na msinimind ila nilishawahi kuachiwa wosia huu...Mwanangu usimwamini mwanamke hata kwa dakika moja...

  A thread like this bring a very bad memory to some pipo.
   
 8. ZENITH

  ZENITH JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 732
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 60
  Hii inanipa hofu sana kuhusu hawa akina eva!
   
 9. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Bibilia inasema muishi na wanawake kwa akili!!
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,253
  Trophy Points: 280
  Too sad....
  umuue nduguyo, umpore mali zake na mke wake ujimilikishe.
  Kweli siku za mwisho watu watakuwa wenye kupenda fedha na upendo wa wengi utapoa
   
 11. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukistaajabu ya musa,utayaona ya firauni.!!!!
   
 12. roby2006

  roby2006 JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 399
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa haya mambo hawawezi kuyapanga juu kwa juu tu halafu wakaelewana lazima walikuwa faragha,hii ndio tabu ya kutokuwa na hofu ya Mungu
   
 13. k

  kisukari JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,763
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  mwanamke akiwa na roho mbaya,ni zaidi ya mnyama.na alikuwa anaishi bila kuji feel guilty.inasikitisha kwa kweli
   
 14. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #14
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Jamani mtoto alindwe na ndugu maana ndio.shahidi mkuu wa mauaji na ndio damu pekee ya marehemu kwani hawa wauaji wanawashana km kawa watajapata mtoto wamuone halali
   
 15. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Woman! Anyway, tukumbuke EDEN, lakini tuwapende.
   
 16. s

  sugi JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  lazima walikuwa na u husiano tu,asingeweza kushawishika kama angekuwa na mapenzi ya dhati kwa mumewe,wanawake wanawakeee,mtatumaliza sasa,heeee!na Kanumba mlituulia hivi hivi
   
 17. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mbaya sana hiyo! Tamaa gani hiyo ya pesa hadi utoe uhai wa mtu?
   
 18. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,309
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Utawajua tuu wanaosoma biblia mstari mmoja kwa miaka 3.
   
 19. aye

  aye JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,989
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  kweli duniani hakuna siri
   
 20. M

  Mboerap Senior Member

  #20
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wala usihisi hio minara sijui na nini inasehem ndogo sana ya mauaji haya. Ni kama 1% tu.ishu hapa ilikua ni uzinzi tu.ni dhahiri walikua wanaibana toka siku nyingi na ilipowakolea wakamwona marehem anawawekea night ndipo mipango ilipoanza
   
Loading...