Mtikila: Viongozi wa dini wanafiki

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,780
3,227
na Andrew Chale

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameponda hatua ya ujumbe wa viongozi wa dini nchini kumtaka Dk. Willibrod Slaa, kukubali matokeo ya kushindwa kwenye uchaguzi wa rais uliomalizika hivi karibini na kuwafananisha na Yuda Eskalioti, aliyepewa vipande 30 vya fedha kisha kumsaliti Yesu.

Mtikila aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akiongea na Tanzania Daima, akidai kuwa, kitendo hicho ni cha kinafki, kwani viongozi hao hawakupaswa kumfuata Dk. Slaa na ujumbe wao huo wa kumtaka akubali matokeo ili kulinusuru taifa na machafuko ya kisiasa.

Badala yake aliwataka viongozi hao wangeanza kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Rais Kikwete ili kuona hatua ya kufuata ili kuzuia mpasuko uliopo sasa nchini.

“Tume imekubali kuwa kulikuwa na makosa mbalimbali kwenye uchaguzi na watayafanyia kazi ili yasitokee tena, vivyo hivyo walitakiwa kumfuata na Rais Kikwete ili kumuona angesemaje juu ya hatua hiyo ya Dk. Slaa, lakini kwa kitendo cha kwenda kwa Dk. Slaa sasa ni cha kinafki na ndio wanaoifanya dini kama mradi wa kuficha maovu,” alisema Mtikila. Akinukuu vifungu vya Biblia, kikiwamo cha Tito 2:11, Waraka wa pili wa Timotheo 4:2, ambavyo vyote vinalaani na kukemea machafuko na dhuluma kwa wanadamu, Mtikila alisema kuwa viongozi wa dini wameafiki hali ya uchakachuaji uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuiba kura za wananchi na kudhani ni za Dk. Slaa.

“Kilichotakiwa kufanywa na viongozi hawa wa dini kama wanaona kuna machafuko, walitakiwa wagome kwa pamoja hatua ya kuapishwa kwa rais na kudai maridhiano ya pamoja. Lakini wao waliafiki moja kwa moja kwa kukubali kupewa vipande 30 vya fedha kama Yuda na kisha kumsaliti Yesu,” alisema Mtikila.

Aidha, Mtikila alikubaliana na hatua hiyo ya Dk. Slaa kuyakataa matokeo hayo yaliyochakachuliwa, kwani ni kitendo cha dhahiri, anasimamia masilahi ya taifa ambalo lilimchagua ili awakomboe.

“Kura zilizoibwa na CCM ni za wananchi wote wa Tanzania wanaopenda mageuzi ya kweli, waliochoka na manyanyaso na masuala ya ufisadi, ijulikane hawakumuibia Dk. Slaa ambaye kura yake ni moja tu,” alimalizia Mtikila.

Alisema kuwa kama ingekuwa ni wahuni tu wanamfuata Dk. Slaa na kumtaka akubali matokeo, tungesema wameshalewa madawa, lakini viongozi wa dini ambao ni taswira kwenye taifa ni jambo la kushangaza, halitavumiliwa kamwe na lisifumbiwe macho,” alisema Mtikila.

Pia aliweza kutolea mfano juu ya nchi mbalimbali ambazo viongozi wa dini waliamua kupambana waziwazi ili kulinda hali ya amani, ikiwemo kutoa ushawishi mkubwa wa kupatikana haki ya msingi, ambapo ushawishi wao ulisaidia kufanikisha baadhi ya mambo.

Mtikila alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na maaskofu wa nchi ya Afrika Kusini, waliokuwa upande wa watu walioonewa wa vyama vya ANC na PNC, kwa Malawi viongozi wa dini 16 waliamua kwa pamoja kumpinga Rais Banda. Hivyo hivyo ilifanyika katika nchi za Ukraine, Thailand na Kenya, ambao walikuwa na machafuko makubwa.
 
