Mtikila has extreme genocide ideology, says Kagame


Kikwete yupi, Ridhiwani au?
 

Hapana, hujaniudhi hata kiduchu. Huwa napenda kujadiliana na wewe.
Sasa tuanzie suala la Uganda na Idi Amin. Obote alipinduliwa akiwa kwenye mkutano wa Commonwealth Singapore ambako alikuwa kiongozi pekee kumuunga Nyerere mkono katika suala la Uingereza kuiuzia silaha Afrika kusini. Waingereza wangekuwa na uwezo wangempindua Nyerere lakini kwa sababu uwezo huo hawakuwa nao wakaona Obote ndiye weakest link. Nakumbuka waziri mkuu wa Uingereza wakati huo (jina linanitoka, labda unaweza nikumbushia, ilikuwa mwaka 1971) alisema pale kwenye kikao kuwa kuna baadhi yenu mnapaaza sauti hapa lakini hamtaweza kurudi nyumbani kwenu. Na kweli siku mbili baadaye Obote akapinduliwa. Hicho ndicho kisa kikubwa kilichomfanya Nyerere amchukie Amin (msimamo) Pili, Museveni wakati huo alikuwa mwanafunzi pale chuo kikuu cha UDSM (siyo muuaji) Na unakumbuka nchi ya kwanza kumkaribisha Amin ilikuwa Uingereza, mpaka pale alipowatimua Wahindi (1972 au 73) ndio waingereza wakamwona kuwa mtu wa hovyo. Hapo ndipo Amin alipopata marafiki wepya, Saudi Arabia na Libya. Sasa tukimlaumu Nyerere kwa mauaji yaliyotokea Uganda baada ya Museveni na Obote kurudi kwao, shurti pia tumlaumu basi kwa kumsaidia Mugabe kuingia mamlakani na kwa makosa ambayo Mugaba ameyafanya Zimbabwe. Is that fair?
 

Ruta,
Hebu tupatie hizo links za posts za Mtikila na Kagame ili tuweze kutoa maoni yenye uhakika na yaliyonenwa.
 
Wote Mtikila na Kagame hakuna wanaoishi karibu na ziwa Buligi wilayani Muleba...wanaoishi huko wameshashtaki kwa Kanali Masawe aka Mulokozi (RC Kagera) na magazeti yalishaandika juu ya unyama wanaofanyiwa wahaya na wasukuma wanaoishi huko. Kama Kagame amepata taarifa za watu hao ni dalili kuwa anajihusisha kwa namna moja na yanayotukia kule Buligi na Mtikila kama hakupata taarifa za magazetini basi ana agenda yake juu ya watu wa Buligi.
Si vema klia mtu akisemwa akaacha kuona sehemu yake kama wanavyosema nyani huwa haoni sehemu fulani ya mwili wake na akipaona anahisi pamefunikwa kwa vazi jekundu kumbe ndo utupu wake. Mtikila na Kagame tuachiene Tanzania yetu nanyi endelezeni siasa za wahutu na watusi mpate la kusemezana. Mbona mtikila aliweka simu yake kwenye uzi ule si ungempigia simu tu kuliko kuja hapa jamii forum kuonesha ujinga wenu
 
Jasusi, RUTAJUMBUKIRWA,

..I dont think this is about genocide.

..had it been about genocide, the western powers/"international community" would not have looked the other way while millions of Congolese ppl' were being slaughtered.

..the powers that supported Rwanda and Uganda incursions into Congo, are the same powers that have now turned around and are supporting SADC involvement in Congo.

..remember in the late 90s SADC sent a combat force to stabilize Congo and prevent the then government frm being toppled by Rwanda and Uganda armies. Now, tell me what has changed btn now and then??

..sisi wa-Tanzania tunakwenda na upepo tu. We are just following the cardinal rule of politics and international relations that there are permanent interests and not permanent friends.

