Mtikila atinga mkutanoni kwa Bajaj

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila juzi alikuwa kivutio kwenye semina ya ripoti ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mpango wa Kutathmini Utawala Bora nchini (APRM) baada ya kuwasili sehemu ya mkutano huo akitumia usafiri wa pikipiki ya matairi matatu, maarufu kama bajaji...
Tukio hilo lilitokea katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati mwanasiasa huyo machachari alipoingia na pikipiki hiyo ya miguu mitatum usafiri ambao umetokea kupendwa na wakazi wa jijini Dar es salaan kutokana na unafuu wake wa bei na uwezo wa kukwepa foleni.

Mtikila aliwasili kwenye eneo hilo majira ya saa 3:00 asubuhi akiwa amevalia suti na mkononi akiwa ameshikilia mkoba wa nyaraka (briefcase), huku watu waliobahatika kumuona,

wakiwemo washiriki wa semina hiyo, wakivunjika mbavu.

Nilichukua bajaji ili niwahi kwenye mkutano kwani niliona nimechelewa sana, alisema Mtikila ambaye aliwahi kufanya kampeni za urais mwaka 2005 kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kutumia pikipiki.

Mtikila aliiambia Mwananchi akisema: "Bajaji ina uwezo mkubwa wa kupita kwenye kona mbalimbali na hivyo kumfanya mtu afike kwa haraka zaidi."

Kiongozi huyo wa DP alifafanua kuwa kama angetumia gari angeweza kuchelewa kwenye semina hiyo aliyoiita kuwa muhimu kwa taifa.

"Bajaji ina uwezo wa kupenya hata pembezoni mwa barabara na kumfanya mtu afike kwa uharaka zaidi sehemu anakoelekea na kwa kuwa niliona nimechelewa kwenye mkutano huo, niliona njia pekee ya kuwahi ni kutumia bajaji," alisema Mtikila.

Mtikila aliusifia usafiri huo na kurusha kombora kwa viongozi wa serikali akisema kuwa bajaji ni muhimu hasa katika kipindi ambacho nchi haina viongozi wanaojali shida za wananchi.

"Matatizo hayo yanaonyesha kuwa rais wetu hana sifa ya kuongoza nchi na hii inaonyesha kuwa ameshindwa kusimamia mambo mbalimbali ya nchi," alisema Mtikila.

Ndani ya ukumbi wa mikutano, Mtikila alikuwa wa kwanza kunyosha mkono ili atoe hoja na alipopewa nafasi alipendekeza semina hiyo iwe ya siku mbili badala ya siku moja.

Alitoa pendekezo hilo baada ya katibu mtendaji wa APRM, Rehema Twalib kusoma ratiba iliyoonyesha kuwa mkutano huo ungefanyika kwa kutwa nzima ya juzi na kumalizika siku hiyo.

Ndugu washiriki kwa vile vitu ambazo vitajadiliwa hapa ni vya muhimu na vinagusa taifa letu, ingelikuwa vizuri zaidi kama semina hii itafanyika kwa siku mbili ili watu waweze kujadili mada mbalimbali kwa ufasaha zaidi," alipendekeza Mtikila.

CHANZO: MWANANCHI
 
Mtikila is the man of the time, uwa afichi neno , anaesma yote moyoni. Hadi sasa tunashuhudia anavyo mnanga rais adharani na akiwa na ushindi mkubwa wa mahakama ya rufaa dhidi ya Mgombea binasi
 
Back
Top Bottom