Mpinzani wa kweli!!! genius Mtikila

Slaa hupo?? tukitaka tuamini kuwa wewe ni 'wakweli' basi hakuna kukaa kimya!! huu ukimya unaleta maswali mengi,

mnaendela kama kawaida na shuguli za kiserikali na mmeshateua wabunge n.k ijumaa mko mjengoni, HIVI kukataa matokeo kunaendana na nini?? si kuzira shughuli zote za kiserikali??

amsheni watu, amsheni ulimwengu, watu wajue kuna chama kinaitwa chadema, chama cha kweli cha upinzani, na sio kuburuzwa kama CUF !!!

Tunasubiri kabla hatujatoa matamko yetu ya ndani kabisa

Mtikila hupo?? aha! aha! aha! kweli ukubwa jiwe!
 
MTIKILA ANAJULIKANA, SIO MWANADEMOKRASIA

1. NI MSEMA OVYO
2. DOMO JALALA
3. I would not any view of Reverand Mtikila Serious

He is always there seeking for cheap popularity
 
Rev. Mtikila siku zote 71 za kampeni mbona hakusikika kabisa au vyombo vya habari vilimsusa? Comments zake zina mantiki, kumtuliza mtendewa bila kuwakemea watendaji ilikuwa haina maana
 
mtikila ni mchemfu
 
Mpinzani wa kweli!!! genius Mtikila

Slaa hupo?? tukitaka tuamini kuwa wewe ni 'wakweli' basi hakuna kukaa kimya!! huu ukimya unaleta maswali mengi,

mnaendela kama kawaida na shuguli za kiserikali na mmeshateua wabunge n.k ijumaa mko mjengoni, HIVI kukataa matokeo kunaendana na nini?? si kuzira shughuli zote za kiserikali??

amsheni watu, amsheni ulimwengu, watu wajue kuna chama kinaitwa chadema, chama cha kweli cha upinzani, na sio kuburuzwa kama CUF !!!

Tunasubiri kabla hatujatoa matamko yetu ya ndani kabisa

Mtikila hupo?? aha! aha! aha! kweli ukubwa jiwe!

TATZO LETU NI KUTAKA KUFANYIWA KILA KITU NA WENGI ETU KUTAKA KUBAKI SPECTATORS. KUANZSHA NA KUJIUNGA NA VYAMA VYA SIASA NI HIARI YA MTU/WATU. HIVYO KAMA MTU/WATU WANAONA KUWA MAZINGIRA YA TANZANIA HAYAWAFAI WAO KUFANYA SIASA WANA HIARI YA KUTOSHIRIKI SIASA HIZI ZA KINAFIKI. NDIO MAAN IDADI KUBWA YA WATANZANIA WANABAKI PASSIVE, HAWAJADILI, HAWACHANGII NA WALA HAWATAKI HATA KUPIGA KURA.

HALI HII NI VERY CONDUCIVE KWA CCM, KWANI WANAWEZA KUENDELEA KUTAWALA ENDLESSLY. NDIO MAANA WANAMAGEUIZ WACHACHE WAKAAMUA KUANZISHA VYAMA VYA MBADALA LICHA YA MAPUNGUFU YOTE YALIYOPO. NDIO MAANA NA SISI WENGINE TUKAHAMISIKA KUJINUGA NA GURUDUMU LA KUDAI MABADILIKO. CHA KUSHANGAZA NI PALE MTU ANATAKA MABADILIKO LAKINI HAYUKO TAYARI HATA KUFUTA TONGO TONGO MACHONO MWAKE KILA KITU ANATAKA DR SLAA AFANYE, MBOWE AFANYE, CHADEMA IFANYE N.K. KWANINI TUSIJIULIZE SISI TUMEFANYA NINI KURA ZETU ZILIPOIBIWA?

