Hizi ni kingo za Mto Mara (Rorya). Ukiupita Mto Mara hutajua kuwa unaweza kuua bustani ya mtu. Huu weupe ni Chumvi. Chumvi hii inabebwa na mto toka unakoanzia hadi ziwa Victoria. Kutumia maji haya kwa kilimo kama bustani inabidi kuchukua tahadhari ya kupambana na maji haya vinginevyo kimzahamzaha miaka michache utajikuta bustani haifai
Mto Mara unaanzia misitu ya Mau huko Kenya. Hii chumvi ni kutokana na virutubisho vya udongo. Tatizo ni kwamba kwenye maeneo ya tambare na joto huwa hii chumvi inaonekana kiurahisi baada ya maji ya ukingoni kukauka