Mtoto afariki kwa kukosa matibabu Wazazi waliamini nguvu ya Maombi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Laela A, Ruti Sikapita amefariki dunia baada ya wazazi wake kukataa kumpeleka hospitali kwamadai kuwa imani ya dhehebu lao haliruhusu waumini wake kutibiwa hospitali.

Tukio hilo lilitokea Machi 17 baada ya mtoto huyo kuugua kwa siku tatuhuku akiwa anafungiwa ndani na baba yake Cossam Sikapita, akidai kuwahawataki aende hospitali kupatiwa matibabu kwani kwa kufanya hivyo angekuwa ametenda dhambi kwani dini hairuhusu kutibiwa na dawa za hospitali.

Soma zaidi:Mtoto afariki kwa kukosa matibabu, wazazi waliamini maombi pekee
 
Sasa si aliandikiwa kufa kifo hicho?? Hospitali ingesaidia nini ka majirani waliruhusu upuuzi huo kuendelea? RC kamata wote hadi jirani, sweka ndani masaa 48 vyumba vilivyowekwa maji baridiiiiiii
 
huu ni ujinga! sana! kuna baadhi ya madhehubu ya kikristo yana viroja mno
 
SILOAM hao!!
Kuna dada alifiwa na mwanae wapekee kwa imani yao hiyo mtoto anaumwa malaria ye anapiga maombi
tiba yao nikummwagia mgonjwa maji na kumfunika magazeti ya kanisa.
 
Sasa si aliandikiwa kufa kifo hicho?? Hospitali ingesaidia nini ka majirani waliruhusu upuuzi huo kuendelea? RC kamata wote hadi jirani, sweka ndani masaa 48 vyumba vilivyowekwa maji baridiiiiiii
Huko kwako jirani anakuja kukuamulia mambo yako.
 
Ni nyakati ambazo tuna shule nyingi lakini hatuna elimu. Kuna wapo wapo radhi kabisa kutembea uchi na kula kinyesi "nabii" wao akisema.
 
91b325e2b97d0ec8f8ccfcf4f2c842a6.jpg

Hii inawahusu hao wazazi wajinga!!!
 
Huko kwako jirani anakuja kukuamulia mambo yako.

Molembe;
Hivi jirani yako weye nnani? Hata aliyeandika uzi huu weka ndani. Alitakiwa aripoti polisi kumsaidia mtoto si ungojee kafariki uje jf kutangaza mpaka sababu ya kifo. Si haki, jirani kazi yake ni kuwasemea wasoweza kujisemea.
 
Jirani anaweza kuwa hajui kinachoendelea ndani mwako.
 
Kuna makanisa yalitakiwa yafutwe usajili kisha wapelekwe mbele ya sheria kwakuposha waumini wao. Coz Mungu kamwe haponyi ugonjwa ambao tiba yake iko chini uwezo wa kibinadamu.
 
Back
Top Bottom