Mtoto afichua siri nzito.

Mtoto afichua siri nzito.

Wakubwa, kuna kitu sijakielewa hapa. Huyo mtoto alikuwa na miaka mitano na nusu wakati baba yake anauawa (3 years ago) au sasa ndo ana umri huo?
 
Wakubwa, kuna kitu sijakielewa hapa. Huyo mtoto alikuwa na miaka mitano na nusu wakati baba yake anauawa (3 years ago) au sasa ndo ana umri huo?

hata mimi nashangaa..kama sasa hivi ndo ana miaka 5 na nusu that means enzi hizo alikua na miaka 2 na nusu is it possible akumbuke hilo tukio kweli??
 
Wakubwa, kuna kitu sijakielewa hapa. Huyo mtoto alikuwa na miaka mitano na nusu wakati baba yake anauawa (3 years ago) au sasa ndo ana umri huo?
Huyu jamaa aliyenipa dondoo hizi alinambia kwamba huyu mtoto kwa sasa ana umri huo wa miaka mi5.5,lakini kwa sababu yeye si mzazi wa huyu mtoto,sina uhakika sana kuhusu umri alionitajia.
 
Wakubwa, kuna kitu sijakielewa hapa. Huyo mtoto alikuwa na miaka mitano na nusu wakati baba yake anauawa (3 years ago) au sasa ndo ana umri huo?

You know what mkuu, Lies have short legs!
 
Nikiwa njiani kurudi ofisini nilikutana na umati mkubwa wa watu wakilifuata kwa nyuma gari la polisi.Hii ilikuwa maeneo ya Ifunda-iringa.Polisi pamoja na umati wote huu walikuwa wametoka kufukua kaburi la mtu aliyezikwa kwa siri kwenye shamba la migomba miaka mitatu iliyopita. Watuhumiwa wakuu wa haya mauaji ni mke wa marehemu pamoja na kaka wa marehemu.

Inasemekana aliyetoa hii siri ni mtoto mdogo wa miaka mitano na nusu ambaye anasema aliyashuhudia haya mauaji na aliona pale mwili wa baba yake ulipofukiwa.Mauaji haya yalitokana na tamaa na wivu wa kaka mtu kutokana na eneo la mdogo wake kutumiwa na makampuni ya simu kujenga minara. Mdogo wake akawa akipata donge nono kila mwisho wa mwezi kutoka makampuni haya.Kaka mtu akamshauri shemeji yake wamtoe uhai mumewe.

Baada ya mauaji kufanyika na kumzika kisirisiri mumewe,kaka mtu akaanza kuishi na shemejiye kama mke na mume na kuendelea kuzifaidi pesa za makampuni ya minara ya simu. Baada ya kupita siku nyingi bila kumuona mume wa huyu mama,watu walimhoji huyu mama wasipate jibu la kueleweka. Kilichowastua na kuwapa mashaka ni malalamiko ya mtoto mdogo wa familia akinung'unika kwa kusema,"mama alimuua baba na kumfukia migombani usiku".Haya maneno yaliwashawishi majirani kuwaita polisi na kwenda pamoja na yule mtoto pale migombani na hatimaye kufanikiwa kufukua mifupa inayosadikika kuwa ya binadamu.

Hawa ni wa kabila gani? Kuna wanawake wengine hovyo kweli! Huyu mwanamke anathubutu kumwua mumewe kweli?
 
Hawa ni wa kabila gani? Kuna wanawake wengine hovyo kweli! Huyu mwanamke anathubutu kumwua mumewe kweli?

Jamani, mbona mnapenda kulalamika sana kuhusu wanawake? Huyu mleta hii fiction, anadai marehemu aliuwawa kwa ushirikiano wa mke wa marehemu pamoja na shemeji yake (kaka wa marehemu), jinsia mbili zilishiriki - ME na KE. Why blame a woman?
 
Na vyombo vya usalama vi wapi?, tuendelee kupashana kama vyombo vilikuwa vimefanya uchunguzi ama vilifurahia kuona wazinzi cum wauaji wawili wakisherehekea kifo cha muungwana?
 
hata mimi nashangaa..kama sasa hivi ndo ana miaka 5 na nusu that means enzi hizo alikua na miaka 2 na nusu is it possible akumbuke hilo tukio kweli??

Mtoto wa miaka miwili anaweza kukumbuka, kwani wewe hukumbuki chochote kilichotokea wakati ukiwa na miaka miwili?!, basi wewe utakuwa zoba.
 
Back
Top Bottom