..If Rwanda was OK with Tanzania supporting her in the late nineties, and going against SADC[Tz is a signatory of SADC defence treaty], then they should not be surprised that now we are supporting SADC.

..This is about how Congolese resources are going to be exploited and by which powers. Kagame should position his country according to that new reality.

cc: gombesugu, THE BIG SHOW, Kabaridi, Nguruvi3, zomba, Ritz
 
Last edited by a moderator:
Nimefurahi kujua pia Kagame ana vijana wake humu, hii ni muhimu sana kuona kuwa anapata feedback ya baadhi ya mambo na sio tunaandika tu kufurahishana wenyewe. Hili la Mtikila ngoja niupitie kwanza waraka maana kaandika sio mchezo, kisha nirudi...
 

Mzee Jasusi,

Nashukuru ndugu yangu,lakini imenilazim kucheka kiduchu.

Nakumbuka mara nyingi tunapojadiliana,explanations/excuses zako zinakua triangular!?

Nafikiri mimi nilikua nakujibu tu kiduchu ile hoja yako ya awali yakuwa Tanzania tunasifika kwa kuwa na msimamo thabit...ndipo ikanilazim kiduchu nigusie mfano wa Uganda kama ulivofanza wewe.

Kumbuka Nyerere alipinga kabisa na wala alikua hataki asilan kusikiza washauri wake binafsi wa karibu au Usalama wa Taifa ilipokua kuhusu khabar za Obote...sasa kwanini alikua akifanza vile!?

Matokeo yake; yale yoote washauri wake au hata Usalama waliyokua wakimkataza au kumshauri...ndio yale yale yaliyotokea wakti Obote aliporejea madarakani na alipokhis yakuwa nae muda wake wa kulipiza kisasi umefika!?

Kuhusu Museveni,wewe binafsi unajua yakuwa yule jamaa tayari aliaanza kuwa mtu mbaya na ana mipango mingi mno ya kinyama,tangia yuko pale UDSM.

Nakumbuka mara kadhaa kukutana nae kwenye ile ilokua mikutano ya MWAKENYA pale UDSM.

Nyendo zake zoote mbovu,Nyerere pia alifahamishwa na Usalama na washauri wake wa karibu, nafikiri mwanzoni hakutaka asilan kusikiza.

Kile kile kipindi alichoamuru hatimae Museveni afukuzwe nafikri ilikua tu ni kwasasabu ya fitna za Obote...na pia tunajua yakuwa Obote ndie aliekua favourite kwa Nyerere.

Hizo khabar za Mugabe,Nkomo na Zimbabwe...nafikiri mimi nawe tulishazijadili kwa utuvu.

Nafikiri unakumbuka msimamo wangu!?ahaha!!

Nachelea tusijerejea kule kule tutokeako!?

Kwa kifupi huu mjadala kwangu mimi binafsi ni mzuri mno,kuna kuna vitu vingi mno nachungulia na kujifunza upya.

Nisingependa kuchangia kwa kina,kwa wakti huu. Nakhis ni wakti muafaka kuwaachia wataalamu wengine nami niwasikize maoni yao.

Natanguliza shukran zangu za dhati pia kwa ndugu yetu JokaKuu kwa kunalika kwenye jamvi hili pia.

Ahsanta sana.

Cc;JokaKuu.
 

Sasa Tanzania mmepeleka jeshi la nini CONGO kama muwataalamu wa mazungumzo?
 
Ndugu yangu Gombesugu,
Huenda ni kweli Nyerere hakutaka kusikia ushauri wa maafisa wa usalama katika suala la Obote. Lakini kumbuka kuwa Nyerere aliamini kuwa Obote alipinduliwa kwa kumuunga Nyerere mkono katika mkutano huo wa Commonwealth. Kumbuka kwamba Obote alipopunduliwa kituo cha kwanza ilikuwa ni Kenya. Waingereza wakamwambia Kenyatta asimpe hifadhi.
Ungekua wewe Nyerere ungefanya nini? Fadhila ndugu yangu, fadhila. Haya hilo limekwisha. Obote aliporudi mamlakani mara ya pili alijikuta amesquander opportunities zake. Akapinduliwa tena. Akakimbilia Zambia. Nasikia mwenyewe anasema alipokuwa Narobi alimpigia Nyerere simu mara mbili bila kupata majibu. Kaunda akamchukua. Hebu jiulize ni kwa nini Nyerere hakumsikiliza Obote mara ya pili?
 