NAUNGANA NA MTIKILA AKISEMA KUWA KURA HIZO NI ZA WANANCHI NA SIO ZA DR SLAA, KWANI HATA FEDHA ZILIZOTUMIKA KUGHARIMIA UCHAGUZI HUU SI ZA DR SLAA NI ZA UMMA YAANI WATANZANIA WOTE. HIVI KAMA MWAKA 2005 BUNGE LA CHADEMA LA WATU 11 LINGEZIRA SHUGHULI ZA SERIKALI LEO HII TUNGEKUWA NA NINI CHA KUJIVUNIA?. UKIZIRA SISI TWALA NDIO KITAKACHOFANYIKA KWA KUWA IDADI YA CCM INATOSHA KORAMA YA BUNGE KUENDELEA.

UNAPOSEMA AMSHENI WATU, SIJUI UMA MAAN GANI? WEWE BAADA YA KURA YAKO KIIBIWA UMESHAMSHA WANGAPI?

"Tunasubiri kabla hatujatoa matamko yetu ya ndani kabisa" KAMA HUWEZI KUGOMBEA HAKI YAKO YA KURA YAKO KUIBIWA HATA UKITOA MATAMKO YA NDANI NDIO YALE MHE JAKAYA KIKWETE ALISEMA HAYAMNYIMI USINGIZI. LAKINI UKITAKA KUINYIMA CCM NA KIKWETE USINGIZI JIUNGE NA CHADEMA HAMASISHA KUFUNGUA MATAWI, HAMASISHA WATU KUJINUGA NA CHADEAMA BADALA YA KUSUBIRI UCHAGUZI WA MWAKA 2015 TUKIWA WANYONGE KWANI SIASA ITABAKI KUWA NI WATU, NA MWENYE WATU NDIO ANAYEWEZA KUFANYA SIASA.

MWAKA 2010 CHADEMA ILIKUWA IKUNGWA MKONO SANA NA WATU AMBAO BADO HAWAJAJITANABAISHA NA CHAMA KAMA AMBAVYO WANACCM WAMEFANYA.
 
Mtu akizungumza point tumpongeze hata kama huko nyuma aliwahi kuzungumza pumba au kuropoka kama mchangiaji mmoja alivyoandika.

Mimi naungana na Mtikila kwamba viongozi wa DINI wamejaa unafiki mkubwa, badala ya kutafuta namna ya kutatua tatizo wanataka kulipoza kwa kumuomba aliyeibiwa kura akubali kuibiwa. DINI zetu zimekuwa za kuwatukuza wenye fedha na kuwaacha masikini wakionewa na kudhulumiwa bila huruma.
 
Huyu mdau ana chuki na Dr. Slaa, wala usiumize kichwa kumuandikia, atakusoma lakini atarudi pale pale, hawezi kumaliza post yake bila kumtaja Dr. Slaa.
 
Ukiondoa ishu zake za blackmailing. Mtikila ni mpinzani wa kweli na anaongea point kila apatapo nafasi.
Unafiki wa viongozi wa dini utaiingiza nchi kwenye machafuko yes
 
Mtu akizungumza point tumpongeze hata kama huko nyuma aliwahi kuzungumza pumba au kuropoka kama mchangiaji mmoja alivyoandika.

Mimi naungana na Mtikila kwamba viongozi wa DINI wamejaa unafiki mkubwa, badala ya kutafuta namna ya kutatua tatizo wanataka kulipoza kwa kumuomba aliyeibiwa kura akubali kuibiwa. DINI zetu zimekuwa za kuwatukuza wenye fedha na kuwaacha masikini wakionewa na kudhulumiwa bila huruma.

Safi sana Saharavoice, naungana na wewe kuwa ktk point chache ambazo mtikila kaongea hii ni moja wapo. Hawa viongozi wa dini ni part and parcel ya wizi wa kura, tena wao ndio wabaya zaidi kuliko ccm na nec maana hawa wamejificha kwenye mgongo wa dini.

