Mtikila awasafisha Warioba, Sumaye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila awasafisha Warioba, Sumaye

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mahesabu, May 4, 2011.

 1. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  :israel:Na Moshi Lusonzo
  1st May 2011
  [​IMG] Asema ni wasafi ndani ya CCM
  [​IMG] Wanastahili kuongoza nchi na chama
  [​IMG] Viongozi Chadema siyo wasafi  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Chama cha Democraty party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila


  Mwenyekiti wa Chama cha Democraty party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amefyatuka na kuwasafisha mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Warioba na Fredirick Sumaye kuwa ni wasafi ndani ya CCM na wanastahili kuongoza nchi na chama hicho.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Mtikila alisema kitendo cha CCM kuamua kujivua gamba hakitakuwa na maana kama watu hao wataendelea kuzibwa mdomo na kuachwa kuwekwa katika nafasi muhimu katika nchi hii.
  Alisema, ndani ya CCM kuna viongozi wengi ni mafisadi na wanaonufaika na raslimali ya nchi, hivyo upo umuhimu kwa Chama hicho kuamua kikamilifu kuwaondoa viongozi wote mafisadi wakiwemo viongozi wa juu na kuwaacha watu waadilifu na wenye uchungu wa nchi ambao ni wachache ndani ya CCM.
  Kati ya watu ambao alisema sio mafisadi na wana uwezo mkubwa wa kuongoza nchi na CCM kama wakipewa nafasi mbali ya Sumaye na Warioba ni Naibu wa Wizara ya Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
  Alisema kwa makusudi zimejitokeza njama ya kuanzishwa kampeni ya kuwaziba midomo ili wasiendelee kusema kile wanachoamini hakiendi kwa misingi ya haki.
  "Nadhani kujivua gamba kama wanavyoeleza CCM hakutoshi kama viongozi wote mafisadi hawataondolewa na kubaki watu wenye uchungu wa nchi ambao kwa makusudi wanawazibwa midomo ili wasionekane kwa wananchi," alisema Mchungaji Mtikila.
  Aliongeza "Yule Jaji Warioba na Sumaye nawajua sana licha ya kuwa ndani ya chama kilichojaa mafisadi, lakini hawa ni wasafi wana uwezo mkubwa wa kunusuru nchi hii," alisema.
  Hata hivyo, alisema bado hataweza kuomba radhi kwa kitendo cha kumuita Sumaye kuwa fisadi wakati alipokuwa Waziri Mkuu, kutokana na wakati huo hakuwa na uwezo wa kupinga vitendo vilivyokuwa vikifanywa vya kuiibia nchi kwa kuogopa kuondolewa madarakani.
  Alisema kwa muonekano halisi CCM imeanza kuugua ugonjwa aliouita `Ndambulila' ambapo mtu anaonekana amekufa akiwa bado yupo hai, hivyo CCM imeanza kufa huku viongozi wake wakikitizama wasijue la kufanya.
  Mchungaji Mtikila alisisitiza kwamba kujiuzulu nyadhifa zao kwa Rostam Aziz, Edward Lowassa na Endrew Chenge wanaotuhimwa kuwa mafisadi sio suluhisho la kuondoa gamba bali kinachohitajika kwa viongozi wote wanaoonekana kuwa magamba kuondoka haraka.
  Alisisitiza kwamba kwa hali siasa inavyoonekana nchini, upepo wa mageuzi hautakikumba CCM pekee bali hata Chadema kuna dalili ya kuwepo mageuzi makubwa kutokana na viongozi wakuu wa chama hicho kutokuwa wasafi.
  "Suala la mageuzi linakuja kwa lazima na sio matakwa ya uongozi wa juu, mapambano haya hayataikumba CCM tu hata Chadema kuna vuguvugu la watu wasiotaka ufisadi kukataa kuongozwa na viongozi mafisadi," aliongeza.
  Akizungumzia juu ya mabadiliko ya Katiba, Mchungaji Mtikila alisema DP kinataka mjadala wa Katiba mpya uwe na uwanja mpana wa kujadili kwa kina juu ya Muungano pamoja na kuondoa madaraka makubwa kwa Rais wa nchi.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Kavuta chapaa za Sumaye tayari
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hapigi msuba huyu kweli?
   
 4. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #4
  May 4, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Other issues no Comment, lakini napingana naye kwa kusema viongozi wetu wakuu si wasafi. Hapo si kweli. Sisi huwa kwenye vikao vyetu tuko makini. Viogozi wetu ni wasafi.
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Hii habari imeshaexpire, inaonekana mtoa mada alikuwa kijijini.
   
Loading...