Jasusi embu rudi kwenye mstari....pamoja na msaada wetu bado vita haikwisha na RENAMO mpaka watu walipoamua kwa dhati kukaa kwenye meza ya mazungumzo. Sihitaji kutumia analogy ya RENAMO bali wewe ndio ulileta mfano wa RENAMO, ila pia ni ukweli ulio wazi kuwa wapiganaji wengi wa FDLR ni wale waliokuwa recruited ukimbizini na ukweli unafahamika kuwa wengi wao hawakuhusika na genocide. Pili kuna mifano mingi ya makamanda wa FDLR ambao waliamua kujisalimisha na kurudi Rwanda, sasa cha ajabu pamoja na propaganda zote hizo kuhusu FDLR hakuna hata mmoja ambaye aliporudi alifunguliwa mashtaka ya genocide badala yake wengine wameingizwa jeshini na kupewa vyeo, wengine wamepewa kazi nyinginezo. Kwa hivyo kusema FDLR ni watu waliohusika na genecide ni propaganda tu ya kunyamazisha baadhi ya watu kama wewe muendelee kutishwa na yale yaliyotekea 1994! Pili uwezo wa Kagame ku-deal na FDLR ni mdogo kwa vile uhalisia ni kuwa kwa Rwanda mhutu yeyote anayeishi Congo ni FDLR na mhutu yeyote popote alipo nje ya Rwanda ni supporter wa FDLR, kitu ambacho si kweli. Kwa sasa mashariki ya Congo kuna vikundi vingi vyenye silaha vya kikabila kwa ajili ya kujilinda kutokana na hali ya kiusalama kuwa ndogo mfano Raia Mutomboki, sasa kwa vikundi vya namna hiyo vikihusisha wahutu pia basi vinaunganishwa kuwa ni sehemu ya FDLR kwa mtazamo wa kipropaganda wa Rwanda. Nimekuwekea ramani hiyo uone makundi ya wapiganaji yaliyopo Congo kwa sasa.....ingawa mengine yanakosekana.
 
Asante kwa ramani. Asante pia kwa maelezo yako. Kumbe unajua mengi zaidi juu ya Rwanda kuliko ilivyoonekana. Kumbe kuna wapiganaji wa Kihutu ambao wamerudi nyumbani na kuingizwa kwenye jeshi la nchi. So far so good. Sasa ningependa kujua malengo ya FDLR. Are they just a political party or are they also a military? Nchi haiwezi kuwa na majeshi mawili kukawepo amani. Ndio maana nilitoa mfano wa RENAMO. Renamo ceased to be a military force and became a political party. That is why there is peace and development in Mozambique. Is FDLR willing to go through the same metamorphosis?
 

Watusi mmezoea kumuona binadamu mwenzio kama si binadamu solong as siyo mtusi.Eti rais ana girl friend, sishangai maana ndiyo dharau zenu
 
Watusi mmezoea kumuona binadamu mwenzio kama si binadamu solong as siyo mtusi.Eti rais ana girl friend, sishangai maana ndiyo dharau zenu

Kaka, mimi si mtusi, unless unataka niwe born again.
 
Kaka, mimi si mtusi, unless unataka niwe born again.

Wewe na Kobe sasa ameongezeka Rutajumbirwa nyie ni tutsi extremist mnaona kama Kagame is your everything lakini mnasahau kuwa ile kazi ya 1994 ikuwa ya CIA kwa hiyo for sure mlianza na CIA na mtamaliza na CIA kama alivofanya Savimbi.That is how western play
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…