Viongozi wa dini walijua mpango wa ccm kuiba kura lakini badala ya kwenda kuwaonya nec na ccm wakatembelea ofisi za CHADEMA kumwomba Slaa awe tayari kukubali matokeo ya aina yoyote ile. (mashetani wakubwa) Walipoona tayari wizi umefanyika wanajifanya wana uchungu na amani ya nchi hii, eti badala ya kusherehekea na wezi wenzao ccm na nec wanaelekea ofisi za CHADEMA kumwomba Slaa akubali matokeo kama vile kura za Slaa alijipigia mwenyewe kumbe ni wananchi tumempigia. (wanafiki wakubwa) Anachotakiwa kufanya Slaa ni kutamka kile ambacho kiko ktk akili za watu wengi kuwa kura zimeibwa hivyo uchaguzi umechafuliwa, na uchaguzi mchafu hauwezi kutoa rais wa jamhuri ya muungano. Akisema hivyo yeye amemaliza, hilo suala la amani ni la wananchi wenyewe. ukizingatia amani yenyewe haipo ila kuna utulivu ambao umetokana na hofu waliyojengewa wananchi, ujinga wa wananchi, kiwango duni cha elimu na wananchi wengi kutojua maana ya amani.
 
Anachosema MTIKILA sawa lakini sina haja ya kuumiza kichwa na habari zake sio msafi. Huyu Bwana anafadhiliwa na Manji, alichukua fadha mil. 3 kwa RA na madeni mengi ya wahindi ambao siku za nyuma alikuwa anataka na kupandisha jazba kuwa ni MA********* wasiostahili kuishi TZ.
 
MTIKILA ANAJULIKANA, SIO MWANADEMOKRASIA

1. NI MSEMA OVYO
2. DOMO JALALA
3. I would not any view of Reverand Mtikila Serious

He is always there seeking for cheap popularity
Hon. Makame ,
Read this very article , then comment about it. Forget about the Mtikila you know. Itakusaidia kujikita kujadili hoja badala ya watu.
 
TATZO LETU NI KUTAKA KUFANYIWA KILA KITU NA WENGI ETU KUTAKA KUBAKI SPECTATORS. KUANZSHA NA KUJIUNGA NA VYAMA VYA SIASA NI HIARI YA MTU/WATU. HIVYO KAMA MTU/WATU WANAONA KUWA MAZINGIRA YA TANZANIA HAYAWAFAI WAO KUFANYA SIASA WANA HIARI YA KUTOSHIRIKI SIASA HIZI ZA KINAFIKI. NDIO MAAN IDADI KUBWA YA WATANZANIA WANABAKI PASSIVE, HAWAJADILI, HAWACHANGII NA WALA HAWATAKI HATA KUPIGA KURA.

HALI HII NI VERY CONDUCIVE KWA CCM, KWANI WANAWEZA KUENDELEA KUTAWALA ENDLESSLY. NDIO MAANA WANAMAGEUIZ WACHACHE WAKAAMUA KUANZISHA VYAMA VYA MBADALA LICHA YA MAPUNGUFU YOTE YALIYOPO. NDIO MAANA NA SISI WENGINE TUKAHAMISIKA KUJINUGA NA GURUDUMU LA KUDAI MABADILIKO. CHA KUSHANGAZA NI PALE MTU ANATAKA MABADILIKO LAKINI HAYUKO TAYARI HATA KUFUTA TONGO TONGO MACHONO MWAKE KILA KITU ANATAKA DR SLAA AFANYE, MBOWE AFANYE, CHADEMA IFANYE N.K. KWANINI TUSIJIULIZE SISI TUMEFANYA NINI KURA ZETU ZILIPOIBIWA?

NAUNGANA NA MTIKILA AKISEMA KUWA KURA HIZO NI ZA WANANCHI NA SIO ZA DR SLAA, KWANI HATA FEDHA ZILIZOTUMIKA KUGHARIMIA UCHAGUZI HUU SI ZA DR SLAA NI ZA UMMA YAANI WATANZANIA WOTE. HIVI KAMA MWAKA 2005 BUNGE LA CHADEMA LA WATU 11 LINGEZIRA SHUGHULI ZA SERIKALI LEO HII TUNGEKUWA NA NINI CHA KUJIVUNIA?. UKIZIRA SISI TWALA NDIO KITAKACHOFANYIKA KWA KUWA IDADI YA CCM INATOSHA KORAMA YA BUNGE KUENDELEA.

