MTIKILA: CCM ni Manyani - Epidomea

MTIKILA: CCM ni Manyani - Epidomea

Sayansi hii ya 'epidomia' ni ngumu sana kwa Ma-CCM kuielewa, na hawakamii kuanza kulalamika kwa JK katukanwa, kakashifiwa na kazalika...! Tatizo lao ni woga na wigo wao wa fikra wasiopenda kuupanua na kujitawala kutokana na wanavyotawaliwa kifikra...ndiyo 'epidomia' yenyewe....unyani 🙂!
20250221_210713.jpg
 
Akihutubia maelfu kwa maelfu ya watu wa visiwa vya Pemba jana alianza kwa kusema ''Saa ya ukombozi imefika'' akaendelea kumwaga vitu kama ifuatavyo:-

''Siku 1 mi mwenzenu ni mchungaji kule uingereza niliwauliza maaskofu wenzangu kwamba sisi sote kama si wanafiki kwanini mulisema sisi watu weusi ni nyani? Askofu 1 akanijibu aliokuambia hivyo hakukumalizia kulikuwa na biashara ya utumwa kwaiyo vyuo vikuu vya uingereza vya kanisa vilikaa vikavilamisisha serikali lazima ziende vikavunje ile biashara ya utumwa afrika na kukomesha biashara ya utumwa afrika''

''Kwaiyo walipofika afrika wakarudi kutoa majibu kwamba wale watu si binadamu halisi kwa sababu wanauzana wao wenyewe kwa wenyewe kwa tende na halua''.

''Kiongozi anachukua watu akishaonjeshwa anauliza je mtanipa kiroba? Ndio! kwaiyo anatoa amri wanakamtwa walalahoi waliokuwa wanalima wanakwenda ambako hawatarudi''.

''Ndio maana tumeona tutoe ripoti askofu akatumabia hawa ni binadamu wenzetu ila wanahitaji elimu, dini safi manake hata na sisi tulikuwa watu wa pangoni''.

''Sasa tatizo ni tofauti kati ya wadamu na wanyama ndio tulioizingiatia ila waliumbwa kwa roho ya uhanga ila wao wanauza utu wao wanakwenda utumwani halafu hawarudi''.

''Kuna lile gonjwa linaitwa Epidomia. Ukimuona mtanganyika hajali utaifa wa wana utanganyika kwa sababu anapata pesa, utawala, anataka chochote basi ndio ule ule unyani wa siku zile''.

''Unaweza kumuona mtu mwenye unyani anasindikizwa na mapikipiki lakini yuko tayari apate madaraka kwa watanganyika dodoma asikubaliane na wazanzibar, awafanye wazanzibar wanavyotaka wenzake kule Dodoma, ni sayansi ya kweli. Mtu huyu ana tatizo la unyani, anayo Epedomia''.

''Kinacho wasumbua serikali 2 serikali 2 ni unyani (Apedomia). Matatizo ya Jakaya kikwete ni makubwa sana na tatizo ni lile lile la Epedomia''.

Akaendelea kusema Kikwete anasema Jeshi litachukua nchi amesahau kuwa hao hao wanajeshi kuna ndugu zao ambapo kila mtu ana ndugu mwanajeshi si rahisi jeshi kuja na kumtawala ndugu yake na kumtesa akasema pia Rais JK kuwa na mawazo hayo ni tatizo la Epedomia (Unyani).
Alikuwa sahihi,yaangalie manyani ssa hii Singida
 
huyu jamaa alikuwa ni mwingi sana, ila watanganyika hawakumuelewa, mana wao always mihemko ndio wameeka mbele
 
Back
Top Bottom