Mtikisiko wa uchumi duniani-2 unanukia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikisiko wa uchumi duniani-2 unanukia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPIGA ZEZE, Jul 17, 2011.

 1. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Na hili ni swali la papo kwa papo kwa Mhe waziri Mkuu, Dkt Kayanza Pinda.
  Zama za kale wahenga walinena kwamba ‘ngoma ikipigwa Unguja, Bara hucheza’ (enzi zile za utawala wa Waarabu, Unguja ndicho kilikuwa kitovu cha utawala na uchumi). Hapana ubishi, zama hizi za leo tunaishi katika dunia tandawazi. Tanzania haiwezi kujidanganya kuwa ni kisiwa, na mintaarafu ukweli huu ni kwamba ‘ngoma ikipigwa Washington, DC, dunia nzima hucheza!’ Huko DC moto unawaka. Janga la kiuchumi la kutengenezwa liko jikoni. Wademokrati na Warepablikani wameshikana koo juu ya kupandisha ‘paa la deni la taifa’ (national debt ceilling). Wasipoafikiana ifikapo Agosti 2, 2011 wataalamu wa uchumi na siasa wanatabiri kwamba taifa la Marekani litakumbwa tena na mporomoko mkali wa kiuchumi kuliko hata ule wa 2008. Na Marekani ikiyumba, dunia nzima inayumba – mtikisiko wa pili wa kiuchumi duniani katika kipindi kisichozidi miaka mitano. Serikali za majimbo ya Marekani zimeanza kuchukua tahadhari iwapo janga hili litatokea.
  Swali: je serikali yetu ya JMT ina habari kuhusu uwezekano wa kutokea janga hili? Kama jibu ni ndiyo, imechukua hatua gani za tahadhari? Na imeundaaje umma angaa kihisia iwapo janga litatokea? AU tunasubiri mtikisiko utokee halafu tuunde TUME?
   
 2. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh...wachukue hatua gani vilaza hawa,wanachowaza ni kushibisha matumbo yao tu!Watakuja na 'Stimulus package' tena.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Kikwete wala hajui kuwa mporomoko wa uchumi umekaribia.
   
 4. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hakuna la kuchukuliwa hatua kwani uchumi wetu unakuwa vizuri sana kwa 7.pinda huyo
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Recession mkuu haiwezi kutokea kwasasa hivi kwasababu USA jana walishakubaliana kuongeza NAtional Debt Ceiling . Fununu zinasemekana mjadala kwasasa uko katika lini wataanza kupunguza matumizi ya serikali. Tishio la uchumi liko bara la ulaya kwasababu ni mkusanyo wa nchi mbali mbali zilizofilisika. Inasemekana Italy na Spain wanafuatia baada ya Greece, Ireland na Ureno. So far Ireland ndio wanaofanya vizuri kuliko wote ila kama zitafilisika nchi za Italy na Spain, Ireland nao watazama na maji na mtikisiko wake utahamia dunia nzima kwasababu utandawazi wa sekta ya benki.

  Pia nchi hizi zikifilisika misaada hatupati kwasababu ndio wafadhili wakuu wa Donor Fund Budget support. Swali serikali yetu inahabari hiyo?
   
Loading...