UNAPOSEMA AMSHENI WATU, SIJUI UMA MAAN GANI? WEWE BAADA YA KURA YAKO KIIBIWA UMESHAMSHA WANGAPI?

"Tunasubiri kabla hatujatoa matamko yetu ya ndani kabisa" KAMA HUWEZI KUGOMBEA HAKI YAKO YA KURA YAKO KUIBIWA HATA UKITOA MATAMKO YA NDANI NDIO YALE MHE JAKAYA KIKWETE ALISEMA HAYAMNYIMI USINGIZI. LAKINI UKITAKA KUINYIMA CCM NA KIKWETE USINGIZI JIUNGE NA CHADEMA HAMASISHA KUFUNGUA MATAWI, HAMASISHA WATU KUJINUGA NA CHADEAMA BADALA YA KUSUBIRI UCHAGUZI WA MWAKA 2015 TUKIWA WANYONGE KWANI SIASA ITABAKI KUWA NI WATU, NA MWENYE WATU NDIO ANAYEWEZA KUFANYA SIASA.

MWAKA 2010 CHADEMA ILIKUWA IKUNGWA MKONO SANA NA WATU AMBAO BADO HAWAJAJITANABAISHA NA CHAMA KAMA AMBAVYO WANACCM WAMEFANYA.
Mkuu wangu huwa nakukubali sana. Ninashawishika kukubaliana na kila uliloliandika hapo juu. Mungu akubariki na kukupa afya ili ufikie kusudio jema la makusudi yako kwa Chadema. Asante sana.
 
Hon. Makame ,
Read this very article , then comment about it. Forget about the Mtikila you know. Itakusaidia kujikita kujadili hoja badala ya watu.
Udini umemtangulia huyo. Hawezi kukusikiliza wala kukuelewa. Labda kama lingezungumzwa na Sheik!
 
mtikila anajulikana, sio mwanademokrasia

1. Ni msema ovyo
2. Domo jalala
3. I would not any view of reverand mtikila serious

he is always there seeking for cheap popularity
lets not be biased, the guy has spoken points no matter if he is mtikila, or even if these things were spoken by mwendawazimu. The fact remains they are absolutely correct, so lets give credit where its due well done mtikila for speaking the truth
 
Mtikila nae ni great thinker maana huwa anaingia na Kibajaji pale Kisutu.

Halafu nusura afungwe kwa kumdhulumu mwalimu wa shule ya msingi hahaha
 
Naunga mkono kauli ya Mchungaji Mtikila, hata jana nilitoa post moja juu ya unafiki wa viongozi wa dini hasa wakristo. Ni wanafiki , ni waoga, ni walamba viatu vya watawala. Hapa mkosaji ni CCM na NEC kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola wamevuruga uchaguzi kwa kuchakachua kura na kumtangaza JK kuwa ameshinda ilhali yeye ndiye ameshindwa.Dr Slaa anataka kusimamia haki ya Watanzania wote ambao fedha yao imetumika kufanya uchaguzi ambao kwa makusudi mazima umeharibiwa ili kumbeba JK.LAZIMA WAHALIFU WAWAJIBIKE KWA UHALIFU WAO NA SIYO KUBEMBELEZWA,
 
He is looking for popularity!!! He won wonderful cases against the GVT,yes he is popular,for he has always stood for TRUTH AND JUSTICE. Truth is always popular.Do you believe lies are more popular than truth? Aseme nini wakati ni kweli matokeo na kura za wananchi zimechakachuliwa? Je si busara viongozi waa dini wakakemea hali hii? waoga au wanafiki au yote hayo. Sasa anasema tuanze kufanya reconciliation is that a bad thing, even JK has stated the same.
Then how do you see him?!! A mnafiki au mkweli ,mpenda amani na umoja? Angalia hoja yako isiyo na kigezo cha kusimamia!!
 
Back
Top Bottom